Tanzania Roadmap to 2050: A Monarch regime?

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
359,869
Reaction score
828,402
Hali ni mbaya sana kuliko tunavyoweza kudhani

Mabadiliko ya katiba ya ccm kumpa "mighty powers" mwenyekiti wa chama sio ya bahati mbaya.

Kupitishwa kugombea ubunge kwa wanafamilia ambao wazazi wao walishawahi kuwa marais na wengine bado wakiwa madarakani ni mpango mkakati uliosukwa vema kutawala kifamilia walau mpaka 2050.. In short utawala wa kiimla na kifalme.

Hao waliopitishwa watapata backup na watiifu wengine waliopitishwa.. Watu waoga, wasio na maono yoyote na watu wa ndio mzee.

Kama uchaguzi utafanyika kwa kura ambazo wameshaziandaa baada ya hapo ni kukamilisha tu kupanga safu zao kuanzia juu mpaka chini

Kitakachotokea ninini hapo!? Ni kitu kibaya mno.

Wakiamua kuongeza ukomo wa vipindi vya utawala hakutakuwa na kuwapinga.

Wakiamua kuuza, kugawa ama kutoa zawadi rasilimali yoyote hakutakuwa na kuwazuia.

Watakuwa na power kubwa zaidi kuliko sasa ya kufanya chochote na kwa wakati wowote bila shida yoyote!

Wenye uthubutu wote wamepigwa chini.. Baadhi yao watapozwa kupewa vyeo nje ya mfumo

Wenye maono ya mbali hao wataendelea kukandamizwa.

Wenye kuitakia mema Tanganyika hawa... Mhm tuwaombeee sana!

Kuna baadhi wamepitishwa kimkakati kwakuwa wanajulikana cv zao kwa ukatili.. Hawa ndio watakuja kuwa watu wa kuogopwa zaidi kuliko ilivyokuwa mwanzoni.

Kama uchaguzi huu utafanyika kwa kura zao feki.. Yajayo yanatisha sana!
 
Kwanza hongera kwa kufanya Projection ya miaka 25 ijayo.

Ila tukubali kuwa wananchi ambao wanamiliki nchi hawapo serious na nchi yao.

Kwakuwa tukiangalia generation ambayo ingeleta mabadiliko ya 1990s na ndo hii ilikuwa imeshika hatamu 2015 kuiondoa sisiemu madarakani .

Ndo hii imeharibiwa kwa kunywa sungura , Jobless , simba na yanga na ndo hii generation inayoenda kuwa trash.

Tungeangalia na hapo kuwa Sisiemu wanapata wapi kiburi cha kuamini hii ni nchi ya familia Fulani jibu linakuja kuwa wameua kizazi kile cha kuhoji ,kufikiri na kukosoa kwa hoja.
 
Hali ni mbaya sana kuliko tunavyoweza kudhani
Mabadiliko ya katiba ya ccm kumpa "mighty powers" mwenyekiti wa chama sio ya bahati mbaya
Kupitishwa kugombea ubunge kwa wanafamilia ambao wazazi wao walishawahi kuwa marais na wengine bado wakiwa madarakani ni mpango mkakati uliosukwa vema kutawala kifamilia walau mpaka 2050.. In short utawala wa kiimla na kifalme
Hao waliopitishwa watapata backup na watiifu wengine waliopitishwa.. Watu waoga, wasio na maono yoyote na watu wa ndio mzee
Kama uchaguzi utafanyika kwa kura ambazo wameshaziandaa baada ya hapo ni kukamilisha tu kupanga safu zao kuanzia juu mpaka chini
Kitakachotokea ninini hapo!? Ni kitu kibaya mno
Wakiamua kuongeza ukomo wa vipindi vya utawala hakutakuwa na kuwapinga.
Wakiamua kuuza, kugawa ama kutoa zawadi rasilimali yoyote hakutakuwa na kuwazuia
Watakuwa na power kubwa zaidi kuliko sasa ya kufanya chochote na kwa wakati wowote bila shida yoyote!
Wenye uthubutu wote wamepigwa chini.. Baadhi yao watapozwa kupewa vyeo nje ya mfumo
Wenye maono ya mbali hao wataendelea kukandamizwa
Wenye kuitakia mema Tanganyika hawa... Mhm tuwaombeee sana!
Kuna baadhi wamepitishwa kimkakati kwakuwa wanajulikana cv zao kwa ukatili.. Hawa ndio watakuja kuwa watu wa kuogopwa zaidi kuliko ilivyokuwa mwanzoni
Kama uchaguzi huu utafanyika kwa kura zao feki.. Yajayo yanatisha sana!
Hakuna lolote,nyie watu wa chadema mnapenda kutia hofu,na nia yenu ni kuona nchi inaingia katika machafuko.

Mfano:Asilimia tisini ya walioamua kugombea ni hiyari yao na mambo yalikuwa wazi kwa kila mtu.Jimbo la mchinga hakuna aliyejitokeza sasa kamati kuu ifanye nini?

Majina kufanana au ndugu kufanya kazi flani isiwe chanzo cha kuonekana kubebana,lkn panapo ushahidi wa wazi ni muhimu kukataa tabia hiyo,haya unayoyasema leo ni hisia,lkn jutahidi kuwa na ushahidi uone kama umma haujaamka na kukataa tabia hiyo.

Wakati Mzee Mwinyi anafanya hivyo watu waliona ni kawaida sababu pia sifa za mtoto wake zinaruhusu,Mbona Jimbo la Musoma hawapokezani?

Mbona Mkapa aliibuka mbele ya Nyerere?
Mbona Lissu ameibuka bila kuwa na backup yeyote?
Ukiwa mwanasiasa mzuri utaibuka tu bila kutiliwa shaka ya kubebwa japo dunia ina rafu nyingi.
Asalam aleykum,waislamu wenzangu.
 
Kwanza hongera kwa kufanya Projection ya miaka 25 ijayo.

Ila tukubali kuwa wananchi ambao wanamiliki nchi hawapo serious na nchi yao.

Kwakuwa tukiangalia generation ambayo ingeleta mabadiliko ya 1990s na ndo hii ilikuwa imeshika hatamu 2015 kuiondoa sisiemu madarakani .

Ndo hii imeharibiwa kwa kunywa sungura , Jobless , simba na yanga na ndo hii generation inayoenda kuwa trash.

Tungeangalia na hapo kuwa Sisiemu wanapata wapi kiburi cha kuamini hii ni nchi ya familia Fulani jibu linakuja kuwa wameua kizazi kile cha kuhoji ,kufikiri na kukosoa kwa hoja.
Asalam aleykum,muislam mwenzangu.
Kwanza ktk hoja ya kukubali kuwa wananchi wengi hawapo serious nakubaliana na wewe,pili ni kuwa mifumo haina huruma na wazembe ktk ulimwengu wa ubepari.
Nchi hii inaingia ktk ubepari halisi kwa nguvu na ndio jambo linaleta fujo kuonekana kuna watu wanabebwa.

Nchi sio ya familia,nchi hii tulizoea ujamaa ,,sasa enzi zimepita na yule mwenye nguvu ndie anapata na anaweza kukosa pia.hivyo tubadili bongo zetu kuwa za kibepari tuone fursa
 
Usipotoshe mada! Usifanye spinning kwenye mambo serious ya Tanganyika
Lazima uwaze na kufikiri kama Mtu unayejua dunia inakokwenda 🐼

Usidhani akili za Museveni ndio za Muhozi hiyo dunia ilishapitwa na wakati

Kizazi cha Mayai hakitafua dafu mbele ya kizazi cha bodaboda siku si nyingi mbeleni
 
Asalam aleykum,muislam mwenzangu.
Kwanza ktk hoja ya kukubali kuwa wananchi wengi hawapo serious nakubaliana na wewe,pili ni kuwa mifumo haina huruma na wazembe ktk ulimwengu wa ubepari.
Nchi hii inaingia ktk ubepari halisi kwa nguvu na ndio jambo linaleta fujo kuonekana kuna watu wanabebwa.

Nchi sio ya familia,nchi hii tulizoea ujamaa ,,sasa enzi zimepita na yule mwenye nguvu ndie anapata na anaweza kukosa pia.hivyo tubadili bongo zetu kuwa za kibepari tuone fursa
Unaelewa maana ya ubepari kwanza .

Utafauti wa ubapari na ujamaa upo hivi

Ubepari - Serikali inakuwa little intervation katika issue za kiuchumi ,

Na ujamaa Serikali inakuwa ndo each and everything in economically., n.k

Sasa njoo katika Concept ya mtoa mada kuwa ni sahihi nchi kuwa na mifumo ya kuruhusu familia fulani kuongoza nchi ?

Hauwezi ukachukua Ubepari Ukauingiza katika Siasa .

Kwakuwa ubepari wazungu waliunzisha target ilikuwa uchumi na sio siasa.

Ila Serikali haiwezi kuruhusu uingize bidhaa mbovu sokoni au zisizo na ubora kisa tu Serikali Ina little iintervasion in ur business.

Hauwezi kusema kila mtoto wa Rais anabidi kuwa waziri , Mbunge n.k kisa tu tupo katika dunia ya kibepari kwa kufanya hivyo ni sawa na kumruhusu Bakhressa auze kiroba cha ngano kg 25 kwa laki mbili kisa tu tumeingia katika ubepari.

Kwahiyo jaribu kuelewa ubapari unahusu nini.
 
Lazima uwaze na kufikiri kama Mtu unayejua dunia inakokwenda 🐼

Usidhani akili za Museveni ndio za Muhozi hiyo dunia ilishapitwa na wakati

Kizazi cha Mayai hakitafua dafu mbele ya kizazi cha bodaboda siku si nyingi mbeleni
NWO sio ishu tena labda kwako ndio habari mpya sana... Hiyo Ina miaka zaidi ya 30.. Hapa ni ishu wachache wanachopanga ili kurithishana madaraka kifamilia
 
Unaelewa maana ya ubepari kwanza .

Utafauti wa ubapari na ujamaa upo hivi

Ubepari - Serikali inakuwa little intervation katika issue za kiuchumi ,

Na ujamaa Serikali inakuwa ndo each and everything in economically., n.k

Sasa njoo katika Concept ya mtoa mada kuwa ni sahihi nchi kuwa na mifumo ya kuruhusu familia fulani kuongoza nchi ?

Hauwezi ukachukua Ubepari Ukauingiza katika Siasa .

Kwakuwa ubepari wazungu waliunzisha target ilikuwa uchumi na sio siasa.

Ila Serikali haiwezi kuruhusu uingize bidhaa mbovu sokoni au zisizo na ubora kisa tu Serikali Ina little iintervasion in ur business.

Hauwezi kusema kila mtoto wa Rais anabidi kuwa waziri , Mbunge n.k kisa tu tupo katika dunia ya kibepari kwa kufanya hivyo ni sawa na kumruhusu Bakhressa auze kiroba cha ngano kg 25 kwa laki mbili kisa tu tumeingia katika ubepari.

Kwahiyo jaribu kuelewa ubapari unahusu nini.
Si ajabu hata hapa tayari wana mkono wao
FB_IMG_1753878416647.jpg
 
Kwanza hongera kwa kufanya Projection ya miaka 25 ijayo.

Ila tukubali kuwa wananchi ambao wanamiliki nchi hawapo serious na nchi yao.

Kwakuwa tukiangalia generation ambayo ingeleta mabadiliko ya 1990s na ndo hii ilikuwa imeshika hatamu 2015 kuiondoa sisiemu madarakani .

Ndo hii imeharibiwa kwa kunywa sungura , Jobless , simba na yanga na ndo hii generation inayoenda kuwa trash.

Tungeangalia na hapo kuwa Sisiemu wanapata wapi kiburi cha kuamini hii ni nchi ya familia Fulani jibu linakuja kuwa wameua kizazi kile cha kuhoji ,kufikiri na kukosoa kwa hoja.
Wewe upo serious ?
 
NWO sio ishu tena labda kwako ndio habari mpya sana... Hiyo Ina miaka zaidi ya 30.. Hapa ni ishu wachache wanachopanga ili kurithishana madaraka kifamilia
Madaraka ya kifamilia walianzisha Mtei na Ndesamburo hapo Chadema kwa kuwajaza bungeni akina Grace, Lucy, Freeman kisha Lisu na Zitto wakaiga kwa kuwaleta bungeni dada zao na Dr Slaa akamleta Mtalaka wake 🌹 kabisa

Sasa kipya ni kipi hapo wanachofanya CCM? 🐼
 
Back
Top Bottom