Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 16,987
- 20,271
Mimi nataka maisha mazuri tu hata kama hakutakuwa na uhuru, ukombozi au mapinduzi. Njaa na mbu wamenichosha.
Kwani uhuru, ukombozi au mapinduzi ni nini?
You tell me.
Kitendo cha wewe kutaka maisha mazuri tu tayari nikuwa unahitaji UHURU
Unachanganya madude. Kwanini wachina wana uhuru?
Uhuru upi? Uhuru unatafsiri nyingi hasa unaposimama ktk tuko husika!
China ni nchi huru na watu wake wapo huru,
Lakini china ilaumiwa na jumuiya za kimaghari kwa usimamiaji wa katiba na sheria za nchi hiyo yenye wakwasi wengi
Kumbe unazijua tafsiri nyingi za uhuru? Katika hizo tafsiri kuna moja au mbili zitakazoonyesha tupo. Sasa tatizo lipo wapo?
Tatizo ni watanzania tunahitaji lipi kati ya Uhuri,Ukombozi na Mapinduzi?
Hivyo vitu vilishafanyiwa kazi miaka 50 iliyopita. Matatizo yaliyobaki ni kupambana na maradhi, umasikini na ujinga. Chagua kimoja wapo hapo na pambana nacho. Mtoto wako anatambana na kingine na mjukuu waku anamalizia kazi.
Unataka kurudia mambo aliyofanya Nyerere miaka 50 iliyopita, huko mwezini tutakwenda lini?
mi naona tunahitaji zaidi mapinduzi na ukombozi wa fikra, kwa vile uhuru wa ndani ya nchi tunao tayari. labda uwe unaongelea uhuru wa kimahusisno kati ya nchi yetu na zingine huko duniani.
Hivi kuna tofauto kati ya kwenda shule na mapinduzi na ukombozi wa fikra?
tofauti ipo
unaweza ukaenda shule lakini ukawa hujakomboka kifikra, unaweza ukaenda shule na ukashindwa kufanya mapinduzi vilevile japo shule inaweza kuwasaidia baadhi kukomboka kifikra na kusababisha mapinduzi.
hata ukimsoma karl marx utaona middle class ndio huleta mapinduzi, hao sio wale wenye phd after all hao wenye elimu za juu sana huwa wameridhika kuwategemea kuleta mapinduzi ni shida kidogo.
IL;
Tofauti inakuja kwa sababu watoto wanahudhuria shule lakini hawasomi. Watu wanakwenda makazini lakini hawafanyikazi. Lakini tungekuwa na moyo ya kufanya vile tunavyopanga japo kwa 75% basi huu mjadala usingekuwepo.
Uwezi kupiga risasi bila kulenga shabaha na utegemee kupata targets zako. Wafundishe vizuri wanafunzi na baadaye uwape uhuru wa kufikiri na kuongea, watakushangaza na jinsi wanavyotumia elimu yao.
Ukombozi wa fikra mnaosema hapa ni branding ya slogans za miaka ya nyuma zilizopita. Hakuna tofauti kati ya kufuta ujinga na ukombozi wa fikra.
Usiku mwema.
Z-10
mkuu zakumi naomba kupingana na wewe
si kweli kila aendae na kusoma akawa amefunguka kifikra, nakukatalia kwa sababu hata akisoma vp akaelewa kama anachosoma chenyewe kimelenga kumfunga ama hakijawa katika lengo la kumfungua hata apate A kila siku anaweza kabisa akawa amefungwa kifikra. hajafunguka kifikra.
ni aina gani aya elimu mtu huyo anayopata ndio hapa tunachosema.
kufanya kazi au kutofanya kazi ni jambo jingine la mjadala lakini suluhu yake ni mapinduzi. sijui unanipata.
ni sawa na kusema si kila aliyeenda shule ameelimika. sawa kabisa na kusema si kila aliyesoma amefunguka kifikra.
jitu limekremisha miformula tu ya shuleni cheti kizuri lakini uwezo wake wa kufikiri juu ya mambo mbalimbali ya maisha na suluhu zake ni mtihani kwake. hawa utasemaje kiongozi wangu.
Bibi Chuma;
Kiswahili lugha yangu ya pili kama kiingereza. Labda ukunielewa katika posti yangu ya mwisho kabla ya hii. Nimesema ukimfundisha mtu vizuri na kumpa uhuru atafanya mambo mengi sana na kustaajabisha kwa jinsi anavyotumia akili zake. Shule nyingi za Tanzania ni vituo vya kulelea watoto lakini hakuna mafundisho.
Tukirudi kwenye posti yako, watu wana krem formula sio kwa sababu wanapenda kufanya hivyo. Ukiwa na waalimu wazuri hakuna mtu atakayepoteza muda kukrem. Hivyo hakuna sababu ya kuomba mapinduzi ya kielimu wakati huna walimu wa kufundisha. Yakitokea mapinduzi ya kifikra leo, viongozi wa mapinduzi hayo watakimbilia kazi za ofisini na kuwaachia waalimu hawahawa kufundisha.
Chuo cha kwanza kujengwa na wananchi Tanzania kilikuwa ni chuo cha kivukoni (July 1961). Chuo ambacho kilikuwa na lengo kukukomboa kifikra. Miaka zaidi ya 50 leo watu bado mnataka ukombozi mwingine. Something must be wrong.