Tanzania na Ombwe la Opinion Leaders, Tutafika?

WOWOWO

JF-Expert Member
Aug 3, 2011
590
500
Wana Bodi kwa kawaida katika taifa lolote lazima kuwe na mijadala yenye afya ambayo hutumika kama dira ya kuleta mabadiliko na maboresho katika masuala mbalimbali yahusuyo jamii na taifa kwa upana wake.

Moja ya sekta ambayo inapaswa kuongoza kwa kuibua mijadala ni vyombo vya habari kupitia kuandaa vipindi vya mijadala na kuarika watu weledi (Naomba tuwaite Opinion Leaders/Makers) ambao wataongozwa na Mwandishi aliyebobea katika uchokonozi na kuwafanya wageni wake (Opinion Leaders) waweze kutoa michango ambayo itakuwa guideline katika issues mbalimbai zinazoibuka katika jamii yetu.

Niweke wazi kabisa kwamba opinion leaders ni aina ya watu waliobobea kwenye masuala mbalimbali katika jamii ambao kwa kawaida kunapotokea issue yoyote burning katika jamii basi vyombo vya habari na kila mtanzania anakuwa very curious kusikia nini watasema na kwa maana hiyo kuwa kama dira ya jambo lililoibuka.

Faida za Opinion Leaders katika jamii ni nyingi sana lakini baadhi ni pamoja na kukuza kisima cha fikra katika jamii, kuwa dira ya mijadala ya kitaifa, kusaidia kupatikana kwa fikra za kulisogeza taifa letu mbele, kuset agenda mbalimbali za kitaifa na kubwa zaidi kuwafanya wananchi kuwa na uelewa wa kina, misimamo na baadaye maamuzi sahihi katika issues mbalimbali za kitaifa.

Hata hivyo, pamoja na umuhimu huo wa Opion Leaders katika kujenga afya ya mijadala, Taifa letu linakosa tunu hiyo muhimu kwa maendeleo. Vyombo vya habari vimekosa programu zenye kuibua mijadala na fikra nzito na baadhi vimebaki kuwa mawakala si tu wa kuzima mijadala bali pia kuiharibu jamii ili isiwe na uwezo wa kushiriki mijadala hiyo.

Naomba niazime mifano ya vipindi kama This Week in Perspective (TBC), Kipima Joto (ITV), Tuongee Asubuhi (Star TV), Je Tutafika? (Channel 10), General on Monday (Channel 10), Hamza Kasongo Hour (Channel 10), Medani za Siasa (Star TV) na vingine ambavyo nimevisahau, vimekaaje? Vinasaidia kweli katika kuibua mijadala na kuset agenda za Taifa? Vinakidhi kweli haja? Jibu ni hapana.

Binafsi naviona kama si tu vimeshindwa kufikia viwango lakini pia hata vile vilivyokuwa vimejaribu kuchomoza hasa vile vya Je Tutafika cha Makwaiya wa Kuhenga, Kipima Joto cha ITV na Tuongee Asubuhi cha Star TV vimeporomoka ghafla na kupoteza mvuto kabisa.Kwa ujumla hatuwezi kuvitegemea kwa uhuru, uwazi, weledi na bila kuegemea upande wowote katika kuibua na kujadili issues nzito za kitaifa

Hata hivyo, kuna maswali ya kujiuliza hapa.Je huenda vipindi hivyo vimekosa mvuto kutokana na ombwe la Opinion leaders? Au waandaaji wa vipindi wanakosa mbinu na weledi? Lakini swali lingine inawezekanaje waandaaji hawa wa vipindi waka brach na kuhost wageni (Opion leaders) kutoka almost kila nyanja? Wanaweza kumudu kila taaluma?

Ukweli mchungu ni kuwa kama Taifa TUNA OMBWE LA OPION LEADERS/MAKERS ndiyo maana kwa muda mrefu tumekosa ajenda za kitaifa, mijadala yenye afya na kujenga na mara nyingi tumekuwa ni wa kushangilia matukio na yanapopita tunasahau kila kitu.

Naomba nitaje baadhi ya mijadala ya hivi karibuni tu ambayo naamini imekufa kutokana na ombwe tulilonalo la Opinion Leaders/Makers na vyombo vyetu vya habari kushindwa kukidhi haja..Ripoti ya Brig. Ngwilizi kuhusu Wabunge kupokea Rushwa, Tundu Lissu na Majaji bandia nchini, Sakata la Meno ya Tembo kukamatwa Hong Kong, Uchaguzi wa kimafia wa Meya wa Ilemela, Kashfa ya Polisi na Makuruta feki nk. nk.

Unaweza ukafikiria tu; hivi ni wasomi gani tulionao kwa sasa ambao wanaweza kujadili issues za kitaifa kwa weledi, uwazi, umakini na bila kubebwa na unazi/itikadi? Ukweli ni kwamba idadi ni finyu sana na ya kukatisha tamaa. Wengi wao wamekuwa waingiza mikono kwenye makoti ya wakubwa na kwa maana hiyo mambo mengi mazito yanapeperuka kama upepo na hakuna anayejali wala kuyashikia kidedea.

Kazi hii ya Opinion Leaders sasa imebebwa na Wanasiasa, kila siku utakumbana na Dkt.Bana, Dkt.Kitila Mkumbo, Dkt.Slaa, Kinana, Nape, Zitto, Mangula, Mnyika, Mbowe, JK, Shibuda, Lema, Kafulila nk.nk.Hatuna mijadala ya kiweledi na elekezi.Tumekufa ganzi. Hata akina Prof. Shivji (ambaye kwa sasa ndiyo naona yuko impartial) hawas
 
vukani

JF-Expert Member
Dec 30, 2009
245
195
Mimi nadhani JF ingetumiwa vizuri kama opinion leader kama ulivyosema tungefika mbali.

Hebu chunguza mijadala mingi inayoanzishwa humu inavyojadiliwa na wadau mbalimbali wenye uchungu na nchi yao bila kujali kwamba wapo nchini au wako nje ya nchi.

Siamini kama hivyo vipindi vya TV vina msaada wowote kwa taifa zaidi ya porojo tu.
 
Mchambuzi

JF-Expert Member
Aug 24, 2007
4,853
2,000
WOWOWO,

Naunga mkono hoja; lakini tatizo ni kwamba kama ulivyojadili, Politics has become supreme to everything, supreme even to rationality and common sense; Ndio maana kila mtu aidha anakimbilia kuwa a PhD hata kwa kuchakachua au anakimbilia uongozi wa kisiasa kwani anajua akifanikisha kati ya haya, atapewa a prominent role na kuwa influential katika jamii au akiwa mmoja ya maswahiba wa kiongozi wa nchi, jamii itawaheshimu;

Tatizo lingine ni kwamba mtu anakuwa muhimu pale tu anapokuwa na madaraka, anayatumiaje na kwa faida ya nani? hilo halipewi nafasi; Na ikitokea kiongozi husika anapoteza madaraka, hoja yake hata kwenye ukurasa wa michezo wa gazeti haitawekwa; Wealth, Prestige, Social Status, and Power ndio vigezo vikuu vya watu kutumika kama opinion leaders, bila ya kujalisha wamefikiaje hayo - on merit? uadlifu? utiifu wa sheria? elimu? uzalendo? mfano wa kuigwa na jamii? haya yote hayajalishi;
 
Last edited by a moderator:

Mutakyamirwa

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
4,943
1,500
Mkuu WOWOWO,

Mada yako umeidadavua vizuri. Kwanza kufika tutafika ila kwa kuchelewa sana. Sababu za kuchelewa kwetu hizi hapa: Umaskini umekuwa kisababishi kikubwa-wengi wanafikiria kuiba, kutajirika haraka n.k. Pili mfumo wa elimu yetu unazalisha hakiri mgando-no creativity, fast thinking and making decisions rightly and quickly. Wakati mwingi najiuliza mengi juu ya taharuma ya uandishi na sipati majibu.

Hebu fanya random sampling kwenye vyombo vyetu vya tv-mtagazaji nani anayeweza kuuliza maswali ktk nyanja za kisiasa, kiuchumi na kijamii ktk viwango vya hard talk ya cnn/bbc na 101 ya eljazeer?

Tulipotaka kupima weledi wa viongozi wetu kupitia mahojiano wakati wa uchaguzi 2010 nini kilitokea kwa chama tawala?

Kumbuka nini kilitokea ktk mijadara ya kugombea urais 2010 namaswali yaliyoulizwa na waandishi njaa? Tumewaikujiuliza kwanini hakuna midaharo ya kuwapima viongiozi wetu? Infact si muda mlefu kwa utaratibu huu ikulu ataingia kichaa-kama hajakuwepo.

Tanzania!!! Tanzania!!! Nani ametuloga? Viongozi wetu wanasema uongo hakuna wakuwawajibisha! Mfano, na sitalisahau kamwe pale Rais alipowambia wafuasi wake Dodoma 'hata mie simjui mmliki wa Dowans'.
 
Rweye

JF-Expert Member
Mar 16, 2011
16,666
2,000
hao tunao ila tuna upungufu wa patriotic leaders who can stand strong on issues
 
blueray

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
2,217
0
WOWOWO,

Ni wazo zuri. Ila nijuavyo mimi, though by nature I am not pessimistic, hata kama mwanzo litapata mwitikio mzuri haitachukua muda mrefu kufeli.

Kushindwa ni dhahiri mifano wewe mwenyewe umetoa mifano ya kushindwa kwa vipindi mbalimbali kama ulivyovitaja hapo juu.

Kitu ambacho hujakichambua ni sababu ambazo zimefanya vipindi hivi kupoteza mvuto au hata kushindwa kukidhi kiu ya wanajamii.

Ukweli ni kwamba katika nchi hii kumezuka kundi dogo kwenye jamii, kundi lenye nguvu na uwezo wa kudhibidi media na hata kudhibiti mtu mmoja mmoja. Ni kundi linalozingatia maslahi binafsi, lenye uwezo Wa kudhibiti vyombo vya dola kama taasisi ya urais, bunge, mahakama na vyombo vya ulinzi na usalama wa nchi.

kundi hili dogo ndio tunaowaita mafisadi. Mafisadi wanaingilia kazi nzuri za watu wazuri wanaijitokeza kuwa opinion leaders kwa maslahi ya wananchi. Wanaingiliiwa kwa kupewa hongo ili waongee yale yanayowapendeza wao na hongo ikishindikana hupata vitisho vikali ikiwemo kutishiwa maisha yao.

Vyombo vingi-au tuseme vyombo vyote-vya habari hupata vitisho mbalimbali ikiwemo hata uwezekano wa kufungiwa vituo vyao kama wataruhusu mawazo huru.

Hii ina maana kwamba sasa hivi tuko kwenye kipindi ambacho hakuna uhuru wa mawazo. Hata wale watu tunaotegemea kuwa opinion leaders tayari ni waoga kutokana na vitisho wanavyopokea pindi wanapojitokeza kuwa Na mawazo huru.

Baadhi ya wanasiasa hasa kutoka upande wa vyama vya upinzani unaowaona kusimamia upande Wa wananchi ni wale waliojitolea maisha yao kupambana na huu ufisadi unaoziba sauti ya wanyonge kila sehemu kwa kutumia nguvu za dola na kudhibiti vyombo vya habari.

Wanasiasa wa upande wa chama tawala wanaongea kifua mbele kwa sababu wengi wao wako upande wa mpini.

Mkuu hata hapa jf watu kutotumia true identity zao ni Matokeo ya uhuru wa maoni uliodhibitiwa. Watu hawana uhuru wa kusema mawazo yao bila uoga.

Kazi kubwa tuliyonayo ni kupambana na woga na ujinga wa kukubali kudanganywa na hili kundi la watu wachache kwa manufaa yao. Badala yake tujiweke huru, tuwe watanzania na tutoe mawazo yetu kwa manufaa ya wote na taifa letu kwa ujumla.
 
Last edited by a moderator:

mambomengi

JF-Expert Member
May 16, 2009
829
250
Nafikiri ni uoga wetu ndio unachangia zaidi.

Yeyote atakaye toa mawazo gongano na serikali atachukuliwa hatua madhubuti. Bila kusahau wengi wetu sio wasafi. Ukiichambua sera ya serikali kama karanga kesho unakamatwa kwakuwa moja ya biashara yako hukulipa kodi sahihi. Halafu njaa nyingi miongoni mwetu kiasi kwamba inakuwa ni rahisi kununuliwa kimawazo.

Tufanyenini? Tujisafishe kwanza wenyewe ili wadhalimu wasipate cha kusingizia halafu tuanze toa maoni na mawazo yetu kwa uwazi.
 
Kitila Mkumbo

JF-Expert Member
Feb 25, 2006
3,350
2,000
Opinion leadership ya kweli huwezi kuitenga na siasa. Hatuhitaji opinion leaders ambao ni neutral (if this is what you mean by 'impartial), bali tunahitaji wale ambao ni objective. Impartiality and neutrality are very close to indifference!

Kosa lingine ambalo unaelekea kulifanya ni ku-judge 'impartiality' ya mtu kwa kuangalia kama ni mwanachama wa chama cha siasa au la. Kuwa mwanachama haina maana huwezi kuwa objective, na kutokuwa mwanachama wa chama cha siasa hainamaanisha ndio umekuwa impartial or neutral.

Ma-opinion leaders wazito kibao tunaowajua walikuwa wanachama na wakati mwingine viongozi wa vyama vya siasa. Hawa ni pamoja na Wole Soyinka, Walter Rodney, Che Guevera, Abrahaman Babu.

Njia rahisi kabisa ya kuficha uwoga ni kusema mimi sina chama chote chote cha siasa. Ni kwa sababu ya mitazamo kama hii ndio maana wanaharakati watanzania hawana impact kubwa katika kuleta mabadiliko ya kidemokrasia.

Huwezi kuwa opinion leader mwenye impact kama utajitenga na harakati za kisiasa kwa nchi inayojaribu kujenga demokrasias kama Tanzania. We cannot afford to be indifferent in our context.
 
sixgates

JF-Expert Member
Mar 19, 2011
3,979
2,000
Opinion leaders wapo.

Tunakosa vitu viwili..kwanza tulichokosa ni platform iliyo huru na focused (mfano tbc inarepresent status quo), itv ni consevative na sio wabunifu wana bias, clouds media wanafiki, star tv bado wapo enzi za ujima/enzi za herode kuna saa najiuliza ivi star tv hawaoni kua wapo nyuma ya wakati?.. Jambo la pili tanzania hatuna wanahabari extraordinary km larry king ama aina ya akina richard quest. Waandishi wa habari hawaheshimiki,are just ordinary people, hawjiamini na inatia wasiwasi uwezo wao.

Mfano. Hata raisi aite wahariri pale ikulu hamna mwandishi anaethubutu kumuuliza maswali magumu, utasikia wanauliza mh raisi umejipangaje, vipi maoni yako. Ooh mh raisi tumesikia sikia inaboa sana! Hata ukienda kwenye hizi media wanakupangia uongee nini, mfano kipindi cha mgongano wa hoja itv ukisema viongozi wa tanzania ni wabinafsi,au wadhaifu utaona deo reyunga anakunyanganya mic..ukienda kwa makwaia hajui kuhoji..mfano tulienda kwenye kipindi chake katika kuongea nkawa nimesema.

Jeshi la police nalo ni sehemu ya tatizo la ubakaji wa democrasia nchini,Nkaendelea kusema Said Mwema ameshindwa.....(Hata sijamalizia kusema nlichokua nimenuia akanikatisha). Akadakia weewe umesema Said Mwema ameshindwa si ndio? Hebu tuende kwa ndugu yangu hapa, (akamuuliza nlieenda nae kwenye kipindi "mwenzako kasema saidi mwema hafai na ameshindwa wewe unasemaje"..ukitizama aina ya interview ya makwaia ni ya kichonganishi.

Yapo mengi natizama kipima joto hamna kitu, sehem yenye uhuru ni hapa JF tuu..nadhan mliona interview ya mh Zitto
 
WOWOWO

JF-Expert Member
Aug 3, 2011
590
500
Opinion leadership ya kweli huwezi kuitenga na siasa. Hatuhitaji opinion leaders ambao ni neutral (if this is what you mean by 'impartial), bali tunahitaji wale ambao ni objective. Impartiality and neutrality are very close to indifference!

Kosa lingine ambalo unaelekea kulifanya ni ku-judge 'impartiality' ya mtu kwa kuangalia kama ni mwanachama wa chama cha siasa au la. Kuwa mwanachama haina maana huwezi kuwa objective, na kutokuwa mwanachama wa chama cha siasa hainamaanisha ndio umekuwa impartial or neutral.

Ma-opinion leaders wazito kibao tunaowajua walikuwa wanachama na wakati mwingine viongozi wa vyama vya siasa. Hawa ni pamoja na Wole Soyinka, Walter Rodney, Che Guevera, Abrahaman Babu.

Njia rahisi kabisa ya kuficha uwoga ni kusema mimi sina chama chote chote cha siasa. Ni kwa sababu ya mitazamo kama hii ndio maana wanaharakati watanzania hawana impact kubwa katika kuleta mabadiliko ya kidemokrasia.

Huwezi kuwa opinion leader mwenye impact kama utajitenga na harakati za kisiasa kwa nchi inayojaribu kujenga demokrasias kama Tanzania. We cannot afford to be indifferent in our context.

Kitu ninachokiamini kuhusu Opionion Leaders ni uwezo wa kuset agenda za kitaifa na kukubalika katika makundi mbalimbai ya kijamii kama reference point. Sasa hili sidhani kwa hali tuliyonayo sasa hivi ya siasa za minyukano, zilizokosa uenezezaji wa itikadi, sera na zaidi reflection kwenye national goals (ambazo hatuna) tutalipata kwa wanasiasa.Maana wao ndiyo wamekuwa wauaji wakuu wa Opionion Leaders/Makers.

Jiulize tu leo hii maoni ya akina Dkt. Bana, Dkt. Lweitama hata wewe mwenyewe (Samahani kwa kutaja majina haya) yanakubalika na kupewa nguvu kiasi gani miongoni mwa makundi ya kisiasa tuliyonayo katika jamii na kwa maana hiyo vyama vyenyewe vya kisiasa? Kila wakiibuka itikadi na mielekeo yao inayafanya makundi hayo tuliyonayo ama yapuuze na kubeza huku mengine yakifurahia kutokana na kubebwa.

Majina ya akina Wole Soyinka,Walter Rodney uliyoyayataja ni sawa walikuwa na partial lakini sidhani kama utatilia shaka misimamo yao na hata falsafa walizokuwa wanazisimamia. Kwa watu ambao tunawaamini ni Opinion Leaders hapa kwetu ni wazi wamekosa hayo.Misimamo na falsafa zao haziko wazi kiasi cha kujijengea uhalali katika jamii pana.

Siamini katika 'Siasa huwezi kuitenga na Opinion Leader' naamini Katika ujenzi na uimarishaji wa taaluma na kwamba Siasa isimame kama zilivyo taaluma nyingine. Siamini katika Political suppremacy dhidi ya taaluma nyingine.Hatuwezi kuwa na issue inayohusu Wabunge kuhongwa halafu Wanasiasa haohao ambao ni sehemu ya Wabunge ndiyo wanajijadili.
 
WOWOWO

JF-Expert Member
Aug 3, 2011
590
500
WOWOWO,

Naunga mkono hoja; lakini tatizo ni kwamba kama ulivyojadili, Politics has become supreme to everything, supreme even to rationality and common sense; Ndio maana kila mtu aidha anakimbilia kuwa a PhD hata kwa kuchakachua au anakimbilia uongozi wa kisiasa kwani anajua akifanikisha kati ya haya, atapewa a prominent role na kuwa influential katika jamii au akiwa mmoja ya maswahiba wa kiongozi wa nchi, jamii itawaheshimu;

Tatizo lingine ni kwamba mtu anakuwa muhimu pale tu anapokuwa na madaraka, anayatumiaje na kwa faida ya nani? hilo halipewi nafasi; Na ikitokea kiongozi husika anapoteza madaraka, hoja yake hata kwenye ukurasa wa michezo wa gazeti haitawekwa; Wealth, Prestige, Social Status, and Power ndio vigezo vikuu vya watu kutumika kama opinion leaders, bila ya kujalisha wamefikiaje hayo - on merit? uadlifu? utiifu wa sheria? elimu? uzalendo? mfano wa kuigwa na jamii? haya yote hayajalishi;

I agree with jaribu kumsoma Kitila Mkumbo hapo juu yeye anasema Siasa huwezi kuitenga na Opinion Leader na kwa maana hiyo hoja yako anaikataa.

Sababu ya siasa kutawala kila kitu ni kutokana na ukweli kwamba media zetu zimeamua iwe hivyo.Linapotokea jambo zito la kitaifa na linalohitaji mjadala mpana media hazihangaiki kutafuta suluhu ya kiweledi (Professional consensus) badala yake zimekuwa zikikimbilia kutengeneza political debates ambazo mwisho wa siku ni kupoteza isssue yenyewe iliyoibuka na ndiyo sababu ya kauli za 'Ni upepo tu utapita' zimekuwa very common maana media ni vehicle ya hilo.

Ndiyo maana hapo juu nimesema kuna kila sababu ya media kubadilika na kuwa na professional outlook pale linapoibuka suala zito. Kwa mfano tu, suala la Dowans na hukumu iliyotolewa dhidi ya Tanesco ni la kisheria, tungetegemea Media kuhoji zaidi wataalamu wa Sheriza za kimataifa ambao naamini tunao hapa nchini lakini media zinakimbilia kuchukua kauli za wanasiasa pekee as if issue hiyo ni political matokeo yake issue kama hiyo inabaki ya wanasiasa kubezana na kupashana kwenye majukwaa then inapeperuka.
 
Last edited by a moderator:

Mchambuzi

JF-Expert Member
Aug 24, 2007
4,853
2,000
WOWOWO,

Nimemsoma Kitila Mkumbo; Kuna maeneo nakubaliana nae lakini kuna mengine sikubaliani nae; Pia nahisi kama anajichanganya kidogo:

Kwa upande mmoja anasema kwamba hauwezi kuwa an opinion leader mwenye impact kwenye jamii iwapo utajitenga na harakati za kisiasa; Kwa upande mwingine anasema kwamba, hauwezi kutenga siasa na opinion leadership; Nakubaliana na kauli yake ya kwanza lakini hii ya pili kwa mtazamo wangu sio sahihi; Opinion leadership na Siasa ni vitu viwili vinavyojitegemea; Alichotakiwa kufanya ni kuwa consistent na hoja kwamba – iwapo suala husika linahitaji mchakato wa siasa kuleta mabadiliko, basi ni muhimu kuchanganya opinion leadership na siasa; Vinginevyo sio kila ‘change' inahitaji mchakato wa kisiasa;

Nikija kwenye mifano yake ya Soyinka, Che Guevara, Walter Rodney, na Babu, nadhani anatambua kwamba hawa hawakuwa wanasiasa per se bali walikuwa ni professionals katika maeneo yao husika, lakini kwa vile masuala waliyokuwa wanayasimamia yalihitaji mchakato wa kisiasa, hapo ndio wakaingiza professions zao katika siasa, lakini sio kama wanasiasa, bali wanaharakati, to influence the political process;

Vinginevyo Soyinka was a poet and writer ambae alitumia vyema profession yake to influence change in Nigeria, bila ya kuwa mwanasiasa per se; Che Guevara was a medical student ambae hakuwa na dini zaidi ya Marxism, na alitumia imani yake hiyo to influence the political process - kama mwana harakati, sio mwanasiasa; Walter Rodney was a PhD/an intellectual/lecturer/mtafiti katika masuala ya historia, nae pia alitumia kipaji na elimu yake kama mwanaharakati to influence the political process; Mzee Babu - alikuwa ni mtaalamu wa masuala ya uchumi na fedha, ambae pia kama Che Guevara, yeye pia alikuwa Marxist; Babu ndiye alikuwa na mkono wa chuma katika harakati za kumtoa sultani Zanzibar ingawa historia inaliweka hili sivyo; Kutokana na influence yake kubwa, Karume alimwomba Nyerere amchukue na kumtoa Zanzibar, na hapo ndipo Babu akageuzwa rasmi kuwa mwanasiasa kwa kupewa Uwaziri wa Mambo ya Nje wa JMT; Lakini kwa Babu kama Babu, shughuli yake ilikuwa ameshaimaliza, na harakati zake zikaishia hapo;

Kwahiyo ukitazama kwa makini, wote hawa hawakuhitaji uongozi wa kisiasa per se (with mild exception ya Babu), to influence the political processes to bring about change in their environment; Ni uwezo wao waliojijengea nje ya siasa ndio ulifanikisha waonekane muhimu katika jamii husika, kufanikisha mabadiliko yaliyo hitaji a political process;

Tukirudi kwenye hoja ya msingi, kuna aina fulani za mabadiliko ambazo zinahitaji a political process, na ni hapa ndio nakubaliana na Kitila Mkumbo; Lakini tunasahau kitu kimoja, hatujamchambua opinion leader kwa undani sana; Wowowo umejaribu kufanya hivyo, na mimi naomba nijielekeze kidogo huko;

Opinion leader ni mtu ambae anaheshimika sana miongoni mwa watu, hasa wanaopokea au kutekeleza mawazo/maoni yake; Mtu wa namna hii kwa kawaida huwa na ushawishi mkubwa sana on people's opinions, actions and behaviors; Na mtu anafikia kiwango hiki cha heshima na influence by merit, Cheo cha kisiasa, PhD, Utajiri au Ukaribu na mkuu wa nchi peke yake haitoshi; Kwa bahati mbaya, Media zetu zina tabia ya kuwapa heshima hii watu wenye nafasi za uongozi wa kisiasa, utajiri, PhD hata kama hazijafanyiwa kazi ya kutosha, au ukaribu na utawala husika; Na inapotokea media inampa uzito huu kiongozi wa kisiasa, mara nyingi sio lazima awe na professional approach, na badala yake, akiwa crritical to the government na kutikisa system na nchi ni tiketi tosha; Ndio maana hatuna consistent opinion leaders, akipoteza uongozi, TUPA KULE;

Tunafanya makosa sana kuachia Media ndio ituchagulie opinion leaders; Kwa kawaida, Opinion leaders wana influence kubwa kuliko MEDIA, na hii ni kutokana na ukweli kwamba inatakiwa opinion leaders wawe trustworthy na non – purposive; Hizi ni sifa kuu mbili, ambazo bila hata ya kupoteza muda, nadhani sote tunakubaliana kwamba hakuna media organization yoyote Tanzania inazo; Kutokana na sifa hizi mbili, UMMA hauisi kunadanganywa na kuongozwa kifikra katika kuamini jambo ambalo sio;

Last before least, naomba niseme tu kwamba – ili kuwa an opinion leader, hauhitaji kuwa mwanasiasa; Kinachotakiwa ni uwe educated (ingawa not always), experienced katika fani yako, demonstration ya achievement hasa zilizoleta mabadiliko au kuchangia mabadiliko kupitia utafiti n.k, integrity, credibility na moral authority; Opinion leaders sio watu wa kushughulika na matukio kama kwetu Tanzania, badala yake wanajishughulisha na masuala kimfumo; Ndio maana mara nyingi opinion leaders hutokea kwenye think tanks au institutions of higher learning where knowledge and understanding about Society husika inakuwa produced; Haitakiwi kuokota opinion leaders barabarani kwa sababu tu wana Vyeo au Ukaribu na System/Mkuu wa nchi, au Uwezo wa Fedha; Katika mfumo wetu uchwara Tanzania Kisiasa na Kiuchumi, mtu anaweza kuwa na Phd, madaraka, ukaribu na watawala, uwezo wa fedha, lakini akawa useless kabisa kwa jamii at large; Ndio maana inabidi tuwe waangalifu katika ku – select opinion leaders;

Media huwa inapo wachukua kina Kitila Mkumbo na wengine kutokea taasisi za elimu ya juu ni jambo jema, lakini haitoshi kwani hatujui wahusika hawa wamefanya tafiti gani katika maeneo yao, kwani utafiti unasaidia zaidi uelewa wao wa mambo over and above partisan politics; Lakini huwa siachi kujiuluza, inakuwaje wataalam kutoka REPOA & ESRF (watafiti wa mambo ya uchumi na Maendeleo wanaotumiwa kimataifa) au CEEST ( watafiti wa masuala ya nishati na mazingira wanaotumiwa kimataifa for East, Central and Southern Africa), kwanini hata siku moja hatuwaoni wakisikilizwa mawazo yao?

Mwisho, watanzania wanaendelea kuangushwa sana na intellectuals; Intellectuals are supposed TO GIVE MEANING TO & READ MEANING INTO, WHAT MAY LOOK LIKE THE OBVIOUS TO THE SOCIETY - kuna mambo mengi nchini ambayo Siasa (not logic or rationality) hutumika kuyafanya yawe unquestionable, obvious, acceptable, and intellectuals do nothing about it]; Watanzania wanategemea intellectuals kuwapa meaning to and read meaning into things that are perceived to be ‘Unobjectionable' and routine; Whereas Wanasiasa PRETEND TO THINK FOR THE SOCIETY, INTELLECTUALS HAVE A DUTY TO HELP THE SOCIETY THINK FOR ITSELF!

Given this critical role of intellectuals kwenye jamii, ndio maana sio ajabu kwa viongozi wengi wa chama tawala na serikali yake kukaa mbali na independent and critical thinkers – e.g. mfano Critical and Professional Economists, Lawyers, Journalists, Engineers n.k; Mifano ni mingi - kina Shivji, Ulimwengu, n.k; And more often than not (not always), if you are a professional, na ukajikuta upo upande tofauti na hawa katika siasa za Tanzania, basi wewe unatumika (again, more often than not, not always);
 
Mkuu Mchambuzi nakubaliana na wewe katika hoja ya kuwapa status Opinion Leaders katika jamii na ukweli kwamba si lazima wanatane na siasa au watumie siasa katika kubrain storm na kutoa miongozo ya kimfumo na kihoja katika taifa letu kama anavyoeleza Kitila Mkumbo. Ninachojua Opion Leader akishakuwa partisan anakosa status na credibility katika jamii pana.

Kama ulivyoeleza Opinion Leaders mara nyingi wanakuwa ni wanataaluma, researchers na watu wenye heshima katika jamii ambao kwa kweli wakisimama na kuzungumza kila mtu (kutoka makundi mbalimbali ya kijamii na kisiasa) anawachukulia kama reference. Swali la kujiuliza ni je hawa watu tunao kweli katika taifa letu? Taasisi zetu za elimu ya juu zina hazina kweli ya Opinion Leaders? Hapa ndipo ninapo ona tatizo la msingi katika nchi yetu.

Mijadala mingi ya kitaifa imekosa agenda ya kudumu na mingi imekufa ikiwa bado ya moto sana. Imekuwa ikiishia mikononi mwa wanasiasa ambao ni wazi wana maslahi binafsi nayo. Hata media zetu zimekuwa zikichukulia masuala mazito ya kitaifa katika mkondo huohuo wa kupopulize wanasiasa na hatimaye kuteka agenda na hoja zote za kitaifa.

Sijasema media zitutengenezee Opion Leaders kama ulivyoninukuu ila media zitusaidie kuwa identify na kuwapa status stahili katika jamii kwa kuwapa priority kila kunapoibuka suala zito la kitaifa linalohitaji opinion directives na professional consensus. Hili tumelikosa kutokana na media kukimbilia kwa wanasiasa kila mara na kila wakati.

Ninachoamini tuna wasomi na wanataaluma wengi ambao heshima na hadhi zao zimevuka hata nje ya mipaka yetu lakini hapa nyumbani hawathaminiki na hawapewi nafasi. Nahisi hata tabia ya Serikali kupuuza mawazo mbadala inaweza kuwa pia ni sababu ya kuisambaratisha kada ya Opinion Leaders. Kwa kweli inahitajika sana na kuna kila sababu ya kuanza harakati za kuiimarisha na kuipa nafasi stahiki katika jamii.
 
Last edited by a moderator:

assadsyria3

JF-Expert Member
Apr 9, 2013
6,881
2,000
CHAMA cha demokrasia na maendeleo bila shaka ni chama imara ila kinatatizo moja tu la uongozi. UONGOZI ULIOPO umeshindwa kabisa kusoma alama za nyakati, unapokuwa na viongozi ambao kwao kila wanaetofautiana ni threat hapo uongozi kimsingi unakuwa dhaifu na kuanza kufukuza wale wanaowaona either ni threat au wanawapa changamoto.

Mfano mzuri MH SHIBUDA akihojiwa hot mix mwezi uliopita alikiri wazi kwamba nilizani CHADEMA nitakuwa na uhuru wa mawazo lakini nimekuta yaleyale nilioyakimbia ccm nikitoa mawazo tofauti naitwa msaliti au pandikizi la ccm, zamani ccm waliniita kibaraka wa upinzani au ww si mwenzetu sasa nashangaa hata upinzani nao wanafanya upuuzi uleule wa ccm wa kutotaka changamoto. embu ndugu fatilia mh clinton alipata hofu kubwa baada ya kusikia obama nae anataka kugombea na alifanya kila aina ya ubaya ili obama asichaguliwe lakini mwishowe alikiri kuwa kiongzi sio tu kutamani bali uonekane kweli kwa vitendo,mfano mwingine ni kule sudani kusini ambapo viongozi dhaifu huwakimbia wapinzani wao kwa kuwafukuza na baadae kuleta vurugu kubwa kwenye jamii.

chama makini kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu viongozi wake wangejikita katika kuimarisha chama kwa mikutano makonganmano lakini si kujikita katika kuwamaliza waleta changamoto.

NOTE
KUKIMBIA CHANGAMOTO NI DALILI YA UDHAIFU ,, KICHWA KIKIUMA UNAKUNYWA DAWA SI KUKIKATA KWANI UKIKIKATA HATA MWENYEWE UTAKUFA.
 
nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
1,225
CHAMA cha demokrasia na maendeleo bila shaka ni chama imara ila kinatatizo moja tu la uongozi. UONGOZI ULIOPO umeshindwa kabisa kusoma alama za nyakati, unapokuwa na viongozi ambao kwao kila wanaetofautiana ni threat hapo uongozi kimsingi unakuwa dhaifu na kuanza kufukuza wale wanaowaona either ni threat au wanawapa changamoto. mfano mzuri MH SHIBUDA akihojiwa hot mix mwezi uliopita alikiri wazi kwamba nilizani CHADEMA nitakuwa na uhuru wa mawazo lakini nimekuta yaleyale nilioyakimbia ccm nikitoa mawazo tofauti naitwa msaliti au pandikizi la ccm, zamani ccm waliniita kibaraka wa upinzani au ww si mwenzetu sasa nashangaa hata upinzani nao wanafanya upuuzi uleule wa ccm wa kutotaka changamoto. embu ndugu fatilia mh clinton alipata hofu kubwa baada ya kusikia obama nae anataka kugombea na alifanya kila aina ya ubaya ili obama asichaguliwe lakini mwishowe alikiri kuwa kiongzi sio tu kutamani bali uonekane kweli kwa vitendo,mfano mwingine ni kule sudani kusini ambapo viongozi dhaifu huwakimbia wapinzani wao kwa kuwafukuza na baadae kuleta vurugu kubwa kwenye jamii.
chama makini kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu viongozi wake wangejikita katika kuimarisha chama kwa mikutano makonganmano lakini si kujikita katika kuwamaliza waleta changamoto
NOTE
KUKIMBIA CHANGAMOTO NI DALILI YA UDHAIFU ,, KICHWA KIKIUMA UNAKUNYWA DAWA SI KUKIKATA KWANI UKIKIKATA HATA MWENYEWE UTAKUFA.

Kama UKO FAIR & SQUARE -- Angalia CHAMA CHA MAPINDUZI... UONGOZI wao wa JUU UKOJE???? SIO wa KINAFSI?
Ni Maamuzi ya MTU MMOJA TU --- HUYO MWENYEKITI -- Ni kwanini yeye kaamua Vyeo Vya KAMATI KUU hataki MAWAZIRI wavishike??? Ilikubalika Kidemokrasia Ndani ya MKUTANO MKUU wa CCM?

Ni Wapi ILISHINIKIZA ya kuwa MWENYEKITI wa CHAMA CHA MAPINDUZI ndie mwenye SAUTI YA MWISHO kwenye kuchagua WAJUMBE watakaopata kura NEC au MKUTANO MKUU???

HIYO NI DEMOKRASIA???

Na ni kwanini Basi Mwenyekiti wa CHAMA ndie lazima AGOMBEE URAIS? HIYO SIO MIZENGWE ya KIKOMINISTI?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom