Tanzania tulikosea wapi na Kenya walipatia wapi?


Ndugu umenena[emoji1474]
 
Unafikira za kujidanganya au umedanganywa. Kuna maelezo mengi ambayo hayana
Ukweli umeandika hapa. Nitakutafuta tuzungumzie yawezekana ukasaida wengi ambao wana ufahamu kama wako.
 
Sisi ni sawa na yule aliyepewa talanata halafu akazichimbia ili ku mrudishia mwenyewe badala ya kuzalisha. Huu ni mfano wa zaidi ya miaka 2000.. Je sis tunazitumia hizo talanta!!?
 

embu niambie daktari wa tz akienda nchi gani anakosa sifa!!!vipi eng??

wote sisi tumetohoa elimu za kikoloni ambazo kimsingi haimjengi msomi katika kujikomboa,na ukitaka ujue wana ujinga zaidi wanatudharau kwa kutojua kiingereza,kwao majengo na madaraja yanaanguka.
 
Fafanua hizo namba
System mpya ipo Hivi Mkuu, lengo kuu ni kuondoa dhana kuwa tunasoma tupite mitihani bali sio watoto wetu kupata elimu.
Fafanua hizo namba


All students take 2 years of Pre-primary, then 6 years of Primary, and then 3 years of Junior School. If you pass the Grade 9 exams at 15 at the end of Junior School, you can then go on to take 3 years of Senior School. University under CBC will be just 3 years instead of 4..
 
Tanzania ilipata Uhuru wake kwa porojo, ila Wakenya walipigana vita vya MAUMAU ambayo viliua wakenya wengi sana hasa wa kabla la wakikuyu. Kupata kwetu Uhuru kwa njia ya porojo ndipo kunakoliponza Taifa letu - dhana ya woga na kutojiamini ndiko kunaliangamiza taifa letu - killing softly... Porojo porojo tu ni kila pahala !!
 
Baada ya Uhuru Tanzania tulifuata ujamaa na kuelimisha wananchi wetu. Nyerere alitaka kila mtanzania awe kasoma ili tuweze kujitawala wenyewe baadaye na ndiyo maana tukawa na elimu ya watu wazima na Tanzania ndiyo iliyokuwa inaongoza Afrika kwa literacy ikifuatiwa na Misri. Nyerere alita wananchi wake wawe wanamiliki ardhi yao na wajitegemee. Kenya wao walibaki na sera za kibeberu, sehemu kubwa ya ardhi nchini kwao inamilikiwa na wazungu ama wahindi (mpaka leo) wakati wananchi hawana kitu. Someni historia ya nchi zetu mjuwe, msipende kuandika ujinga tu.
 
Shida ni Kiingereza, sidhani kama kuna kingine
Yaani sijapata kusoma majibu ya kijinga kama haya....Kiingereza ni lugha tu wala si kigezo cha maendeleo hii ni kasumba ya kijinga sana. Mkuu hujasoma hata kidogo maishani mwako?
 
Moi amekaa madarakani 22yrs (1978-2020)
Nyerere amekaa24yrs (1961-1985), na ccm 59yrs (1961-2020
Moi amekaa madarakani 22yrs (1978-2020)
Nyerere amekaa24yrs (1961-1985), na ccm 59yrs (1961-2020)
Mambo mapungufu mabayakiasi ya Kenya tunaweza kuyajua vizuri. Maovu mabaya sana ya Tanzania sio rahisi sana kujulikana hasa na wasioelimika/wavivu wa kutafuta habari. Ni sababu kenya kuna uhuru wa habari, sisi vyombo vya habar vimewekwa mfuko.Mfano mdogo: mwanahabari anatoa habari kupitia chombo chake kuwa eneo fulani barabara imeharibika, anapata matatizo kibao eti unatakiwa utoe taarifa hizo srikalini, wewe sio mzalendo ni kibaraka wa mabeberu nk. Tz ili meanahabari uwe salama tangaza tu habari za kumsifu Magufuli na serikali. Tanzania usiku na mchana ni kujipa tu sifa za uongo. Ukisikiliza tbc utadhani tanzania imegeuka kuwa ulaya nyingine. Tunajenga hiki, tunajenga kile. Tunajenga hapa tunajenga pale. Tumenunua ndege tumenunua kile. Nchi nyingine wanafanya mengi zaidi huwezi sikikia makelele ya kujisifu.
 
Unataka kutuaminisha waTz wameelimika kuliko wakenya? Unataka tuamini wakenya wamekosa ardhi ya kulima? Sio kweli. Kenya kuna matajiri wakubwa wanamiliki ardhi kihalali, wamewekeza miradi ya uzalishaji, wanaajiri na wanalipa kodi . Sisi ardhi kubwa imekaa tuu bure tunafaidika vipi? Naona kama wewe ndio mjinga hujajitambua.
 
Ok
 
dhana ya kipumbavu ni ulochoandika, the thing is : kenya is not a country in itself. It's a proxy of USA Africa, would you be proxy of a wealthy person just to rub shoulders with the VIP? that's the question Tanzania asked themselves and decided our dignity comes first. We are our own country, we fight our own wars, we choose who to support free willy. Kenya can only support who the USA is supporting.
 
Kosa tumejengwa kwenye msingi wa kuongozwa na viongozi miyungu watu, hawahojiwi hawaambiliki,wanakuwa watakatifu kipindi cha uchaguzi wakijipitisha kwa njia za haramu wanakuwa juu ya waajiri wao ambao ni wananchi kwa kuwacharaza mijeledi.
 
Na pia ulete stori ya watu wanaoishi vijijini Tanzania. Chukua Kijiji kimoja tu, tena nakuruhusu uchague kile kinachoonekana ni kielelezo cha ustawi, halafu ulinganishe na Kibra, tuone!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…