Tanzania ni zaidi ya CCM na CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania ni zaidi ya CCM na CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kigarama, Aug 17, 2011.

 1. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #1
  Aug 17, 2011
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Wakati na muda wetu mwingi tunautumia kujadili vyama vya siasa na hususani udhaifu wa CCM na uimara wa CHADEMA. Kwanza lazima nikiri kwamba yote mawili yana ukweli. CCM ni dhaifu na CHADEMA ni imara angalau kwa viwango vyetu vya kitanzania. Lakini lazima tukubaliane na ukweli kwamba Tanzania ni zaidi ya vyama hivi viwili. Hivi vyama vinaweza kusambaratika lakini nchi yetu itabakia. Tujadil nchi yetu na hatima yake bila ya kujali sana maslahi ya vyama hivi viwili. Najua kuna watu watasema tatizo letu kwa sasa ni CCM na matarajio yetu ya baadaye ni CHADEMA, watu hawa wanajua sehemu ya ukweli tu ya tatizo letu. Tatizo letu kama jamii na nchi ni uozo uliosababishwa na ulafi wa baadhi yetu na kwa bahati mbaya watu hao wamo kwenye kila chama!! Maslahi yetu kama taifa hatuwezi kuyaweka kwenye bakuli moja, yaani siasa!
   
Loading...