Tanzania na Saudia Arabia Kushirikiana Kisekta

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
741
479
Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Ali Mwadini amekutana na Mhe. Dkt. Abdullah bin Abdulaziz Al-Rabeeah, Msimamizi Mkuu wa Kituo cha Huduma za Kibinadamu cha Mfalme Salman wa Saudi Arabia kujadili ushirikiano kwenye sekta za afya, elimu na miundombini baina ya Tanzania na Taasisi hiyo.

Dkt. Al-Rabeeah ameahidi kuendeleza mpango wa Kituo hicho kuwasaidia watoto wenye uhitaji wa matibabu ya magonjwa ya moyo na kufanyiwa upasuaji. Kituo kinatarajia kupokea watoto pacha waliogandana kutoka Tanzania hivi karibuni kwa ajili ya kutenganishwa.

20230607_210641.jpg
 
Kwa sasa sio mda waarabu ni adui no mmoja wa Tanzania sisi kama wananchi wanatakiwa ondoka ndani ya nchi hii mara moja, watake wasitake wataondoka tu, hatuko tiyari watufanye watumwa ,shame
 
Back
Top Bottom