SoC04 Tanzania Tuitakayo: NHC katika Kujenga Mustakabali Endelevu

Tanzania Tuitakayo competition threads

Damaso

JF-Expert Member
Jul 18, 2018
1,662
2,219
Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) la Tanzania, lililoanzishwa kwa lengo mapana la kuboresha upatikanaji wa makazi, pamoja na malengo ya kuhakikisha kila Mtanzania anapata nyumba tena ya bei nafuu. Lakini ni ukweli mchungu kubwa NHC ni shirika ambalo limeshindwa kufikia uwezo wake. Ingawa inajivunia sifa ya kujenga nyumba bora, NHC wanapoteza sifa kabsa katika masuala ya kuweka gharama nafuu za maisha, vikwazo vya urasimu, na ukosefu wa kuzingatia makazi ya watu wa kipato cha chini. Makala hii itaonesha mtazamo wa mambo mengi, unaojumuisha urekebishaji wa fedha, mageuzi ya uendeshaji, na mtazamo mpya wa kijamii, ni jambo muhimu sana ili kufufua NHC na kutimiza dhamira yake ya awali.​

1714654428210.png

Picha kwa hisani ya NHC
Kwanza, nyumba za nyumba za NHC mara nyingi bei zake hazifikiwi na Mtanzania wa kawaida. Mfano, NHC inajivunia kuwaletea watanzania nyumba za bei nafuu zilizoko ndani ya eneo tulivu la Kibada. Kigamboni Housing Estate ambayo ipo Kigamboni katika eneo linalofikika kirahisi, ni kilomita zisizopungua 17 kutoka pale Feri. Huu ni mradi wa nyumba zipatazo 182 zilizopangwa kwa kuzingatia vigezo vya miji ya kisasa yenye huduma za msingi zikiwemo sehemu za maalumu za watoto na shughuli mbalimbali za imani, lakini je gharama zake zipoje? Ni gharama za aina gani? Nyumba ya vyumba viwili yenye mita za mraba 56 bei yake ni Tsh 41,987,160.00 bila kuwepo kwa VAT. Serious kabsa! Nyumba ya vyumba vitatu na mita za mraba 70 bei yake ni Tzsh 46,599,300.00 bila VAT. Na ikumbukwe hapo hizo ni nyumba ambazo zimekamilika zikiwa na umeme,maji na nyingi zikiwa na huduma muhimu. Hapo wengi tunaelewa kuwa nyumba hizi sio za watanzania wa hali ya kati na chini.​
1714654531144.png


Pili, shirika limejiingiza katika urasimu. Mchakato wa maombi ya kununua nyumba za NHC ni mgumu na unatumia muda mwingi, umejaa makaratasi magumu na ucheleweshaji wa muda mrefu. Hii inakatisha tamaa wanunuzi na inadhoofisha ufanisi wa mfumo. Mfano, NHC ina michakato mitano ambayo inatakiwa mtu kupitia yote ili aweze kununua nyumba, kuanzia, mosi unatakiwa kupakuwa House Purchase Application Form ambayo utaijaza na kuirudisha ikiambatana na malipo ya 12,500 pamoja na 10% ya gharama ya ununuzi wa nyuma husika, kitaalamu unalipa 4659930 ambayo hairudi, yaani unalipa milioni 4 kuonesha kuwa una utayari wa kununua nyumba (Ajabu hii). Mlolongo wa mchakato huu ni mrefu kupita maelezo na unachosha sana.​
1714654687565.png

Picha kwa hisani ya NHC
NHC inakosa mwelekeo wa wazi wa suluhisho la makazi ya watu wa kipato cha chini. Ingawa baadhi ya mipango ipo, mara nyingi huwa na mipaka katika kiwango na upeo. Mbinu ya sasa inashindwa kushughulikia hitaji muhimu la masuluhisho ya nyumba za bei nafuu na zinazostahiki kwa watu wa kipato cha chini na wakazi wa makazi duni. Miradi ipo mingi ila bei haijawahi kuwa Rafiki kwa wananchi au wenye nchi hata siku moja. Ni wazi kuwa mnapewa sifa na Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya PIC anapofurahia utekelezaji wa miradi ya NHC Jijini Dar es salaam lakini gharama zenu ni kubwa sana.​
1714654742369.png

Picha kwa hisani ya Lady Detective.
NHC inapaswa kutafuta mbinu mbadala za ufadhili badala ya kutegemea ruzuku ya serikali pekee. Ushirikiano wa sekta ya umma na binafsi unaweza kuongeza mtaji wa sekta binafsi kwa miradi ya nyumba za bei nafuu. Zaidi ya hayo, kuchunguza chaguo za ufadhili mdogo kunaweza kufanya umiliki wa nyumba kufikiwa na watu wa kipato cha chini, NHC lazima irahisishe kwa kiasi kikubwa mchakato wa maombi ya ununuzi wa nyumba. Kutumia majukwaa ya mtandaoni na kurahisisha makaratasi kunaweza kuongeza ufanisi na uwazi. Wanaweza kutumia teknolojia ili watu wafanye maombi kupitia mifumo na kazidata.

NHC mnapaswa kufanya maamuzi ya kuruhusu Ofisi zenu za kanda kuanza kufanya maamuzi ya msingi pasipo kurundika migogoro Ofisi kuu. Kuziwezesha ofisi za kanda kufanya maamuzi na kusimamia miradi midogo kunaweza kuharakisha michakato na kuongeza mwitikio kwa mahitaji ya makazi ya ndani. Serikali, kwa kushirikiana na NHC, inaweza kutekeleza mipango inayolengwa ya ruzuku inayofanya miradi mahususi ya nyumba kuwa nafuu zaidi kwa familia za kipato cha chini na sio wakurugenzi ama watu walio na Maisha ya kiwango cha juu.​
1714654800442.png

Picha kwa hisani ya NHC
Kwa upande mwingine chanya, NHC inaweza kushirikiana na jamii na mashirika yasiyo ya kiserikali kuboresha makazi duni yaliyopo kupitia uboreshaji wa miundombinu na huduma za kimsingi. Mbinu hii inakuza ushirikishwaji wa kijamii na kutumia rasilimali za ardhi zilizopo kwa ufanisi zaidi ndani ya jamii. Waruhusu jamii ihusike katika shughuli za NHC kwa upana wake. Marekebisho haya yanalenga kubadilisha NHC kutoka shirika la kipekee hadi shirika linalojumuisha watu wote. Kwa kuziba pengo la uwezo wa kumudu gharama, kurahisisha shughuli, na kuweka kipaumbele kwa mahitaji ya watu wa kipato cha chini, NHC inaweza kuwa kichocheo cha mabadiliko chanya ya kijamii. Nyumba ya bei nafuu haimaanishi tu makazi, lakini usalama, utu, na msingi wa maisha bora kwa kila mtanzania.​
1714655041411.png

Picha kwa hisani ya Nutcache.
Ushirikiano wa Kitaifa wa NHC una uwezo wa kuwa injini pana yenye nguvu ya maendeleo ya kijamii. Kwa kutumia mbinu mbalimbali zinazoweka kipaumbele katika kumudu gharama, ufanisi wa kiutendaji, na mtazamo mpya wa kijamii, NHC inaweza kutimiza dhamira yake ya awali ya kutoa makazi bora na yanayofikiwa na Watanzania wote. Mustakabali wa mandhari ya makazi ya Tanzania unategemea uwezo wa NHC wa kuziba pengo kati ya hali yake ya sasa na matarajio ya watu wake. Kumbuka kuwa kuanzishwa kwa NHC ilikuwa jibu la serikali ili kupunguza tatizo la makazi ambalo liliwakabili wakazi wengi wa mijini wa Kiafrika.​

Sio kwa Ubaya! SIo kwa Ubaya
 
Nimelisoma andiko, na lengo ni kufanya nyumba zinazohimilika na wananchi.

Sema kwenye sehemu ya gharama hapo sasa ndio tujiulize. Ikiwa gharama ya kuijenga nyumba hiyo pamoja na ukandarasi imefikia milioni arobaini au zaidi? Tukipunguza bei yake hiyo pesa atalipa nani? Kodi?

Labda tuanze kwanza kwa kupunhuza gharama za ujenzi wake, ili kiotomati zipate kuwa na bei rafiki.
 
Back
Top Bottom