Simba Mwepesi
Member
- Nov 17, 2022
- 22
- 13
Kuna mwaka Gari tulilopanda liliwahi kupoteza mwelekeo na kutaka kugonga lingine Ila dereva alirudisha umakini na kuliweka sawa na hivyo kutuepusha na ajali mbaya ambayo na amini kesho yake tungekuwa maarufu( kwa idadi kubwa ya vifo na majeruhi), ilibidi dereva asimamishe ili tuchimbe dawa na kujiweka sawa kiakili maana sio kwa kukoswa kule kwenye ili ajali. Hivi ndivyo naiona Tanzania yangu..,Nchi lipofika sio pazuri.Tumepoteza muelekeo wetu wa Utu,Upendo,Haki,uwajibikaji na Amani. Leo hii kiongozi kafa au akifiwa na mtu wake wa karibu, wananchi wanafurahi badala ya kuhuzunika nae( Hii Hali itaendelea mpaka lini??), Yaliotokea oct 29 na siku zilizofuata hayatasaulika Leo wala kesho( Watu walipoteza maisha,wengine walijeruhiwa na wengine wamepotea mpaka Leo, Ni nani atakayesahau Yale maandamano yaliotangazwa siku zile za 9 desemba Na siku zilizofuata? Nani atasahau zile Barabara kufungwa wakawa Kama wapo kwenye kisiwa?)...Serikali, Watu bado Wana machungu mazito Sana kuhusu yaliyotokea siku Ile,, tunawaona wanacheka machoni Ila moyoni wanaumia, Wasaidieni kisaikolojia watoke huko, Msisahau wale watoto waliopoteza wazazi wao siku Ile,Hawa tukiwaacha wakiwa wakubwa tutazalisha magaidi na watu wasioipenda serikali yao( Angalieni huko uarabuni jinsi kisasi kinavyovitesa vizazi vyao, tusifike huko). Angalieni mfano wa Sauzi Africa walivyofanya kwenye hatua zao za maridhiano ya kitaifa.,Penye nia pana njia,Muda wa kumchukua hatua ni SASA(Hatujachelewa, Tuiokoe Tanzania Yetu na vizazi vyetu)...Mwenye macho haambiwi tazama,Wananchi wenzangu, shime niwaombe asitokee mtu atutenganishe kikabila,kisiasa,kidini au hata kwa rangi zetu, Tulinde tunu zetu walizotuachia waasisi wetu. Nchi hii ni yetu sote, Rasilimali hizi ni zetu sote Amani na Haki ni mapacha walioungana na huwezi kuwatenganisha kamwe. Hivyo Haki na Amani Ndio Asili ya Mema yote., mengine hutokea hapo. Niombe waliofungwa waachiliwe huru,Waliotoroka Nchi warudi(na wasikamatwe kwa hila zozote),turudi mezani kwenye mijadala ya kujenga Nchi na sio kubomoa,Tusiwaruhusu mabeberu watuamulie nini Cha kufanya kwa kuwa hawana huruma na rasimali zetu.Hii Amani ikiondoka tutakuwa zaidi ya Kongo maana Nchi hii imebarikiwa kwa kila kitu. wajibu wa kuilinda Nchi sio ya wanajeshi pekee yao(Respect Comrades) au viongozi,Ni yetu sote na tuilinde Amani yetu kwa nguvu zote(sio Kama zile za oct .29)..Tanzania Nakupenda Sana,2030 itakuja na itapita, Ila Tanzania itabaki. CCM na wapinzani kaeni mrekebishe tofauti zenu tuokoe taifa letu na turudi kuwa kimbilio la wanaonewa na kudhulumiwa utu na Haki zao. VIVA TANZANIA