Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,014
- 144,371
Kutokana na ukweli kwamba nchi hii ina matatizo mengi yanayotokana na ukosefu wa fedha na kuwa na vipaumbele vibovu, nashauri tupitishe itakayotamka kuwa sherehe za uhuru na muungano zitakuwa zinafanyika kila baada ya miaka 2 au 3 na wakati huo huo tufute kab iisa mbio za mwenge na huu mwenge ukahifadhiwe makumbusho.
Badala yake utafutwe utaratibu mwingine wa kuadhimisha sherehe hizi kila mwaka tena ikibidi siku husika ziwe siku za kazi kama kawaida isipokuwa kwa mwaka huo wa 2 au 3 ndio iwe public holiday.
Labda tujiulize kuna logic gani ya kutumia mabilioni kudhimisha sherehe za uhuru wakati nchi haina vifaa vya uokozi wakati wa majanga?
Kuna logic gani ya kutenga mabilioni kila mwaka kwa ajili ya mbio za mwenge huku watoto wetu wanasoma katika shule za udongo zilizoezekwa kwa nyasi?
Je, hii ndio maana ya uhuru?
Bajeti ya sherehe za uhuru, muungano na kukimbiza mwenge kwa mwaka mmoja tu wa fedha, haiwezi kugharamia uanzishwaji wa Tanzania Disaster Management Agency?
Tumekosa viongozi wenye vision ya kututoa hapa tulipo na zaidi tumefeli kwa kiasi kikubwa mno katika swala zima la kupanga vipaumbele katika ngazi ya kitaifa, mikoa, wilaya, n.k.
Kwa kifupi tumekosa dira kama Taifa.