The Zanzibar Echo
JF-Expert Member
- Apr 21, 2025
- 490
- 836
Baadhi ya viongozi nchini Tanzania wameanza kuchukua fomu za kugombea ubunge kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.
Miongoni mwa waliotangaza nia hiyo ni Rais wa Klabu ya Yanga, Injinia Hersi Said, ambaye leo Jumamosi, Juni 28, 2025, amechukua fomu ya kugombea Ubunge wa Jimbo la Kigamboni kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Akizungumza baada ya kuchukua fomu hiyo katika Ofisi ya CCM Kigamboni, Hersi amesema:"Nikiwa kama mwanachama wa CCM, nimekuja kutekeleza haki yangu ya kikatiba ya kuchaguliwa. Nimechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuwania nafasi ya Ubunge kuwakilisha Jimbo la Kigamboni."
Katika hatua nyingine, aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Ester Bulaya, ametangaza kurejea CCM na kutangaza nia ya kugombea Ubunge wa Jimbo la Bunda Mjini, mkoani Mara.
Bulaya aliwahi kuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia CCM kati ya mwaka 2010 hadi 2015 kabla ya kujiunga na Chadema mwaka huo huo, ambapo alishinda ubunge wa Bunda Mjini dhidi ya mwanasiasa mkongwe, Stephen Wasira. Hata hivyo, alijikuta katika mgogoro na Chadema mwaka 2020 baada ya yeye na wenzake 18, akiwemo Halima Mdee, kuapishwa kuwa wabunge wa viti maalum bila ridhaa ya chama hicho kikuu cha upinzani.
Wakati baadhi ya wenzake wametangaza kujiunga na vyama vingine, wakiwemo waliorejea CCM, Bulaya amesema amerejea CCM kimyakimya."Mimi ni mtu mzima, nimesharudi nyumbani na nimeshakabidhiwa kadi yangu kimyakimya bila matangazo. Nitachukua fomu kuanzia leo ili kuwania ubunge wa Bunda Mjini," amesema Bulaya katika mahojiano na gazeti la Mwananchi.
Wengine waliokwisha kuchukua fomu ni pamoja na Jerry Slaa, anayewania kwa awamu ya pili Ubunge wa Jimbo la Ukonga kupitia CCM, na aliyekuwa Mbunge wa Shinyanga Mjini na Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika (PAP), Stephen Masele, ambaye ametia nia ya kugombea tena jimbo hilo kupitia CCM.
Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu unatarajiwa kuwa na ushindani mkali vyama vikuu vya siasa vikijiandaa kwa kampeni zitakazoanza baada ya mchakato wa kuchukua na kurudisha fomu kukamilika.