Keynez
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 3,621
- 6,512
Tanzania ya miaka ya 60, 70, 90 na kuendelea ina kumbukumbu nyingi ambazo nyingi tunaziongelea katika mazungumzo yetu ya kila siku kila tunapozungumza mambo ya siasa, uchumi, kijamii na historia yetu kwa ujumla.
Ila kwa muda nimegundua kuna uhaba wa mazungumzo na kumbukumbu za kutosha kuhusu kipindi cha miaka ya 80. Najua kilikuwa ni kipindi kilichokuwa na changamoto na pilikapilika nyingi, mfano hali ya kisiasa huko Zanzibar, mwisho wa vita vya Kagera na changamoto zake, kung'atuka kwa Mwalimu nk. Ila naona bado sipati picha kamili ya hali ya kijamii ilivyokuwa kiujumla hapa Tanzania.
Nikiongezea, naweza kusema muongo ule wa 1980 inawezekana ndiyo umetoa athari kubwa zaidi (nzuri na mbaya) za kisiasa, kiuchumi na kijamii tulizonazo leo hii.
Wahenga embu mtujuze basi.