Tanzania nchi yenye siasa za ajabu kuwahi kutokea duniani

Freewine

JF-Expert Member
Jan 7, 2018
257
212
Yaani nchi hii ni ya ajabu sana, chama tawala na vyama vya upinzani vyote ni majanga matupu kwa MTU makini mwenye uwezo mzuri wa kufikiri huwezi kuwa mwanachama wa chama chochote kwa sababu ni taabu tu wanayofanya.

Viongozi wa chadema kwa muda mrefu waliaminisha wananchi wapiga kura wao kwamba Mr. Edward Lowassa ni fisadi MTU hatari kabisa kwenye nchi hii, lakini Edward lowassa huyohuyo aliweza kuwanunua viongozi wa cdm na sasa wanamsifia, hilo ni kosa litakalowagharimu cdm mpaka kufa kwake.

Ukirudi kwenye chama tawala ndipo penye shida zaidi, maamuzi ya kitaalamu yanapitiswa kisiasa. Viongozi wa chama tawala hawataki kuona kipo kitu kinawakosoa hata kama wanajua fika wanafanya makosa

*wamezuia Bunge live, huku TV zingine zimeruhusiwa kurusha vipindi muda huohuo wa bunge sasa kipi bora watu kuangalia bunge au kubaki wanacheki miziki kwenye TV nyingine.
* wamezuia mijadala kuhusu upatikanaji wa katiba mpya ili kama ni kweli Rais anaona anapambana na ufisadi na udharimu viingizwe kwenye katiba ili at a tukipata viongozi wengine wajue wanatakiwa kufuata mifumo sahihi tulioiweka kwenye katiba.

Lakini viongozi wa ccm wamekataa kuliona la katiba mpya. Na Huu ni upofu walionao viongozi wa ccm wakiamini watatawala milele.

Yapo mengi ya ajabu yanayofanywa na vyama hivi vya SIASA. Kiufupi Tanzania itaokolewa na MTU mmoja atakaeaminiwa na wanachi kwenda kuikomboa nchi na atakuwa hayupo kwenye mifumo mibovu za SIASA zetu hizi, wenye IQ ndogo wanaongoza wenye IQ kubwa.
 
Ulitaka Chadema wamsifie Lowassa alipokuwa CCM? Wewe ndio mtu wa ajabu kuwahi kutokea duniani
 
Hivi kuna siasa ya ajabu kuliko ile ya kumzawadia Lissu risasi 38 punde baada kutaarifu umma kuwa Bomberdier imezuiliwa Canada?
Ndicho hicho nachokiongelea SIASA za ajabu ukihoji kinachofanywa na serikali unaonekana wewe sio Timamu
 
mbn kitila alikua anatuaminisha kuwa hamfai lakini mko nae huko? nyie ndo watu wa ajabu kuwahi kutokea
 
Nauliza swali, mlisema lowasa hashitakiki akiwa ccm je sasa yuko ccm? Mbona watu wengine mmewakamata na kuwashitaki kwa ufisadi mbona hamjamshitaki lowassa kwa huo ufisadi mliousema na mnaouimba kila mara. Mbona mmebaki vuvuzela na mna meno ya kushitaki. Mtu kila mara anawaambia nendeni mahakamani mkanishitaki kama nimekula mali yenu, hamtaki sasa si mtulie basi.

Kukataa kwenu kwenda mahakamani ni dalili za kuwa hakuna mlilonalo la ajabu ni mavuvuzela tu. Lowassa msafi na acheni ujinga wenu mwizi mnamjua.
 
Yaani nchi hii ni ya ajabu sana, chama tawala na vyama vya upinzani vyote ni majanga matupu kwa MTU makini mwenye uwezo mzuri wa kufikiri huwezi kuwa mwanachama wa chama chochote kwa sababu ni taabu tu wanayofanya.

Viongozi wa chadema kwa muda mrefu waliaminisha wananchi wapiga kura wao kwamba Mr. Edward Lowassa ni fisadi MTU hatari kabisa kwenye nchi hii, lakini Edward lowassa huyohuyo aliweza kuwanunua viongozi wa cdm na sasa wanamsifia, hilo ni kosa litakalowagharimu cdm mpaka kufa kwake.

Ukirudi kwenye chama tawala ndipo penye shida zaidi, maamuzi ya kitaalamu yanapitiswa kisiasa. Viongozi wa chama tawala hawataki kuona kipo kitu kinawakosoa hata kama wanajua fika wanafanya makosa

*wamezuia Bunge live, huku TV zingine zimeruhusiwa kurusha vipindi muda huohuo wa bunge sasa kipi bora watu kuangalia bunge au kubaki wanacheki miziki kwenye TV nyingine.
* wamezuia mijadala kuhusu upatikanaji wa katiba mpya ili kama ni kweli Rais anaona anapambana na ufisadi na udharimu viingizwe kwenye katiba ili at a tukipata viongozi wengine wajue wanatakiwa kufuata mifumo sahihi tulioiweka kwenye katiba.

Lakini viongozi wa ccm wamekataa kuliona la katiba mpya. Na Huu ni upofu walionao viongozi wa ccm wakiamini watatawala milele.

Yapo mengi ya ajabu yanayofanywa na vyama hivi vya SIASA. Kiufupi Tanzania itaokolewa na MTU mmoja atakaeaminiwa na wanachi kwenda kuikomboa nchi na atakuwa hayupo kwenye mifumo mibovu za SIASA zetu hizi, wenye IQ ndogo wanaongoza wenye IQ kubwa.
Wewe ndio.mtu wa hovyo kuliko hata hivyo vyama.vyenyewe, yaani wewe ndio unataka.kujifanya mtu makini kuliko wenye vyama na sisi wafuasi wao tuliopo?

Haka ni kaugonjwa.ka akili. Mkuu anangalia uditupwe milembe.
 
Back
Top Bottom