Aizi Azma
JF-Expert Member
- Nov 30, 2016
- 553
- 1,151
Well,... Kenya wanatupiga gap (Kwa maoni yangu), wana-establish Konza City na wana initiatives mbalimbali za kuhakikisha wanaendana na kasi ya ukuaji wa teknolojia. Rwanda ndo usiseme, wako vizuri... mpaka tunaambiwa wamepenyeza mpaka 'chumbani' kwetu. Huwa najiuliza ina maana sisi Tanzania hatuoni jinsi teknolojia inavyotuacha? Kwanini wenye mamlaka hawaoni umuhimu wa kufanya jitihada za makusudi kama nchi za kuhakikisha tunaendana na kasi ya ukuaji wa Teknolojia? Dunia ina-shift kiteknolojia kwa kasi ya ajabu... Sisi tunaji-position wapi?
Hapa naongelea kuanzia mitaala mashuleni mpaka mipango tunayojiwekea kama nchi. Tusijekuwa tunatumia mtazamo na teknolojia ya mwaka 2000 kupanga mipango ya mwaka 2025... tutaachwa kwenye vumbi wakati wenzetu wakipiga hatua kubwa hasa hasa kiteknolojia.
Mungu ibariki Tanzania.