Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 39,815
- 71,262
Ndege imekamatwa kutokana na deni letu la mkulima. Deni lipo na tunakubali (kwa shingo upande) kuwa lipo. Wanaotudai hatuwalipi, hatukai meza moja kuzungumza, bali sisi tukishinda zuio moja la mahakama tunatumia muda mwingi kujipongeza kuwa tuna wanasheria magwiji kuweza kumgaragaza mzungu.
Tunatumia muda na fedha za umma nyingi kugongeana glass za mivinyo ya Italy na ufaransa kusherehekea jambo la muda huku tukitumia UONGO kumdanganya Rais na Watanzania kuwa tumeshinda lakini kumbe deni liko palepale na tunajua hilo ndio maana tukazuia ATCL isiende tena South Africa kwa UONGO kuwa eti kuna xenophobia utadhani ndege ni zetu pekee ziendazo huko na Rais akakubali.
Njia ya muongo fupi, mzungu kaangalia wapi sheria itam favor na kuona ni Kanada akaenda.
Sasa Kabudi kama kawaida bila hata woga anamuita TAPELI ili kuficha udhaifu wake yeye na watendaji wa serikali katika kushughulikia aibu hii. Hivi kama taifa tunaweza kuchezewa na matapeli kiasi hicho? Jee mkulima mzungu ni mdai wetu au tapeli kwetu?
Nilipata kuona email moja hapa JF ikitoka kwa mkulima kwenda kwa Profesa Kabudi akiwa waziri wa sheria, na kama email ile ilikuwa ya kweli basi suala hili ni completely mishandling yake binafsi na ni makosa makubwa kuendelea kuwa na waziri amayetumia UONGO KUFICHA UDHAIFU.
Ni dhahiri baada ya kesi kule SA badala ya kujipongeza na kujisifia sifia kijinga, tulikuwa na nafasi ya kuzungumza pembeni na mkulima (tapeli) na kukubaliana namna ya kulipa kilicho baki kidogo dogo na kimyakimya bila ya kuaibishana.
Sasa Kabudi anataka kutugombanisha na Kanada, kwani biashara ya kununua ndege hizo ni siri kiasi watu wasijue? Tunanunua bangi kule?
Kabudi umefeli big time!