Tanzania ya miaka ya 1980

Tanzania ya miaka ya 1980

la Kipindi kile nchi ilikua mbele kimaendeleo kuliko sasa!Ajira zilikuwepo angalau,viwanda vingi nchi nzima railway ilikua na ufanisi mkubwa,mashirika ya umma yalimea mf NMC,RTC, nk,Hatukulipia huduma za matibabu hosp ilikua bure!elimu ilikua bora zaidi shule za government...faftari,kalamu bure!
watu tulikua wangapi??? nani alikua anaogoza nchi?? nani alikua msemaji na mwenye sauti ya mwisho???
 
Miaka ya 80 filamu za Kihindi zilikuwa maarufu sana.

Baadhi ya wacheza filamu nyota wa kipindi hicho, kama Mithun Chakraborty, kwa mfano, walikuwa wanakuja hadi Tanzania.

Pia ni miaka ambayo mitindo ya nywele kama 'shegi' na 'panki' ilivuma sana.

Na kama sijakosea, madawa ya kubadilisha nywele [kali kiti - curl kit] ndo yaliingia nchini.

Shashi kapoor ..Amjad Khan(RIP), Rheka, kisura Zeenata Aman ..Cameo cinema. UDA walileta IKARUS toka Hungary zilikuwa ndefu LHD ..na baadae zikaja fupi pia. Enzi hizo ku drop kwenye basi ndio ujanja ...una suruali ya mchelemchele na chachacha ...Handkerchief unanininginiza nje ya mfuko wa suruali yako yenye celebrations. Enzi za ile coaster "Scaba Scuba"....safari buti aka mbwa na raba za ikarus za Bora...duu kipindi sana
 
Baada ya vita ya Kagera.Kulikuwa na msemo wa miazi 18
Ya uvumilivu.Kila Jumatatu na Jumatano tunakwenda duka la ushirika(baada ya kuchukua bidhaa RTC) tunapiga foleni ndefu ya Unga wa Yanga(manjano) mafuta ya kupikia na sukari.Shule nyingi zilikuwa za kulipia serikali ikazi fanya bure.Mabasi ya railway na ya kamata ndio usafiri.Pamoja na yote hayo Tanzania ilikuwa nzuri.Tulikuwa hatujali TV maana hakuna.Simu inabidi uende kwa jirani(waringaji wakubwa na simu zao) au uende posta unaingizwa kwenye (call box) Duh tumetoka mbali.Dar,Mwanza,Tanga na Arusha zilikuwa safiiiiiiii
Na ukifika katika Hiyo miji lazima uripoti kwa mjumbe wa nyumba kumi.

Aisee umenikumbusha enzi zile unaenda na kitabu chako cha ration dukani kila baada ya wiki mbili kununua sukari .
Operesheni Nguvu kazi...nakumbuka polisi walikuwa wanakuja wamevaa kiraia na kama wanapiga tizi (jogging) ..halafu inapigwa filimbi wanatawanyika na wanaanza kamata watu...
 
Ukisema miaka ya 80 ndio Turn point ya Tanzania ilipoanza
Kuteka ndege ya ATC na akina Member Lee kutoka Mwanza hadi Uingereza wakidai Nyerere ajiuzuru
Vita ya hujumu uchumi kuna wahindi walimwaga pesa barabarani.
Kufukuzwa kazi makamu wa kwanza wa raisi Jumbe na kuvuliwa hadhi zote hadi akawekwa under house arrest.
Kifo cha Waziri Mkuu Sokoine kilishtua umma,ili kupoza hasira za wananchi Nyerere akamteua Salim Mohamed Salim kuwa Waziri Mkuu.
Uncle Tom alikula njama na maofisa wa jeshi kumpindua raisi Nyerere,lakini jaribio lilizimwa na watu kadhaa kukamatwa,Commando Tamimu aliepanga kumua Nyerere alipigwa risasi na kachero Mabele Marando.
Nyerere alingatuka chini ya shindikizo za nje na ndani mwaka 1985.Mwinyi akachguuliwa raisi wa Tanzania.
 
And i $=5Tz ndiyo sababu kuna kitu naitwa dala dala.

Miaka ya 80 kabla ya vita ya Kagera pamoja na matatizo ya JON uchumi ilikuwa very strong.Kama Taifa ilimiliki viwanda vingi.Wakati Me into anatoa madarakani $=250 of not 100.

Baada ya kuingia Mkapa pamoja n.a. kuu a viwanda na Bank ya BBC $=1200,hivyo majambazi ya Raslimali zetu yalianzia hasa kipindi cha Mkapa ambaye mpaka leo kodi zetu ndizo zinamlisha,zinamnyeshwa na Kumvisha.

Wakati wa tawala ga Mkapa ndipo Watawala lea ulafi walijilimbikizia Mali kupindukia.Ni aibu leo Mkapa kiwatukana wapinzani wakati yeye ndiyo chanzo cha kuuza Raslimali zetu.
Mkuu huyo Nkapa na familia yake ndio walio filisi nchi yetu.Banks nyingi lakini inayo niuma zaidi ni ya NBC Kabla hajawapa makaburu.Viwanda alivyo vigawa kwa familia yake na wapambe wake.Watu wengi walisota wakati wa utawala wake na Bila ya kusahau mauwaji ya Wazanzibar.Yule nkapa Mungu anamuona.shenzi taipu
Ana haki ya kutuita sisi Malofa
 
Kweli kabisa,pamoja na kuelezwa NBC inajiendesha kwa faida bado akaiuza kwa bei pouwa kabisa.Kweli Mkuu tunahaki ya kuitwa MALOFA
 
Baada ya vita ya Kagera.Kulikuwa na msemo wa miazi 18
Ya uvumilivu.Kila Jumatatu na Jumatano tunakwenda duka la ushirika(baada ya kuchukua bidhaa RTC) tunapiga foleni ndefu ya Unga wa Yanga(manjano) mafuta ya kupikia na sukari.Shule nyingi zilikuwa za kulipia serikali ikazi fanya bure.Mabasi ya railway na ya kamata ndio usafiri.Pamoja na yote hayo Tanzania ilikuwa nzuri.Tulikuwa hatujali TV maana hakuna.Simu inabidi uende kwa jirani(waringaji wakubwa na simu zao) au uende posta unaingizwa kwenye (call box) Duh tumetoka mbali.Dar,Mwanza,Tanga na Arusha zilikuwa safiiiiiiii
Na ukifika katika Hiyo miji lazima uripoti kwa mjumbe wa nyumba kumi.
Duuu wahenga nyie,mbona leo hakuna kureport ukienda sehemu au watu wamekuwa wengi mno?
 
Ukisema miaka ya 80 ndio Turn point ya Tanzania ilipoanza
Kuteka ndege ya ATC na akina Member Lee kutoka Mwanza hadi Uingereza wakidai Nyerere ajiuzuru
Vita ya hujumu uchumi kuna wahindi walimwaga pesa barabarani.
Kufukuzwa kazi makamu wa kwanza wa raisi Jumbe na kuvuliwa hadhi zote hadi akawekwa under house arrest.
Kifo cha Waziri Mkuu Sokoine kilishtua umma,ili kupoza hasira za wananchi Nyerere akamteua Salim Mohamed Salim kuwa Waziri Mkuu.
Uncle Tom alikula njama na maofisa wa jeshi kumpindua raisi Nyerere,lakini jaribio lilizimwa na watu kadhaa kukamatwa,Commando Tamimu aliepanga kumua Nyerere alipigwa risasi na kachero Mabele Marando.
Nyerere alingatuka chini ya shindikizo za nje na ndani mwaka 1985.Mwinyi akachguuliwa raisi wa Tanzania.
Mwinyi hakupigiwa kura?na ilikua mwaka gani
 
Miaka ya 80 filamu za Kihindi zilikuwa maarufu sana.

Baadhi ya wacheza filamu nyota wa kipindi hicho, kama Mithun Chakraborty, kwa mfano, walikuwa wanakuja hadi Tanzania.

Pia ni miaka ambayo mitindo ya nywele kama 'shegi' na 'panki' ilivuma sana.

Na kama sijakosea, madawa ya kubadilisha nywele [kali kiti - curl kit] ndo yaliingia nchini.
Casius Clay (Mohamed Ally) alikuja kipindi hichi pia
 
Kadi za kijani za ration ya unga wa yanga na sukari zilikua ndo mpango mzima. Mafuta aina ya petrol na diesel ilikuwa kuuziwa mwisho lita 6 kwa wiki. Ukimaliza kabla imekula kwako. Magari kuendesha ilikua mwisho saa saba mchana siku ya jumapili isipokua kwa kibali maalum. Kununua gari lazima upate kibali kutoka State Motors Corporation. Ni kipindi ambacho kituo cha tv kilikua zanzibar tu. Na kituo cha redio kilikua kimoja tu. RTD. utake usitake lazima usikilize kipindi cha malenga wetu. ndio kipindi ambacho wazungu walianza kuongezeka nchini kwa gia ya expatriates na magari yao yalikua na vibao vyekundu na kuanzia na herufi TX. unaweza fananisha na DFP kwa sasa.
 
Kipindi hichi ndio nchi yetu ilikua kwenye transition kutoka siasa ya ujamaa na kuanza siasa za kibepari . Ndio kipindi ambacho utaifa ulianza kupotea na kuja kwa ubinafsi na tamaa iliyopita kiasi. Kilikua kipindi kibaya sana. Madawa ya kulevya yakaanza kuingia kwa kasi miaka ya 1985 na kuendelea. Shule za serikali zikaanza kuwa mbaya taratibu na kufanya watu wenye hela kuanza kupeleka watoto Kenya na Uganda kusoma. Maadili yakaanza kushuka kwa kasi mno.
 
Viwanja vya kujirusha Dar vilikuwa YMCA, Ushirika, Lang'ata, vision, Mbowe na Msasani club (Pamoja na Disco toto).
 
yes uchumi ulikuwa ni mzuri,services deliveries kwa wananchi zilikuwa above average,zahanati,shule,mahakama,n.k.ufanisi ulikuwa mzuri mno,unamaliza kidato cha nne unapewa form maalum ya kujaza wapi future yako itakuwa,combinations za kidato cha tano unazozitaka na kuwa na uwezo nao,mwishoni mwa 80s ninaingia pale Mkwawa CNE ni evergreen,mabweni safi kuanzia Magembe hadi Shaaban Robert W,CHAKULA SAFI NA MWISHO WA MWEZI UNALIPWA KICHELE ,yes maisha yalikuwa safi kwa familia nyingi,tatizo kubwa lilikuwepo ni mawasiliano,barabara zilikuwa nyingi hazipitiki hasa kipindi cha masika,hasa mikoa ya kusini but in general nchi ilikuwa na adabu ,uwezo wa kutembea alfajiri ya saa 8 kutoka magomeni kondoa(DDC sikinde) hadi kinondoni shamba ulikuwepo uhakika wa asilimia 99 utafika salama.yeah personal iam mic yale maisha.poleni for this generations sijui ijao.
 
MiaKa hiyo vyuma vilikaza kuliko Hali ilivyokuwa sasa Mpumbavu wa wakati huo Kichaa chake kikampanda akaanzisha 'Uhujumu uchumi' kutesa na kufilisi Watu Kama afanyavyo Kichaa wa sasa japo juhudi hizo hazukumsaidia chochote 'Mnyonge' aliekuwa anatetea asihujumiwe
Wakati mwingine Lugha yako huwa sio ya STAHA
 
Back
Top Bottom