Wengi hatujui tunakokwenda kwa sababu tunapelekwa! Wengi zaidi hatuhitaji kujua tunakwenda wapi kwa sababu tunaamini kwamba wapo wanaojua tunahitaji kwenda wapi badala yetu!!! Wengine hatutafuti sababu kwanini tuko hapa na tumekwama pale kwa sababu tunaamini wapo walio na majibu katika hilo!!! Tena tunakwenda mbali zaidi ya hapo, tunahitaji tufanyiwe kila kitu bila ya sisi wenyewe kuhangaika wala kujishughulisha na matatizo yanayotukabili!!! Wala hakuna hata mmoja anaeona matatizo akatafuta namna ya kuyatatua bado tunasubiri waje kututatulia wale wanaojua matatizo yetu!!!
Haitoshi!
- Wapo wanaofanya bidii kutoboa jahazi na hali tumo ndani na kimya tumekaa!!
- Wapo wanaojitahidi kusema jahazi linatobolewa lakini hakuna hata mmoja anaewasikiliza!!
- Wapo wanaofurahia kila jambo bila kujali ni jema ama ovu!!!
- Wapo wasiojua wala hawahitaji kujua chochote zaidi ya mkate wao wa kila siku wanaousumbukia!!
Hii ndio Tanzania... Nchi yetu wala si ya mwingine... lakini tunakimbia wajibu na majukumu yetu. Tunawaachia wengine watuhangaikie... wala hatujishughulishi kujua ni MBWA MWITU KWENYE NGOZI YA KONDOO au ni KOBOKO kwenye tenga la KAMBALE!! Ila ndio Tanzania yetu tutaenda wapi?! Maana mfanyakazi anaesifiwa ni yule mwenye kutajirika muda mfupi baada ya ajira - ANA AKILI SANA. Na anaesifiwa ujinga ni yule anaetegemea mshahara wake wa mwezi - ANA NINI MJINGA YULE HAMMUONI KILA SIKU YUKO VILEVILE!!! hiyo ndio Tanzania.....
Ipo siku yale ya Malkia wa Ufaransa yatabisha hodi nchi hii... kwa maana wapo waliojisahaulisha taabu na mashaka ya wananchi wao... ndio maana sasa wapo baadhi wanatumika bila kujua kwamba wanatumika visivyo!