Tanzania!! Tanzania!! Tanzania!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania!! Tanzania!! Tanzania!!

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Juma. W, Apr 5, 2011.

 1. J

  Juma. W Senior Member

  #1
  Apr 5, 2011
  Joined: Mar 28, 2011
  Messages: 131
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  [FONT=&quot]Mwaka 2007 nilikuwa miongoni wa wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam waliobahatika kumsikiliza Mh. Thabo Mbeki pale Nkwame Nkrumah Hall. Alitoa hotuba nzuri iliyojaa changamoto nyingi sana. Ni muda mrefu tangu muda huo nimsikie Mzee Thabo, lakini nakumbuka sana kitu kimoja alichokiongelea kwa msisitizo mkubwa. Siwezi kuyarudia maneno yake kwaajili ya muda; lakini angalau alisema hivi “ miaka ile ya nyuma (hasa wakati wa kupigania uhuru) walizoea kuja Tanzania na hasa UDSM kupata ushauri wa kisheria. Hii ilisaidia sana kwa nchi nyingi za Afrika kupata uhuru kwa wakati”. Mzee Mbeki aliuliza swali moja “where is UDSM today?”. Alieleza hivo akimaanisha kuwa mchango wa wataalamu wetu umepungua sana hasa katika masuala muhimu. [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Naifahamu Tanzania, nawafahamu watawala wan chi yetu. Nafahamu pia kuwa nchi yetu imesheheni watalaam wengi ambao kama watatumiwa vyema nadhani tutatumia miaka michache kutuondoa tulipo na kuwa na Tanzania mpya ambayo kila mtu anatamani ije leo. [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Mara ya kwanza niliongea kuhusu “Hukumu ya mfanyakazi wa serikali” kwa kweli watu walizidi kunifungua macho na uelewa wangu kuhusu nchi hii. Leo hii ni ngumu sana kwa yeyote kuuliza “wapo wapi wataalamu tuliowasomesha kwa pesa nyingi sana? Wanafanya nini wakati nchi inaangamia na maisha yanazidi kuwa magumu? Wapo wetu wachumi wetu warekebishe huu mfumuko wa bei ambao kwa kiasi kikubwa unaletwa na hii wanayoiita “multiplier effect” kwenye mafuata na nishati zingine”? Wapo wapi wanasheria wetu ambao wamesoma pale Mlimani, Mzumbe St. Augustine, Tumaini n.k? wanafanya nini leo wakati wajanja wanaimaliza nchi yetu? Wapo wapi wataalamu wa kilimo, miaka yote hii tunatumia jembe la mkono, tunategemea mvua na kuacha maji yote yakielekea baharini wkati twafa njaa”? Wapo wapi? [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Maswali haya hayawezi ulizwa tena ikiwa serikali inawatupa au itawatupa wataalamu. Hayataweza ulizwa tena kama serikali haithani au haitathamini mchango wa wataalamu katika maendeleo ya nchi yetu. Maswali haya hayatakuwa ya msingi ikiwa engineer analazimika kufungua baa auze pombe ili ajiongezee angalau shilingi elfu hamsini imsaidie nauli ya kumfikisha kazini. Maswali hayo hayatakuwa na umuhimu wowote kama walimu wataendelea kunung’unika mara zote kwa kero zisizoisha. Maswali hayo hayatakuwa na msingi kama tutawaacha madaktari na manesi wapoteze muda mwingi kudai mishahara na malimbikizo huku wakiacha wagonjwa mawodini. Maswali haya hayakuwa na majibu kama hatakuwepo anayejali nini kinaendelea.[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]It is time for everyone to be responsible and accountable, to care, to feel and to act. Muda ule wa kumubadilisha binadamu mwenzio kwa shanga umepita. Tupo katika wakati ambao ufahamu umekuwa mkubwa. Tatizo lililopo ni kwamba baadhi ya watawala bado wanaota kutuchuuza kwa shanga. Hawa ni watu wasiofaa kwa maendeleo ya nchi yetu. Ni watu wanaowakatisha tamaa wataalamu wetu. Watu hawa wamefaulu hata kuwakatisha tama wataalamu wazuri na wakaamua kwenda nje wakafanye kazi huko.[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Tatizo letu kubwa leo ni kwamba tumeshidwa kuunganisha siasa na maendeleo. Twadhani siasa pekee inaweza kuleta maendeleo. Kutokana na uelewa huu finyu tunawekeza hela nyingi sana kwenye siasa badala ya miradi ya maendeleo. Tunatumia milioni saba kumlipa politician wakati tunawalipa wataalamu laki tano kwa mwezi. Tumesahau kuwa “politics is a dirty game”, na kuwa hata mchezaji wa huo mchezo huweza kuchafuka mara moja. Tunawalipa walimu laki kwa mwezi na mwanasiasa laki kwa siku. Tunasahau kuwa watu hawa wanaenda katika soko moja. Wote wanakula, wanalala, wanavaa, wanasomesha n.k. Tunajenga taifa la wanasiasa; bahati mbaya siasa ni mwajiri mdogo sana. [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Siasa siyo mbaya kwani ikitumiwa kama inavyotumika na wengine inaweza leta maendeleo. Kwetu sisi siasa ni mtaji, ukifanikiwa kupata “political post” umeula. Utakuwa “mheshimiwa” siyo kama profesa. Utakuwa “kigogo” siyo kama daktari. Mtu wa mamilioni ya shilingi kila mwezi hata kama husemi chochote mjengoni. Wewe “invest” tu kipindi cha uchaguzi, tumia pesa upate mamilioni. [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Tatizo kubwa tumejali sana wanasiasa, tumewajali sana hawa tukasahau watendaji. Tumewajali sana wanasiasa lakini tumewatupa wataalamu. [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Siasa yetu imeacha mwanya; haina muunganiko na uchumi. Tunaendekeza siasa za kutaka kutawala bila ya wajibu. Tunaendekeza siasa ambazo hazileti tija kwa wakati. Tunaendekeza siasa za wongo ilimradi sing’olewi kwenye cheo. Ni siasa za kizamani sana. Siasa zilizokosa shule. [/FONT]
  [FONT=&quot]Siasa ya mtindo huu itaipoteza tu Tanzania. Itawakatisha tamaa wataalamu wetu. Wataalamu wetu wengine watakibilia sehemu wanapoweza jaliwa. Nasema wengi watakimbiwa. Ni siasa ziletazo umaskini. Siasa hizi lazime tuziangalie upya. Kila mmoja wetu ana wajibu hapa. Tanzania ni ya wote, yaani mimi; wewe na yule. [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]It is time to change. Let’s join hands for a better Tanzania. We can make it.[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
   
 2. Makindi N

  Makindi N JF-Expert Member

  #2
  Apr 5, 2011
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 1,068
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  They are joining hands for kleptocracy.............
   
Loading...