Tanzania Sasa tutegemee Kupata Wachezaji Bora.

Mel James

JF-Expert Member
Jun 23, 2015
344
241
Kwa Jinsi ligi kuu bara ilivyoanza na jinsi ushindani unavyoendelea ni mambo mazuri sana. Nazipongeza sana Club ndogo kwenye ligi hii ambazo watanzania wengi walizoe kuona zikifungwa magoli Mengi na timu kubwa au kuwa na ushindani mdogo sana. Jambo hili ambalo limepelekea wachezaji wengi wa Taifa kutoka kwenye club chache na kufanya mpira wa Bongo kuwa wa maneno mengi na kushindwa kufanya vizuri Kimataifa. Ligi kwa sasa ina mvuto wa kipekee ni vuta ni kuvute point tatu kila timu inazitafuta kwa jasho kweli kweli ni mwanzo mzuri kwa mpira wetu wa Tanzania kufika mbali. Pia nawapa sana moyo hizi club zetu ambazo zinauwezo mdogo kifedha kuwa wanaweza wasiangalie ukubwa wa timu au jina la timu wa kaze mwanzo mwisho mpira sasa ni ajira kubwa. Wachezaji sasa bongo na wabunge wanaenda sawa kwa mshahara ni jambo jema sana ni fursa nzuri kwa wachezaji wetu wa ndani wajitume wasikubali kujioana hawawezi pia wasikubali kulubuniwa wacheze kufa na kupona mpira ni ajira kubwa bongo sasa. Mwisho nawaomba sana club hizi zitowe ile zama ambayo ipo mioyoni mwa watanzania wote kuwa ubingwa ni kwa ajili ya timu flani au flani, tunaomba ubingwa uwe kwa club yeyote inayoshiriki ligi kuu. Nawatakieni kila la kheri club zote pendwa za Tanzania bara katika ligi kuu hii, Pia naiombea Tanzania kupata wachezaji wazalendo na wazuri kwa ajili ya kutuwakilisha kimataifa ili mpira wetu na sisi ufike mbali.
 
Back
Top Bottom