Tanzania ni janga la kimataifa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania ni janga la kimataifa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Hakikwanza, Mar 25, 2012.

 1. Hakikwanza

  Hakikwanza JF-Expert Member

  #1
  Mar 25, 2012
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,898
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 180
  Ndugu zanguni hamjambo? Nimejaribu kufikiria kwa kina, hivi kwanini hii nchi inaombaomba misaada kila kukicha wakati tuna maliasili kibao? Ujue tunaomba mno misaada hadi tumekua kero kama sio janga ktk medani za kimataifa. Wazungu wanatushangaa sana tunavyo zunguka na bakuli kama wendawazimu wakati maliasili kibao toka hapa kwetu zinachukuliwa na zinawapa utajiri hao tunao watembezea bakuli.Hivyo nchi hii ina viongozi wendawazimu wanaotawala asilimia kubwa maiti za watu(mtu mwenye akili isiyo fanyanya kazi ni maiti), Viongozi wametugeuza Watanzania pamoja maliasili yetu kuwa mtaji wao, ukiangalia vituko wanavyo na walivyo tufanyia bila kuchukuliwa hatua utakubali kuwa kweli wanatawala maiti zinazotembea, angalia richmond, EPA, DOWANS, KIWIRA, MAJENGO PACHA YA BOT,UNUNUZI WA NDEGE NA RADA, MEREMETA, na mengine mengi yameisha kishikaji na maiti zimekubali na kuunga mkono. Amakweli Tanzania ni janga.
   
Loading...