CHAMA cha demokrasia na maendeleo bila shaka ni chama imara ila kinatatizo moja tu la uongozi. UONGOZI ULIOPO umeshindwa kabisa kusoma alama za nyakati.
mkuu somaga methali mgema akisifiwa....................Sasa kimekuwaje ''chama imara'' kama hakina uongozi mzuri??????
Kama UKO FAIR & SQUARE -- Angalia CHAMA CHA MAPINDUZI... UONGOZI wao wa JUU UKOJE???? SIO wa KINAFSI?
Ni Maamuzi ya MTU MMOJA TU --- HUYO MWENYEKITI -- Ni kwanini yeye kaamua Vyeo Vya KAMATI KUU hataki MAWAZIRI wavishike??? Ilikubalika Kidemokrasia Ndani ya MKUTANO MKUU wa CCM?
Ni Wapi ILISHINIKIZA ya kuwa MWENYEKITI wa CHAMA CHA MAPINDUZI ndie mwenye SAUTI YA MWISHO kwenye kuchagua WAJUMBE watakaopata kura NEC au MKUTANO MKUU???
HIYO NI DEMOKRASIA???
Na ni kwanini Basi Mwenyekiti wa CHAMA ndie lazima AGOMBEE URAIS? HIYO SIO MIZENGWE ya KIKOMINISTI?
Nilizani mwishowe utatoa matusi, maana wafuasi wa CDM wanaposhindwa kukabiliana na ukweli huishia kuporomosha matusi.
Sent from my GT-I9192 using Tapatalk
Opinion leaders wapo.
Tunakosa vitu viwili..kwanza tulichokosa ni platform iliyo huru na focused (mfano tbc inarepresent status quo), itv ni consevative na sio wabunifu wana bias, clouds media wanafiki, star tv bado wapo enzi za ujima/enzi za herode kuna saa najiuliza ivi star tv hawaoni kua wapo nyuma ya wakati?.. Jambo la pili tanzania hatuna wanahabari extraordinary km larry king ama aina ya akina richard quest. Waandishi wa habari hawaheshimiki,are just ordinary people, hawjiamini na inatia wasiwasi uwezo wao.
Mfano. Hata raisi aite wahariri pale ikulu hamna mwandishi anaethubutu kumuuliza maswali magumu, utasikia wanauliza mh raisi umejipangaje, vipi maoni yako. Ooh mh raisi tumesikia sikia inaboa sana! Hata ukienda kwenye hizi media wanakupangia uongee nini, mfano kipindi cha mgongano wa hoja itv ukisema viongozi wa tanzania ni wabinafsi,au wadhaifu utaona deo reyunga anakunyanganya mic..ukienda kwa makwaia hajui kuhoji..mfano tulienda kwenye kipindi chake katika kuongea nkawa nimesema.
Jeshi la police nalo ni sehemu ya tatizo la ubakaji wa democrasia nchini,Nkaendelea kusema Said Mwema ameshindwa.....(Hata sijamalizia kusema nlichokua nimenuia akanikatisha). Akadakia weewe umesema Said Mwema ameshindwa si ndio? Hebu tuende kwa ndugu yangu hapa, (akamuuliza nlieenda nae kwenye kipindi "mwenzako kasema saidi mwema hafai na ameshindwa wewe unasemaje"..ukitizama aina ya interview ya makwaia ni ya kichonganishi.
Yapo mengi natizama kipima joto hamna kitu, sehem yenye uhuru ni hapa JF tuu..nadhan mliona interview ya mh Zitto
Mimi hili la waandishi kuitwa na kukodoa mimacho tu na ku record chochote wanachoambiwa linaniudhigi sana... basi tu...yani mtu unaona kabisa kuna maswali; lakini waandishi wao ---------- kama audience tu ya press conferences...kwa kweli waandishi wetu siwaelewi kwa nini hawajiamini....
nyumba kubwa, katika eneo lenye matatizo nchini ni hii fani ya habari. Siwezi kuongeza zaidi ya ulichokieleza kuhusiana na waandishi.Ila la opinion leaders bado tuko nyuma si kutokuwa na wanedeshaji vipindi waliobobea tu ila hata hao wasomi wetu unauta wanaongea ili wapewe vyeo (nionavyo mimi). wengi wanaongea kwa kujipendekeza nyeupe wanaita nyeusi....
Nchi za wenzetu unakuta prof akiitwa na chombo cha habari ni sifa kubwa si kwake ni kwa chuo kizima na akienda huko anatema cheche...ukipita mwaka alichoongea kinageuka sera....(nimeshashuhudia sana hii)
Na hao host wanaalika msomi tokana na machapisho yake...si kwa kuwa ana network...wanajua kuna so and so ni mzuri kwenye hii sector ngoja tumualike...kwa maana nyingine wana habari wanasoma na kufuatilia mambo...ili kujua nani mkali na anastahili kualikwa kwenye TV au Radio.
Sasa msomi ukishakuwa politician hata serikali inakuwa haina interest na unachoongea (wanasema tu mpinzani huyo) maana hamna anayeamini kuwa uko objective...
nyumba kubwa, katika eneo lenye matatizo nchini ni hii fani ya habari. Siwezi kuongeza zaidi ya ulichokieleza kuhusiana na waandishi. Ninachoweza kusema ni kuwa ili mtu awe mwandishi mwenye weledi wa kuhoji, kuuliza na kuzungumzia mada ni lazima awe msomaji wa habari, mtafiti katika maandishi na mwenye kiu ya kujua mambo.
Waandishi wengi hawawezi kuuliza au kuhoji mambo kwa kutokuwa na weledi wa mada husika. Kwa mfano, waandishi wataitwa kwenye press conference ya kiongozi kutoka Srilanka. Zaidi ya kujua Srilanka katika Atlas hawajui kingine zaidi.
Mwandishi huyo hawezi kuzungumzia lolote kuhusu Tamil Tiger au kudadidis interest ya Srilanaka na Tanzania.
Mwandishi hajui historia na jiografia ya India, Pakistan na Bangladesh atawezaje kuzungumzia mzozo wa Kashmir.
Siyo kwamba wanafanya makusudi ni kwamba hawana exposure na wala hawataki kufahamu hilo.
Fareed Zacharia wa CNN aliitwa White house kufafanua siasa za Pakistan, Afghanistan na eno la middle east kutokana na weledi wake ambao akiuelezea utaridhika kuwa anajua anachosema.
Tatizo la pili ni woga. Katika waandishi wenye weledi wengi wanasubiri fadhila au ni waoga wa kusema kile wanachokiona.
Na kwasababu fani ipo taabani ni ngumu kupata Opinion leaders wa kuzungumzia mada mbali mbali. Kwa wenzetu opinion leader wanatumia habari za utafiti utoka vyombo vya habari ili kutoa mchanganuo wa kina zaidi kwa wasomaji na wasikilizaji.
Opinion leader anaweza kuwa na political affiliations, kinachomtofautisha na political pundits ni ule uwezo wa kulizungumzia jambo objectively.
WOWOWO ombwe unalolizungumzia si tatizo mmoja naweza kusema ni 'cascade of reaction'
Opinion leaders pia wengi hawafanyi tafiti na pia waandishi wengi.Inakera na kuna ombwe kubwa sana.Kuna kituo kimoja kilinialika nikategemea kuwa nitaulizwa maswali deep sana lakini kilichotokea nilikua disappointed kwa kiasi fulani
CHAMA cha demokrasia na maendeleo bila shaka ni chama imara ila kinatatizo moja tu la uongozi. UONGOZI ULIOPO umeshindwa kabisa kusoma alama za nyakati, unapokuwa na viongozi ambao kwao kila wanaetofautiana ni threat hapo uongozi kimsingi unakuwa dhaifu na kuanza kufukuza wale wanaowaona either ni threat au wanawapa changamoto.
Mfano mzuri MH SHIBUDA akihojiwa hot mix mwezi uliopita alikiri wazi kwamba nilizani CHADEMA nitakuwa na uhuru wa mawazo lakini nimekuta yaleyale nilioyakimbia ccm nikitoa mawazo tofauti naitwa msaliti au pandikizi la ccm, zamani ccm waliniita kibaraka wa upinzani au ww si mwenzetu sasa nashangaa hata upinzani nao wanafanya upuuzi uleule wa ccm wa kutotaka changamoto. embu ndugu fatilia mh clinton alipata hofu kubwa baada ya kusikia obama nae anataka kugombea na alifanya kila aina ya ubaya ili obama asichaguliwe lakini mwishowe alikiri kuwa kiongzi sio tu kutamani bali uonekane kweli kwa vitendo,mfano mwingine ni kule sudani kusini ambapo viongozi dhaifu huwakimbia wapinzani wao kwa kuwafukuza na baadae kuleta vurugu kubwa kwenye jamii.
chama makini kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu viongozi wake wangejikita katika kuimarisha chama kwa mikutano makonganmano lakini si kujikita katika kuwamaliza waleta changamoto.
NOTE
KUKIMBIA CHANGAMOTO NI DALILI YA UDHAIFU ,, KICHWA KIKIUMA UNAKUNYWA DAWA SI KUKIKATA KWANI UKIKIKATA HATA MWENYEWE UTAKUFA.