Junius
JF-Expert Member
- Mar 11, 2009
- 3,181
- 139
WAANDAMANA KUDAI 'HAKI' ZAO.
Mashoga hao waliokuwa wamevalia nguo za kike huku wakiwa wamejiremba kushinda hata wanawake wenyewe, walionekana wakikatiza mtaani wakiwa wameshikana mikono na kuimba nyimbo ambazo ziligusia sababu za wao kuamua kuchukua uamuzi huo.
Walieleza kuwa, wameamua kufanya hiyo kutokana na kupuuzwa kwa madai yao hivyo kujaribu kutumia njia hiyo ya kuandamana ambayo wanadhani itawafanya wahusika waone wako 'siriasi' na kile wanachokitaka.
Miongoni mwa mambo waliyokuwa wakiyalalamikia wanaume hao ambao si riziki ni pamoja na kunyanyapaliwa na kuonekana kama wasio na haki ya kuishi nchini humo.
Aidha, mashoga hao waliitaka serikali kuharakisha kutunga na kupitisha sheria itakayotambua uwepo wao katika jamii na kuwaruhusu kuolewa kama inavyofanyika kwa wanawake bila mizengwe yoyote.
Katika maandamano hayo yaliyovuta macho ya wengi kiasi cha baadhi ya shughuli za kijamii kusimama kwa muda, wanaume hao walionekana wakitembea kwa mikogo ya kike na kutinga vivazi vya kimitego huku vikiacha wazi vigimbi vyao pamoja na 'magadeni lavu' yao.
Baadhi ya watu waliotoa maoni yao juu ya maandamano hayo walisema kuwa, dunia inakoelekea ni kubaya kwani kama wanaume wanafikia hatua ya kutaka kutambulika kama wanawake ni hatari.
"Jamani hivi tunakwenda wapi? Wanaume kweli na ma.... yao wanafikia hatua ya kujigeuza kuwa wanawake na kuandamana ili watambulike? Nadhani watakuwa wamelaaniwa na inawezekana huu ukawa ndio mwanzo wa mwisho wa dunia," alisema mtoa maoni aliyejitambulisha kwa jina moja la Suzzy.
SOURCE: RISASI