Rushwa ni janga la kitaifa na kimataifa!

Rushwa ni janga la kitaifa na kimataifa!

isasuna

Member
Joined
Jan 21, 2012
Posts
51
Reaction score
19
RUSHWA NI JANGA LA KITAIFA NA KIMATAIFA!

Nianze kwa kuwasalimu wote wanajukwaa,

Natumaini kila mtu anajua nini maana ya rushwa na inafanyika vipi. Ila kwa kukumbushana tu kwa tafsiri isiyo rasmi ni kuwa …. "Rushwa ni kitendo cha hiari au nguvu ambapo mtu hushawishi, hutoa au kupokea kitu cha thamani kwa ajili ya kuathiri maamuzi fulani hasa ya mtu mwenye madaraka kwa manufaa yake au ya mtu mwingine". Hapa neno "thamani" halimaanishi tu fedha, magari, n.k lakini hata upendeleo wa aina yoyote.

Kwa hiyo basi ili kosa la rushwa likamilike lazima vitu vinne au vitano viwepo. Nasema hivo kwa sababu kwa upande wa serikali/umma ni vinne na upande wa kampuni binafsi vitano. Serikalini vitu hivo ni kutoa au kupokea, kitu cha thamani, kuathiri/athari na maamuzi. Wakati kwenye makampuni binafsi kuna kutoa au kupokea, kitu cha thamani, athari, maamuzi na bila mwenye kampuni kujua.

Tofauti ni hapo "bila mwenye kampuni kujua" kwa sababu kila kampuni ina taratibu zake kuhusu kutoa na kupokea vitu vya thamani. Hivyo inategemea sheria za kampuni husika. Na ndio maana unaona mfano tuna sheria ya manunuzi ya umma(Public Procurement Act, 2004, 2011) lakini hakuna Private Procurement Act. Hiyo haimaanisha kule hakuna matatizo ya manunuzi, hapana, ni kwa sababu ya masuala ya kibiashara.

Rushwa ni kosa la jinai na linaathiri sana uchumi wa nchi kuliko makosa mengine ya uhujumu uchumi. Hii ni kwa sababu athari zake ni kubwa kiasi kwamba zinampata kila mwananchi, awe wa kipato cha chini , kati au cha juu. Hayo ndio sababu tunaliita "Janga la kitaifa na kimataifa".

Kuna sababu nyingi ambazo zinasababisha mtu kutoa na kupokea rushwa. Ila kubwa ni tamaa, ugumu wa maisha na kukosa maadili. Zamani ilikuwa mtu mwizi au mla rushwa alionekana wa ajabu sana, ila siku hizi ukiona mtu ana nyumba kadhaa mjini, magari ya kifahari na maisha ya anasa hatujiulizi kapataje bali tunamsifu na kumwabudu kana kwamba ni mtu mwenye akili sana, mjanja, mchapakazi sana n.k

Leo nataka kuzungumzia namna gani unaweza kugundua kama kuna harufu ya rushwa kwenye mikataba ya manunuzi. Huku ndiko kuna rushwa kubwa za maana(Grand corruptions), achana na rushwa za traffic na dereva daladala, nurse na mgonjwa, secretary na boss wake, afisa utumishi na mwobaji wa ajira n.k. Hizo zinaisha haraka sana baada ya kukomesha huku juu kwa sababu, mfano mazingira ya kazi na uchumi ukiwa mzuri hakuna haja ya kuombana rushwa ndogondogo kama hizo.

Utakapogundua kama wewe ni raia mwema na mzalendo chukua hatua ukizingatia kuna vyombo kama PCCB, POLISI, PPRA, na vingine. Na ukihitaji msaada wa uchunguzi zaidi binafsi utatutafuta kwa sababu kuhisi tu haitoshi mana hata mtoto mdogo anaweza kuhisi hapa kuna tatizo ila kuthibitisha ndio weledi unahitajika.


1. MALALAMIKO KUHUSU UBORA WA BIDHAA AU KAZI.
Unakuta mzabuni kapewa kazi vizuri kwa makubaliano kuwa atafanya moja, mbili, tatu. Ila mwisho wa siku analeta kitu tofauti kabisa na mteja alichotarajia. Au huduma inakuwa kiwango cha chini kabisa hadi watu wanaanza kulalamika. Mfano tumekuwa tukishudia barabara, miradi mingine inafanywa chini ya kiwango na mzabuni analipwa. Ukiona hivyo ujue kuna kitu sio bure.


2. MZABUNI MOJA ANAPEWA KAZI KILA MARA.
Hapa ni pale mtoa huduma au mfanyabiashara fulani anapewa kazi flani kila inapotangazwa. Swali ni je, katika wazabuni wote yeye tu ndio huwa anatimiza vigezo kila wakati hakuna mwingine? Na kweli ukifatilia utoaji wa hiyo tenda kuna uhalisia au uhalali wa yeye kupewa kazi kila mara?


3. MALALAMIKO TOKA KWA WAZABUNI WENGINE
Mara nyingi tumekuwa tukipuuza malalamiko ya wazabuni wanaoshindwa kwenye tenda kwa kudhani ni wivu na chuki binafsi dhidi ya mwenzao aliyepata. Lakini njia nzuri ya kuweza kugundua uwepo wa rushwa ni kufanyia kazi haya malalamiko kwa kuanzisha uchunguzi wa kina ukitumia wataalamu. Wengine wanaweza wasilalamike waziwazi kwa kuogopa kunyimwa tenda wakati mwingine ila tetesi kwa pembeni lazima zipo.


4. TOFAUTI YA BEI ISIYO YA KAWAIDA KATI YA WAZABUNI.
Ni sawa siku hizi tunaambiwa tujali bajeti zetu katika manunuzi ("value for money procurement"). Lakini inakuaje upo kwenye kamati ya tenda unakuta mna wazabuni labda tuseme watano. Kati ya hao wanne wanatoa bei za 100,120,130,135. Lakini wa tano anatoa bei ya 60 kwa kazi hiyo hiyo. Lazima ujue kuna kitu sio cha kawaida.


5. TABIA ZA WAKALA WA MZABUNI
Kama wakala wa mzabuni atakuwa na ukaribu au ukarimu usio wa kawaida kwa mtoa zabuni kabla hata mteja wake hajapata kazi basi ujue kuna tatizo. Na ukifatilia utagundua nini anakifanya ambacho ni zaidi ya majukumu yake.


6. TABIA YA WAZABUNI KUJITOA KWENYE ZABUNI NYAKATI ZA MWISHO.
Inatokea unakuta wazabuni flani wanajuana wanaamua kuomba zabuni kwa pamoja lakini nia yao ni kwamba moja wao apate hiyo tenda ambayo mwisho wa siku watafaidika wote kwa sababu watashirikiana kuifanya hiyo kazi lakini kwa siri. Na utakuta bei zao hazitofautiani sana na ni ndogo. Kabla zoezi la kuchambua zabuni kuanza wanajitoa na kumwacha mwenzao. Ukichunguza hao wazabuni lazima utakuta wana uhusiano wa karibu. Au mara zingine wanaweza wasijitoe ila wanajua akipata fulani ni kwa ajili ya wote.


7. UPOTOSHAJI WA WATU WANAOTATHMINI ZABUNI
Utakuta zabuni inatolewa kwa mzabuni ambaye bei yake ni kubwa. Ukiuliza utaambiwa tunaangalia ubora wa huduma au kazi na sio bei tu. Lakini ukifatilia utagundua hata huyo aliyepewa ana mapungufu kibao tena yanaweza kuzidi hata aliyenyimwa. Mwisho wa siku unakuja kugundua kumbe kuna moja wa wajumbe ana uhusiano na mzabuni.


8. KUONGEZEWA KAZI ZAIDI YA ILIVYOTOLEWA KWENYE TANGAZO LA ZABUNI
Unakuta mkataba unafanyiwa marekebisho kiaina na mzabuni anaongezewa kazi zaidi na hivyo malipo kuwa juu zaidi. Lakini hichi kitu japo utaambiwa taratibu zilifuatwa ila ukichunguza utagundua huo mpango ulikuwepo kabla hata ya zabuni kutangazwa ili watu wapate pesa zaidi.

9. SUALA LA DHARURA NA KUTOKUWA NA MBADALA
Hii najua Watanzania wengi wanaijua. Hapa unakuta taratibu za zabuni hazifuatwi kwa sababu tu kuna tatizo limetokea ambalo linahitaji suluhisho la haraka na unaambiwa mzabuni moja tu mwenye sifa ndio yupo. Sasa hapa kuna mawili, ukweli au kitu kingine kinaendelea.

10.
ZABUNI AU MIKATABA KUTOLEWA KWA UPENDELEO WA MAKUNDI FULANI KWA SABABU MAALUM
Kuna wakati serikali au kampuni fulani inaweza ikawa na nia nzuri tu kutoa kazi kwa watu mfano labda wasiojiweza ili kuwainua katika maisha. Au mara nyingine tunasema wazawa wapewe kipaumbele zaidi kwenye miradi n.k. Wazo huwa ni zuri lakini kuna wakati mambo huwa yanafanyika ndivyo sivyo kwa sababu hayo makundi huwa yanarubuniwa na wenye uwezo zaidi. Mpaka hapo nadhani kwa kiasi fulani umepata machache kuhusu rushwa kwenye manunuzi. Lakini fahamu kuwa hii ni hatua ya kwanza. Hatua ya pili ni kufanya uchunguzi ili kuthibitisha yale mambo manne au matano kwenye kosa la rushwa. Inahitajika uchunguzi wa kina wa kutumia wataalam wa fani zote muhimu kama uhasibu, upelelezi, sheria, IT n.k. Lakini pia tuwe na sheria nzuri utayari wa kufanya hivyo na nia thabiti.


Kampuni binafsi ya uchunguzi ya Homeland Consultancy Ltd ina watalaamu waliobobea kwenye fani ya uchunguzi hasa wa makosa ya "Fraud and Corruption." Sisi tunataka kuleta mapinduzi na mchango wetu katika kutokomeza matatizo yote ya rushwa na ufisadi kwa kufanya upelelezi wa kina na kitaalamu zaidi. Tembelea tovuti yetu: www.homeland.co.tz kujua shughuli zetu au unaweza kuwasiliana nasi kupitia: info@homeland.co.tz simu +255 754 479 420. Karibuni sana.
 
Umesaidiaje taifa kuzuia, kupambana na kuelimisha jamii juu ya janga la rushwa?
 
Nianze kwa kuwasalimu wote wanajukwaa,


Natumaini kila mtu anajua nini maana ya rushwa na inafanyika vipi. Ila kwa kukumbushana tu kwa tafsiri isiyo rasmi ni kuwa …. “Rushwa ni kitendo cha hiari au nguvu ambapo mtu hushawishi, hutoa au kupokea kitu cha thamani kwa ajili ya kuathiri maamuzi fulani hasa ya mtu mwenye madaraka kwa manufaa yake au ya mtu mwingine”. Hapa neno “thamani” halimaanishi tu fedha, magari, n.k lakini hata upendeleo wa aina yoyote.


Kwa hiyo basi ili kosa la rushwa likamilike lazima vitu vinne au vitano viwepo. Nasema hivo kwa sababu kwa upande wa serikali/umma ni vinne na upande wa kampuni binafsi vitano. Serikalini vitu hivo ni kutoa au kupokea, kitu cha thamani, kuathiri/athari na maamuzi. Wakati kwenye makampuni binafsi kuna kutoa au kupokea, kitu cha thamani, athari, maamuzi na bila mwenye kampuni kujua.


Tofauti ni hapo “bila mwenye kampuni kujua” kwa sababu kila kampuni ina taratibu zake kuhusu kutoa na kupokea vitu vya thamani. Hivyo inategemea sheria za kampuni husika. Na ndio maana unaona mfano tuna sheria ya manunuzi ya umma(Public Procurement Act, 2004, 2011) lakini hakuna Private Procurement Act. Hiyo haimaanisha kule hakuna matatizo ya manunuzi, hapana, ni kwa sababu ya masuala ya kibiashara.


Rushwa ni kosa la jinai na linaathiri sana uchumi wa nchi kuliko makosa mengine ya uhujumu uchumi. Hii ni kwa sababu athari zake ni kubwa kiasi kwamba zinampata kila mwananchi, awe wa kipato cha chini , kati au cha juu. Hayo ndio sababu tunaliita “Janga la kitaifa na kimataifa”.


Kuna sababu nyingi ambazo zinasababisha mtu kutoa na kupokea rushwa. Ila kubwa ni tamaa, ugumu wa maisha na kukosa maadili. Zamani ilikuwa mtu mwizi au mla rushwa alionekana wa ajabu sana, ila siku hizi ukiona mtu ana nyumba kadhaa mjini, magari ya kifahari na maisha ya anasa hatujiulizi kapataje bali tunamsifu na kumwabudu kana kwamba ni mtu mwenye akili sana, mjanja, mchapakazi sana n.k


Leo nataka kuzungumzia namna gani unaweza kugundua kama kuna harufu ya rushwa kwenye mikataba ya manunuzi. Huku ndiko kuna rushwa kubwa za maana(Grand corruptions), achana na rushwa za traffic na dereva daladala, nurse na mgonjwa, secretary na boss wake, afisa utumishi na mwobaji wa ajira n.k. Hizo zinaisha haraka sana baada ya kukomesha huku juu kwa sababu, mfano mazingira ya kazi na uchumi ukiwa mzuri hakuna haja ya kuombana rushwa ndogondogo kama hizo.


Utakapogundua kama wewe ni raia mwema na mzalendo chukua hatua ukizingatia kuna vyombo kama PCCB, POLISI, PPRA, na vingine. Na ukihitaji msaada wa uchunguzi zaidi binafsi utatutafuta kwa sababu kuhisi tu haitoshi mana hata mtoto mdogo anaweza kuhisi hapa kuna tatizo ila kuthibitisha ndio weledi unahitajika.


1. MALALAMIKO KUHUSU UBORA WA BIDHAA AU KAZI. Unakuta mzabuni kapewa kazi vizuri kwa makubaliano kuwa atafanya moja, mbili, tatu. Ila mwisho wa siku analeta kitu tofauti kabisa na mteja alichotarajia. Au huduma inakuwa kiwango cha chini kabisa hadi watu wanaanza kulalamika. Mfano tumekuwa tukishudia barabara, miradi mingine inafanywa chini ya kiwango na mzabuni analipwa. Ukiona hivyo ujue kuna kitu sio bure.


2. MZABUNI MOJA ANAPEWA KAZI KILA MARA. Hapa ni pale mtoa huduma au mfanyabiashara fulani anapewa kazi flani kila inapotangazwa. Swali ni je, katika wazabuni wote yeye tu ndio huwa anatimiza vigezo kila wakati hakuna mwingine? Na kweli ukifatilia utoaji wa hiyo tenda kuna uhalisia au uhalali wa yeye kupewa kazi kila mara?


3. MALALAMIKO TOKA KWA WAZABUNI WENGINE Mara nyingi tumekuwa tukipuuza malalamiko ya wazabuni wanaoshindwa kwenye tenda kwa kudhani ni wivu na chuki binafsi dhidi ya mwenzao aliyepata. Lakini njia nzuri ya kuweza kugundua uwepo wa rushwa ni kufanyia kazi haya malalamiko kwa kuanzisha uchunguzi wa kina ukitumia wataalamu. Wengine wanaweza wasilalamike waziwazi kwa kuogopa kunyimwa tenda wakati mwingine ila tetesi kwa pembeni lazima zipo.


4. TOFAUTI YA BEI ISIYO YA KAWAIDA KATI YA WAZABUNI. Ni sawa siku hizi tunaambiwa tujali bajeti zetu katika manunuzi (“value for money procurement”). Lakini inakuaje upo kwenye kamati ya tenda unakuta mna wazabuni labda tuseme watano. Kati ya hao wanne wanatoa bei za 100,120,130,135. Lakini wa tano anatoa bei ya 60 kwa kazi hiyo hiyo. Lazima ujue kuna kitu sio cha kawaida.


5. TABIA ZA WAKALA WA MZABUNI Kama wakala wa mzabuni atakuwa na ukaribu au ukarimu usio wa kawaida kwa mtoa zabuni kabla hata mteja wake hajapata kazi basi ujue kuna tatizo. Na ukifatilia utagundua nini anakifanya ambacho ni zaidi ya majukumu yake.


6. TABIA YA WAZABUNI KUJITOA KWENYE ZABUNI NYAKATI ZA MWISHO. Inatokea unakuta wazabuni flani wanajuana wanaamua kuomba zabuni kwa pamoja lakini nia yao ni kwamba moja wao apate hiyo tenda ambayo mwisho wa siku watafaidika wote kwa sababu watashirikiana kuifanya hiyo kazi lakini kwa siri. Na utakuta bei zao hazitofautiani sana na ni ndogo. Kabla zoezi la kuchambua zabuni kuanza wanajitoa na kumwacha mwenzao. Ukichunguza hao wazabuni lazima utakuta wana uhusiano wa karibu. Au mara zingine wanaweza wasijitoe ila wanajua akipata fulani ni kwa ajili ya wote.


7. UPOTOSHAJI WA WATU WANAOTATHMINI ZABUNI Utakuta zabuni inatolewa kwa mzabuni ambaye bei yake ni kubwa. Ukiuliza utaambiwa tunaangalia ubora wa huduma au kazi na sio bei tu. Lakini ukifatilia utagundua hata huyo aliyepewa ana mapungufu kibao tena yanaweza kuzidi hata aliyenyimwa. Mwisho wa siku unakuja kugundua kumbe kuna moja wa wajumbe ana uhusiano na mzabuni.



8. KUONGEZEWA KAZI ZAIDI YA ILIVYOTOLEWA KWENYE TANGAZO LA ZABUNI Unakuta mkataba unafanyiwa marekebisho kiaina na mzabuni anaongezewa kazi zaidi na hivyo malipo kuwa juu zaidi. Lakini hichi kitu japo utaambiwa taratibu zilifuatwa ila ukichunguza utagundua huo mpango ulikuwepo kabla hata ya zabuni kutangazwa ili watu wapate pesa zaidi. 9. SUALA LA DHARURA NA KUTOKUWA NA MBADALA Hii najua Watanzania wengi wanaijua. Hapa unakuta taratibu za zabuni hazifuatwi kwa sababu tu kuna tatizo limetokea ambalo linahitaji suluhisho la haraka na unaambiwa mzabuni moja tu mwenye sifa ndio yupo. Sasa hapa kuna mawili, ukweli au kitu kingine kinaendelea. 10. ZABUNI AU MIKATABA KUTOLEWA KWA UPENDELEO WA MAKUNDI FULANI KWA SABABU MAALUM Kuna wakati serikali au kampuni fulani inaweza ikawa na nia nzuri tu kutoa kazi kwa watu mfano labda wasiojiweza ili kuwainua katika maisha. Au mara nyingine tunasema wazawa wapewe kipaumbele zaidi kwenye miradi n.k. Wazo huwa ni zuri lakini kuna wakati mambo huwa yanafanyika ndivyo sivyo kwa sababu hayo makundi huwa yanarubuniwa na wenye uwezo zaidi. Mpaka hapo nadhani kwa kiasi fulani umepata machache kuhusu rushwa kwenye manunuzi. Lakini fahamu kuwa hii ni hatua ya kwanza. Hatua ya pili ni kufanya uchunguzi ili kuthibitisha yale mambo manne au matano kwenye kosa la rushwa. Inahitajika uchunguzi wa kina wa kutumia wataalam wa fani zote muhimu kama uhasibu, upelelezi, sheria, IT n.k. Lakini pia tuwe na sheria nzuri utayari wa kufanya hivyo na nia thabiti.


Kampuni binafsi ya uchunguzi ya Homeland Consultancy Ltd ina watalaamu waliobobea kwenye fani ya uchunguzi hasa wa makosa ya “Fraud and Corruption.” Sisi tunataka kuleta mapinduzi na mchango wetu katika kutokomeza matatizo yote ya rushwa na ufisadi kwa kufanya upelelezi wa kina na kitaalamu zaidi. Tembelea tovuti yetu: www.homeland.co.tz kujua shughuli zetu au unaweza kuwasiliana nasi kupitia: info@homeland.co.tz simu +255 754 479 420. Karibuni sana.
 
Mnataka kushindana na PCCB au?

Mmejipangaje kupambana na mitego madhubuti kama iliyomuondoa Jerry Muro katika mzunguko wa Mass Media?

By the way, what do you earn in return? who is behind you?
 
Back
Top Bottom