Kimkakati Mbowe bado anahitajika kuongoza Siasa za Upinzani, anaaminika na Dunia kuliko viongozi wote wa Upinzani!!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,035
142,144
Tanzania siyo kisiwa hivyo tunahitaji viongozi waliobeba maono ya Dunia ambao wakigonga hodi ubalozi wowote wanafunguliwa mlango

Freeman Mbowe amefikia Wakati wa kustaafu lakini Siasa za Tanzania bado zinauhitaji Sana Uongozi wake

Kuorganize Maandamano Hata ya Watu 10 tu kwa Siasa za Tanzania tangia enzi za Akina Mchungaji Mtikila ni jambo gumu Sana lakini huyu Mwamba kafanikisha tena kwa Amani kabisa hajafa Hata Sisimizi

Mlale Unono 😄
 
Nadhani existence ya Dr.Samia Suluhu Hassana inahitajika zaidi mamlakani na huyu mumama atakumbukwa mno, zaid ya kiongozi mwingine yeyote humu nchini....
 
Usemi huo unaongelea. Chochote kwamba tunaweza mkabidhi kijiti bwana mwarabu, rostam aziz.
 
Tanzania siyo kisiwa hivyo tunahitaji viongozi waliobeba maono ya Dunia ambao wakigonga hodi ubalozi wowote wanafunguliwa mlang...
Kuna vyama CHAWA 13 viliungana na RC Chalamila kujikomba kwa CCM, na kudai maandamano hayana faida yataleta vurugu na kuilaani Chadema walioandaa maandamano hayo.

Cha kujiuliza ni kwamba, huku kujikomba kwa vyama hivi vya upinzani faida yake ni Nini? Na baada ya maandamano kwisha kwa Usalama, hivi vyama "VINAJISIKIAJE?"

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
nadhani existence ya Dr.Samia Suluhu Hassana inahitajika zaidi mamlakani na huyu mumama atakumbukwa mno, zaid ya kiongozi mwingine yeyote humu nchini....
Rais Samia tayari ameingia katika Kitabu Cha KUMBUKUMBU, Marais wa kiume wote waliogopa maandamano, yeye ameweza.

Rais aliyepita alisema uchaguzi ukiisha, hakuna mikutano mpaka miaka 5 ipite, mama mlezi ameruhusu. Aliyepita alisema mwanafunzi anayezaa akiwa shule asirudi shuleni, Mama mlezi ameruhusu.

Aliyepita alisema mkurugenzi ambaye eneo lake atachaguliwa mpinzani Hana kazi, hili Sasa mama mlezi aruhusu chaguzi ziheshimiwe, aliyechaguliwa na Wananchi atangazwe. Rais Samia akimudu hili, atakumbukwa kwa kipindi kirefu sana kuwa ni Rais wa kike aliyebadili Hali mbaya na ya dhulma iliyojengwa kwa miaka mingi na CCM.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Tanzania siyo kisiwa hivyo tunahitaji viongozi waliobeba maono ya Dunia ambao wakigonga hodi ubalozi wowote wanafunguliwa mlango...
Ili ndo tatzo kubwa sana la sisi watu weusi tunadhani tunaitaji msaada kutoka kwenye mataifa mengine ndo ile ya kuendelea kutegemea mataifa ya watu …

wakati nao wanamasilai yao… ni lini Tanzania tutakuwa baba wa kuchukua majukumu ya kila kitu kwenye familia? Hatuitaji mtu yoyote Yule zaidi ya sisi wenyewe Kujenga maendeleo yetu.
 
Naanga mkono hoja Mbowe ni Mfalme wetu akae maisha atakayejaribu kumpiga tumshambulie tumfukuze Chadema kama vile Zito Kabwe na Kafulila.
 
Back
Top Bottom