Tanzania ya viwanda

Tanzanite klm

JF-Expert Member
May 7, 2013
453
376
Kama wanasayansi wakubwa ,wana mahesabu, ma engeneer ndio hufanya taifa liwe taifa kubwa basi urusi mpaka leo ingekua taifa kubwa na tajiri, kama ni wanafalsafa basi ugiriki bado ingekuepo kwenye ramani ya dola kubwa duniani, sio kwamba hao watu hawaitajiki la hasha wanachukua nafasi ya pili baada ya biashara.

Ili taifa liendelee na liwe super na liweze kuleta utajiri kwa wananchi wake basi jambo la kwanza la kupewa kipaumbele ni biashara.

Serikali inabidi ipunguze utitiri wa kodi na kutoa mikopo nafuu kwa wafanya biashara.
Wingi wa kodi huuwa viwanda biashara na kukimbiza wawekezaji.

STEGLER GORGE.
Kuelekea Tanzania ya viwanda serikali haina budi kuharakisha mradi wa stiglers gorge ili garama za umeme ziwe chini zaidi ili basi watanzania kupitia viwanda vyao vikubwa na vidogo dogo waweze kuzalisha bidhaa nyingi ambazo zitauzwa kwa pesa ndogo sokoni maana production cost itakua ndogo hata ivyo pia garama za umeme zikiwa chini zaidi itasaidia wawekezaji wengi kuja zaidi kuwekeza.

Serikali ya Tanzania imejitahidi mnoo katika ujenzi wa miundo minu ya barabara amabayo ni kama mishipa ya damu ya uchumi, na sasa inaenda kwenye miundo mbinu ya reli na anga sasa, ni mambo mazuri kwa uchumi mkubwa.
Nchi ya ufaransa inazalisha umeme amabao ni mara 1164 zaidi ya nchi zote zilizopo chini ya jangwa la sahara ukichanganya kwa pamoja. Its a SHAME.

LAKINI pia Tanzania ina wataalamu wa kutosha lakini katika karne hii 21 nchi doesnt need kuwa na experts wote ili uweze uweze kufanya kila kitu unaweza uka hire, .

NUCLEUR PLANT FOR ELECTRICITY.
NI nchi nyingi tuu zina zalisha umeme wa nyuclear hii haina amdhara hata kidogo endapo tutafuata kanuni na masharti ya shirika la atomiki duiani, kwa kushirikiana na ndugu zetu wachina chini ya BELT AND ROAD INITIATIVES hawa jamaa wanaweza kutujengea kinu kimoja cha nuclear cha kuzalisha umeme, hapa tutakua tumelamba karata dume.
kwanini unafikiri haiwezekani?

ni kwasababu ya mfumo uliobuniwa vizuri wa kukufanya uwe nanguvu za mwili za kutosha na psychologically weak. Yanawezekana.

BILA YA KUWA NA UCHUMI IMARA BASI TUTAENDELEA KUWA NA ELIMU MBOVU NA KUTOA WASOMI WENYE HASIRA KALI MAANA WANAMALIZA VYUO HAKUNA KAZI NA WALA HAWANA UWEZO WA KUJIAJIRI.
UCHUMI BORA HULETA TAIFA LENYE WANANCHI WENYE FURAHA NA UPENDO,UPENDO BAINA YA WAO NA WAO NA KUMPENDA MUNGU.
NAOMBA KUWASILISHA.
 
Tukiwa na maingineer, madaktari wanauchumi nk wengi wa zuri wanaweza kupata kazi sehemu yeyote ile duniani na kuchangia kuleta maendeleo nyumbani. Dunia imekuwa kijiji kidogo, sikuhizi unaweka cv kwenye internet asubuhi kama unauzika saa tano unapigiwa simu kutoka Bangkok au au Ottawa kwa Skype interview na okienda vizuri mwisho wa wiki una ticket yako.
 
mazingira ya biashara inabidi yaboreshwe ikiwezekana iondolewe kodi kwa biashara zinazooanza hata kwa muda wa miezi 12
 
Tukiwa na maingineer, madaktari wanauchumi nk wengi wa zuri wanaweza kupata kazi sehemu yeyote ile duniani na kuchangia kuleta maendeleo nyumbani. Dunia imekuwa kijiji kidogo, sikuhizi unaweka cv kwenye internet asubuhi kama unauzika saa tano unapigiwa simu kutoka Bangkok au au Ottawa kwa Skype interview na okienda vizuri mwisho wa wiki una ticket yako.
kabisa tuaeza waajiri hao wataalamu wakaja ku run projects zetu kama vile dubai wazungu wanavyofanya kazi pale
 
kabisa tuaeza waajiri hao wataalamu wakaja ku run projects zetu kama vile dubai wazungu wanavyofanya kazi pale
Kabisa si mbali sana Wakenya wengi wapo U.N. na Ulaya wakifanya kazi professional. Mpaka U.N. nafasi nyingine wanaweka kabisa specific for a Tanzanian maana jamaa wakiona tu wanatuma CV hata projects za Kasulu na Nachingwea huko.
 
Tukiwa na maingineer, madaktari wanauchumi nk wengi wa zuri wanaweza kupata kazi sehemu yeyote ile duniani na kuchangia kuleta maendeleo nyumbani. Dunia imekuwa kijiji kidogo, sikuhizi unaweka cv kwenye internet asubuhi kama unauzika saa tano unapigiwa simu kutoka Bangkok au au Ottawa kwa Skype interview na okienda vizuri mwisho wa wiki una ticket yako.
Mama tufanye mchakato basi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom