African Believer
JF-Expert Member
- Jul 30, 2015
- 436
- 425
Nianze na mistari kadhaa iliyopo kwenye wimbo wa Lucky Dube Crazy World
Nimeinukuu hiyo mistari michache ambayo inasadifu namna hali ya kiusalama ilivyo kwa sasa nchini Tanzania, ambapo watu wanauawa na kutekwa kila uchapo leo na kundi la watu waliobatizwa wasiojulikana. Ndiyo maana mawazo yangu yakanirejesha katika historia ya zama za ubaguzi wa rangi (apartheid)nchini Afrika kusuni.
Ni katika kipindi ambacho raiya wa Afrika kisini wakikumbwa na maswahibu makubwa na wakati huohuo, waliibuka wanaharakati kutoka katika kada mbalimbali ili kujaribu kukemea na kuelezea kile kilichokuwa kinaendelea. Lakini wapo waliokaa kimya kana kwamba hakukua na kilichokua kinaendelea, hasa makaburu pamoja na wale waliokuwa wakiwaunga mkono walipinga kila lile lililosemwa.
Kama ilivyokuwa wakati ule wa ubaguzi wa rangi (apartheid) kule Afrika kusini ambapo watu mbalimbali walitoweka na wengine kuuwawa kinyama ndivyo ilivyo hivi sasa hapa kwetu katika kile kilichoitwa kisiwa cha amani.
Pamoja na yale yote yaliyoripotiwa juu ya kuokotwa kwa maiti kwenye viroba kandokando ya bahari, kuuwawa kwa viongozi wa kiserikali huko Rufiji mkoani pwani, kuuwawa kwa wanasiasa kwa kukatwa katwa na vitu vyenye ncha kali, kutekwa kwa mwanasiasa Ben Saanane, kutoweka kwa mwandishi wa gazeti la Mwananchi Azoy pamoja na matukuo mengine mengi bado kuna watu wanasema hali iko sawa kama walivyosema makaburu wa zama zile za ubaguzi wa rangi kile South Africa.
Ndiyo maana nikahisi wimbo wa Lucky Dube Crazy World unasadifu kile kinachoendelea sasa hapa kwetu Tanzania.
".......In this crazy world
People dying like flies everyday
You read about it in the news but you don't believe it
You'll only know about it
when the man in the long black coat
Knocks on your door because you're his next victim."