Tanzania ya viwanda: Another failure at first place

Tanzania ya viwanda: Another failure at first place

Tusi lipo wapi!? Je wewe ni mmoja wa MANIFESTO ile!?
Kweli tuna watz wagonjwa wewe mmoja wao, hii ni hoja na wala siyo shambulizi kwa serikali wala kwa mtu. Upo ugumu ktk utekelezaji wa sera ya viwanda, huku ukiwa huna mitaji, elimu na sera iliyo wazi kwa uwekezaji, wa ndani na huo wa nje. Hujui utauza wapi, hujui utashindana vipi, huwajui wanufaika muda utatuambia kama ni mapenzi basi wewe kwa ccm umekufa kuoza kila saa hila na matusi
 
hii iikiendelikiendelea itakuwa ni kwa Mungu.Haiwezekani jana Kilimo kwanza,mara BRN...leo yamefukiwa ,yamefukiwa Tsnzania ya Magafuli viwanda na diabomba-! Tulikuwa na mradi wa Katiba umekufa!,Leo NSSF,na wameanza eti kwameankuwekeza viwanda,walifanya lini haya maandalizi?weledi wanao?!

Kwanza Unapaswa kufahamu kuwa Tanzania ya Viwanda sio Sera ya mtu mmoja isipokuwa Ni muendelezo wa MIPANGO ya serikali . Awamu ya 4 ilisimamia kilimo na baada ya kilimo kukua MIPANGO ilikuwa ni kusimamia Ukuaji wa viwanda ili Nchi iweze kuongeza thamani ya bidhaa kabla ya kuuza NJE eg MADINI au Korosho zilizopita kiwandani kuchakatwa na kuongezewa thamani bei yake kubwa NJE ya Nchi kuliko Korosho inayouzwa kama ilivyotoka shambani.
Pia VIWANDA vita ongeza ajira kwa Vijana wetu wengi. India waliweza kuweka mkazo kwenye ubunifu wa machine za viwanda vidogo na vya kati. Mafundi mchundo wa gerezani wakiendelezwa au Veta wakiendelezwa kwa kupewa exposure ya India, China AU Ujerumani wanaweza wakaja na machine modern mkashangaa. Machine za kubangulia korosho, kukamua mafuta ya Alizeti, pamba, ufuta, machine za kutengeneza Nyuzi, kusaga mazao etc. viwanda vidogo vinaweza kuleta ajira kubwa ajabu ktk kipindi kifupi cha miaka 5-10. Wakati huo huo tukiwa tunatafuta foreign direct investments za type ya kina Dangote, Trump etc kwa kuwawekea vivutio.

Serikali iwekeze kwenye elimu ya ufundi. Ipeleke Vijana China , India, Ujerumaniwakajifunze hata kozi za mwaka mmoja mmoja wale wenye ujuzi kidogo wakipata exposure wakirudi wanaweza kubadili mambo.

Malaysia ina peleka Vijana wengi sana Uk, USA, Australia, China, India kujifunza teknolojia mpya. Tusibaki tunajifungia tu humu wenyewe bila kuwa na sera ya kujenga ujuzi wa Vijana wetu Nchi zilizoendelea. Tuwe na program ya kuchagua best 100 science students tuwatawanye Nchi zilizoendelea, tuwalipie gharama za masomo na kuwasainisha mkataba kuwa wakimaliza wanarudi kuleta ujuzi na huo ujuzi uheshimiwe na tujue tunawapeleka wapi wautumie ujuzi wao kwa faida ya nchi.

ELIMU ya ufundi ni chachu ya Tanzania ya viwanda. Then unawezajua Market iko wapi. Bila ya kuwa na quality products huwezi jua soko liko wapi.


Tunanunua viatu, mikanda ya ngozi, pochi toka China. Tuna ngozi kwanini tusijenge viwanda vya kisasa vya vitu hivyo hapa nchini ambapo soko lipo. Tuna import vitanda, sofa etc Sababu quality ya vyetu Si nzuri. Tunanunua gypsum boards toka Thailand wakati tuna raw material ya gypsum kibao lakini ujuzi wetu hauwafikii wa Thailand. Vitu ni vingi mno. Tujiongeze. Kama National Development plan itasimamiwa vizuri ndani ya 5 years tutasogea.
 
Mbona viwanda vipi zaidi ya 7000 vya kufyatua matofali na washing nguo..?
 
Mnataka viwanda gani jamani.mwijage alishataja viwanda vinavyotakiwa.
 
Mkuu Allen Kilewella labda niweke senti moja kwa uchache. Kwanza, mleta mada kaleta mada nzuri tu inayotugusa kama Taifa na wananchi. Haya ndiyo mambo ya kujadili ingawa yanavurugwa makusudi

Mag3 alileta uzi 'kelele' zinavyotumika kuua hoja za msingi

Nikirudi kwenye mada, mletaji kasema nchi za viwanda ziliwekeza katika human capital

Hoja hii inaeleza kwanini ''viwanda'' tulivyokuwa navyo vichache vilikufa.

Hakuna postmortem wala utafiti wa kisayansi unaojibu hoja hiyo.
Ndipo tunakwenda katika hoja ya mleta mada nyingine

Research and Development: Hii inaeleza kwanini tunahitaji viwanda na kwasababu zipi, katika soko gani na tutawezaje kukabaliana na ushindani.

Pia inaeleza gharama za uzalishaji na jinsi ya kukabiliana na bidhaaza bei rahisi

Tatu, kuna suala la nishati.
Je tutaweza kuwa na nishati ya uhakika na nafuu itakayokidhi gharama za uendeshaji?

Kumbuka nishati ni factor kubwa katika kuamua gharama na uzalishaji
Ikiwa hatujaweza kusambaza gesi, kwa miaka 4 tutawezeshaje viwanda?

Nne, katika region integrations na globalization tutalindaje viwanda tarajiwa?
Kama tutafanya protectionism,tutaweza kumlinda consumer asiwe victim?

Hayo ni kwa uchache,yote yapo katika mwamvuli wa jambo muhimu tusilotaka kuliongelea ambalo ni Dira ya Taifa.

Dira na sera ni vitu viwili tofauti. Hapa tunaongelea vision na policy, na kwamba sera lazima zi reflect dira irrespective ya nani au chama gani kinakuwa madarakani

Wanatuambia wameandika sera ya viwanda ni kwa kutumia dira gani?
Tulikuwa na elimu kwa wote, ikaja kilimo kwanza na kuua sera ya elimu.

Ghafla kama walivyosema wachangiaji wengine BRN na sasa sera za viwanda.
Policy hizi zina reflect dira gani ya Taifa?

Pengine kushindwa kwa viwanda kutatokana na mambo mengi, kubwa ni siasa.

Tatizo letu ni kutokaa pamoja kama Taifa na kupanga kisha kuchagua tunataka nini.

Hatuna hamasa ya kujifunza kutokana na makosa yetu (retrospective) na tunaendesha mambo kisiasa kuliko utaalamu.

Tungerafuta kwanza, kwanini Tanganyika packers, Mutex, Mwatex, Mgololo, Kilimanjaro match box, Tanalec, General tyre, Moshi machine, Mangula Machine, Moro polyester, Morproco n.k. n.k. vilikufa tukipata jibu tuanzie hapo

Je, hatuna pamba ya kutosha, hatuna wavaaji wa kutosha, hatuna magari ya kutosha, hatuhitaji vipuri n.k.

Jibu rahisi ni ndiyo kama ni hivyo tulifeli wapi na je sababu za kufeli tumezibaini na kuziondoa?


Kwanza kabisa mleta mada mleta mada amefeli hatua ya kwanza tu. Nawewe hapo hapo ukaingia kwenye mtego wa kufeli vile vile.

Kuti cha kwanza mlichofeli wote mmeandika tungo kama hadithi ambavyo havina references zozote.
Unapoanza kueleza sera na dira za nchi ni vyema ukaziweka hapa ili kila mmoja amweze kuzisoma na kuzielewa aweze kuchangia.
Sasa unapotoa maneno matupu kutoka kichwani mwako bila references watu wenye akili timamu watajua tu kuwa wewe ni mchawi fulani una ajenda nyuma ya taarifa yako. Mtu kama GT hawezi kuongea maneno matupu tu.

Kwanza tembelea katika tovuti ya ofisi ya raisi kuhusu mipango hapa:
http://www.mipango.go.tz/
Hapa kuna mambo mengi utajifunza na kujua ili uwezekutoa duku duku lako usikilizwe ukiwa kwenye mstari.

Kisha soma hapa 5 years plan ya taifa

Vile vile unaweza kutembelea hapa
Tovuti Kuu ya Serikali: Dira 2025 Upate dira ya taifa ifikapo mwaka 2025.

Ukija kwenye upande wa sera zipo sera nyingi tu ambazo lengo lake kubwa ni maendeleo ya jamii. Kuna sera zilizotungwa mda mrefu uliopita na zipo zinazoendelea kutungwa na kuboreshwa.


Jambo ambalo limenishangaza kwako ndugu yangu ni kuhusu kuwa na kikao cha pamoja kama taifa. Hapa sijui unaongelea nini? Sijui unataka tuwe na mkutano mkuu wa nchi nzima. Sijui tutakaa wapi watu mil50.
Hujui kuwa wabunge ndio wanaowakilisha wananchi? Hujui bungeni kuna kamati mbalimbali kazi yao ni kuwa karibu na serikali katika utungaji wa sera. Ndio maana kuna wizara ya Sera na Bunge. Wizara hiyo moja ya kazi yake ni kuunganisha Bunge na serkali. Kwahiyo sera zote na utekelezaji wake wananchi wanajua kupitia wabunge wao. Ambao ni wawakilishi wao.

Halafu jambo la pili:-
Viwanda vilivyo kufa ni kutokana na sababu nyingi tu. Moja wapo ni vita baridi kati ya Nchi za kijamaa na nchi za kipepari. Ambazo nchi kubwa za USSR na Marekani ziliingia katika vita baridi. Kitendo cha kuanguka kwa dora ya kisovieti ilisababisa madhara makubwa kwenye nchi yetu. Na ikichukuliwa nchi yetu ilikuwa bado changa. Na kuna vitu vingi tu vilitokea kipindi kile bila hata ya kuhusianisha na vita ya kagera.

Kwahiyo Ile industrial revolution ya Ulaya ni ya kipindi kile hatuwezi tukaanza kulima kwanza kisha tuanzishe viwanda. Ni lazima kuvifungamanisha vyote kwa pamoja.
Ndio maana sasa Uwekezaji mkubwa katika Umeme unafanyika. Ndio maana ikaanzishwa REA kwaajiri ya kusimamia usambazaji wa umeme vijijini. Kuna mkongo mkubwa wa umeme ambao unamalizika sio mda mrefu wenye uwezo wa MV 400. Unaunganisha nchi ya Zambia Tanzania Kenya. Kiasi kwamba Tanzania inaweza kutoa au kupata umeme toka nchi za Zambia na Ethiopia.

Lile jambo la kuiweka Reli ya kati kuwa Stadard ni moja ya kufungamanisha usafirishaji na viwanda. Ujenzi wa barabara usiesme chochote kwaajiri ya usafiri. Ni mambo mengi tu
 

Attachments

Mtanzania wa kawaida, ambaye anawakilisha kundi la walio wengi, hawezi kununua hata juice ya Azam. Ushindani wa masoko ya nje ni mkubwa mno; sidhani kama tutauweza kwa miongo kadhaa ijayo. Kundi la Watanzania walioweza kununua hata hizo juice linapungua kutokana na serikali kubana matumizi etc; halafu sijui wanadhani hizo bidhaa za Tanzania ya viwanda watamuuzia nani!
Mtanzania wa kawaida, ambaye anawakilisha kundi la walio wengi, hawezi kununua hata juice ya Azam. Ushindani wa masoko ya nje ni mkubwa mno; sidhani kama tutauweza kwa miongo kadhaa ijayo. Kundi la Watanzania walioweza kununua hata hizo juice linapungua kutokana na serikali kubana matumizi etc; halafu sijui wanadhani hizo bidhaa za Tanzania ya viwanda watamuuzia nani!
Ni kweli mkuu...wengi wananunua juice ya shilingi 100 inayowekwa kwenye chupa za maji zilizotumika. Kwa kweli tunahitaji mipango na mikakati madhubuti ili kufikia kuitwa Tz ya viwanda...
 
Tz itabaki dampo la bidhaa za nchi za magharibi
 
Tz kufanikiwa ni ngumu sana mimi huwa nakwenda Zambia na kamtaji kangu ka nyanya nanunua bidhaa sample 4 nakuja nazo dukani kufila boda wananiambia unahitaji kuwa na IMPORT PERMIT masharti yake kila bidhaa unazotegemea utakuwa unaingiza upeleke 5pcs TFDA kanda waende wakale ili wajue kama ni bidhaa tam je, wamenisha nifilisike au vipi¿
 
Stimulus package muhimu, huwezi kuwa unabana matumizi, mishahara midogo halafu unataka muwekezaji aje hapa, wananchi masikini bidhaa hazitanunulika
hii ni moja ya setbacks ya hiyo dream ya Tanzania ya viwanda
I wish huyu jamaa angekuwa anafanyiwa consultation hata monthly
 
Kitulo kuna hoja imetolewa kwamba kabla ya kuuza nje ni lazima kwanza kujenga uwezo wa watanzania kwenye kununua vitu vitakavyozalishwa nchini. Lakini inaonekana kama vile kuna mpango mahsusi wa kupunguza uwezo wa watanzania kwenye kununua.
Uwezo wa kununua utachochewa na ajira katika hivyo viwanda na ongezeko la uzalishaji mali hasa kwa vijana kuanzisha ajira binafsi kama kufuga samaki na nyuki ambvyo vitapelekwa viwandani kuchakatwa.
Nia ipo pale pale kamanda Allen Kilewella
 
Jambo la kwanza kabisa ni lazima tuelewe nini maana ya Tanzania ya viwanda? Kama hatujui nini maana yake, basi kila mtu atakuwa anaongea kutokana na anavyofikiria yeye.

upload_2016-12-12_2-56-19.png


Kwa hiyo, kifungu (i) ndicho watu wanachokishikia bango. Kifungu hicho basically kinamaanisha kuwa kuiondoa Tanzania katika mfumo wake wa sasa wa kiuchumi (Agrarian ) na kuwa Industrialized. Lakini, kwenda kuwa industrialized, you have to pass through some stages.

Ndiyo maana, by 2025 Tanzania ina lengo la kuwa semi-industrialized country (mind you, not industrialized). By 2020 haya ndiyo malengo.

upload_2016-12-12_3-34-6.png


upload_2016-12-12_3-36-28.png


Haya malengo yakifikiwa kwa miaka mitano ijayo, siyo kwamba tutakuwa semi-industrialized Nation, tutakuwa kwenye transformation ya kuelekea kwenye semi - industrialized economy.

According to UNIDO, nchi zimekuwa categorized based on their CIP ( Competitive Industrial Perfomance Index) itafikia 0.01 Tanzania Ina 0.007. Pia ni lazima iwe out of Least Developed Nations (LDCs) yaani GDP iwe above 1045$ per capita.

Sasa baada ya kukubaliana na hayo au kurekebishana, labda niyo tunaweza kuanza kujadiliana jinsi muelekeo ulivyo. Other than that tutakuwa hatuna jinsi ya kupima tulipo na tunapoelekea.
cc. Allen Kilewella , Nguruvi3 , barafu , Eric Cartman , ycam
 

Attachments

  • upload_2016-12-12_2-55-37.png
    upload_2016-12-12_2-55-37.png
    68.3 KB · Views: 36
Binafsi ninapousikia huu usemi napatwa na kigugumizi ,kwa elimu yangu ndogo hii ya uchumi katika dunia ya utandawazi nina maswali mengi kushinda majibu kwa mfano

1.Viwanda vinavyotajwa kwenye makaratasi na mikutano mbalimbali ikitokea vikazalisha bidhaa tutauza wapi? (Market ya products at global level) Je tuta charge tarrifs na quotas kubwa bidhaa za ulaya na Mashariki ya mbali ili zetu ziuzike?

2.Swali la pili sambamba na swali lililopita ,hatuna technology, wala Reseach and deveopment centres ambazo ni nyumba ya innovations na technological capabilities so we depend totally on imported technology and machines. Tutawezaje kupambana katika soko na watu ambao wametuuzia technology? (assume machines tunazo however the fact hatuna) huu sio mpambano wa Tembo na sungura?

3.Swali la tatu historia inaonyesha nchi zote zilizoendelea kiviwanda waliwekeza kwenye rasilimali watu (human capital) tena kwa muda mrefu tu ,itawezekana vipi hii paper policy itekelezelezwe ndani ya miaka mi 5?

4.kwa wanaojua maana hasa ya Globalization is an attemp to make African countries to be primary producers wa raw materials hii ni moja ya objectives zao major political global powers hili halina ubishi utandawazi ni ubepari !hivyo basi kutangaza viwanda kwa nchi za ulaya na East Asia ni kutangaza vita ya masilahi tumejiandaa vipi kukabiliana na hili?tulijifunza kweli kwenye sera ya ISI pilicy ambayo tuli adopt soon after independence ikafa tukajaribu Export promotion industrialization ikafa kibudu ikafuata ujamaa policy then import liberalization na sasa SIDP?

5.Ushirikishwaji wa nchi za kiafrica zingine katika kuunda efficient regional integration and cooperation kwa kuwa na common markets ,free trade areas na ku charge ushuru mkubwa bidhaa za nje ya ukanda ili viwanda vya nyumbani (infantry industry) vikue kama wanavyo propose "Prof viners pure theory of international trade " na kuongeza bargaining power as a regional bloc ukoje na tumehamasishaje?
Au Tanzania as a single countrypeke yake
itazuia soko lake kuuzwa bidhaa kutoka nje ya nchi kama ilivyotokea mwaka 1667 nchi za ulaya walipozuia marekani wasiingie bidhaa za chuma Europe?

6.Aliyetunga sera ya viwanda kupitia chama cha mapinduzi alizitambua changamoto hizo juu?Je kwakutumia tu utashi wa kawaida wa kujua kusoma na kuandika hii sera inatekelezeka ndani ya miaka mitano?????

7.Tukiangalia kwa undani safari ya sera ya technolojia na viwanda na Africa kiujumla zinafana fanana ila moja ya sababu ya kufeli hii sera at first place Tanzania ni kushindwa ku repair machine. kwakua in Africa hamna technological transfer na patent rights za technolojia ni kubwa mno kiasi kwamba wataalamu wengi wana link acquisation ya technolojia na heavy debt burden (mikopo mikubwa) na bado wana control technolojia zao hata baada ya kukukodishia inatia umasikini bara la Africa vipi baba Magufuli umejiandaa nalo vipi hili?
Mbaya zaidi hizi imported technology hatuwezi ku adapt katika mazingira yetu (indegeneous technology )

8.Swali lingine je watunga sera ya viwanda wanajua kuwa maendeleo ya Africa yanaendeshwa na sera za nchi za magharibi?unajua kwanini huu ni muongo wa sita tangua Africa ianze kupata uhuru imeshindwa kuwa na self reliant development (self sustained) licha ya kuwa ni kinara wa resources?

Maswali ni mengi mno,sera ya viwanda kwa sasa hivi ni ya chama hii maana yake nini ikitokea chama kingine kikachukua madaraka upo uwezekano wakaifutilia mbali muda huo lazima tutambue hamna Taifa limekua kiuchumi bila maendeleo ya sayansi ,Techolojia na viwanda katika share yake kwenye GDP,BOP, kutengeneza ajira,kuongeza kipato na kuboresha maisha ya raia wake katika level mbalimbali za kijamii .

Hii hoja inaibua mjadala pia, Je sera ya nchi ikoje katika kukuza maendeleo ya sayansi na Technolijia?Je ilifeli ndo maana ikaanzishwa political party initiation ya viwanda?Huku sio kuanzisha administrative bureaucracy?Yaani tumeanzisha kitu ambacho kilishakuwepo lakini hakukuwa na utekelezaji maana yake tulishafeli?

Wasalam
Hieanda walimanisha vowanda vya maneno matupu kama hapa kazi Tu!
 
Hivyo viwanda vinatoka wapi na kwa Sera IPI...???
Tatizo uwezo wako ni mdogo. Na mwisho wa siku utakuwa pungu wani. Nenda kwenye tovuti za Serikali mipango ukajifunze na kusoma dira ya maendeleo na Sera mbalimbali. La sivyo utabaki kuwa na kichwa kikubwa bila akili.
 
Kama mfumo wa haki ungekuwepo bongo, hii serikali ilitakiwa kufikishwa mahakamani na watu waka-resign maana kwenye kampeni watu waliambiwa kwamba serikali itajenga viwanda halafu baada ya kuanza kazi waziri anasema serikali haitajenga kiwanda na kazi ya serikali ni kupiga saundi ili wawekezaji waje! Kama ndivyo basi hakukuwa na haja ya kuwadanganya wapiga kura kwa sababu awamu zote zilipiga saundi ili kuvutia wawekezaji.
 
Kama mfumo wa haki ungekuwepo bongo, hii serikali ilitakiwa kufikishwa mahakamani na watu waka-resign maana kwenye kampeni watu waliambiwa kwamba serikali itajenga viwanda halafu baada ya kuanza kazi waziri anasema serikali haitajenga kiwanda na kazi ya serikali ni kupiga saundi ili wawekezaji waje! Kama ndivyo basi hakukuwa na haja ya kuwadanganya wapiga kura kwa sababu awamu zote zilipiga saundi ili kuvutia wawekezaji.
Mtu wa kwanza kupelekwa Mahakamani ni Mtei na Mbowe.
 
upo sahihi ila ant kuelewa watakupinga kazi kutukana wenzao kuwaita nyumbu tu
 
Back
Top Bottom