Tanzania na Barrick zasaini mkataba wa makubaliano. Tanzania kuwa na hisa asilimia 16 na kupata faida ya asilimia 50

Nimeuliza swali hilo hilo sijapata jibu. Kwa taratibu za kawaida za gawanyo la faida haingiii akilini kumiliki hisa 16% na gawio 50%.
Tuwasubiri tu wachumi wanaweza kuja kutufafanulia hayo mahesabu yanakuwaje.
 
Mna mtatizo ya kifikra na mnatawaliwa na utumwa wa mawazo. Poleni sana kwa kuonesha utoto kihoja.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sidhani kama kuna utoto wowote kwenye waliyoyasema.
Kwa mfano, unataka kusema ni uwongo Barrick kupunguza wafanyakazi 110. Kuna faida/mafanikio gani watu kupoteza ajira? Kumbuka hii ni round ya tatu or so ya redundancy.
Utumwa wa mawazo wa hawa jamaa uko wapi? Mbona wanazungumza mambo halisi.
 
Unachoweza kufanya ni kuwapa maarifa wenzako hao ili nao watoke
Naamini kuwa ni rahisi kumsadia mtu ambaye hajaanguka ili asianguke mfano msaada wa ada; ushauri wa vitu kusoma LAKINI ni ngumu sana kumsadia aliyeanguka anyanyuke na kusonga tena; utatumia nguvu kubwa sana utaishia kujutia.

Ndugu yangu kwa nafasi yako pambana na vijana wawe kwenye msitari kuliko kutumia nguvu kujaribu kumsaidia mtu mzima aliyekoroga maisha yake kwa hutoweza kamwe kumnyanyua tena.
 
*Rais Dokta John Pombe Magufuli*

#Ndugu Watanzania,Kukaa meza ya Mazungumzo na Kigogo hiki Barrick,chenye msuli mkubwa wa uwezo na Ushawishi,haikua kazi rahisi.

#Nampongeza sana Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Profesa Paramagamba Kabudi,aliyeongoza timu ya Wataalamu Wazalendo kufanikisha jambo hili.

#Mazungumzo hayo yalichukua miaka mitatu yakianzia mwaka 2017 mpaka leo tunapotia saini makubaliano baina yetu na Barrick.

#Mkasimamie vyema makubaliano haya na kwenu Wizara ya Madini,Nawaomba kuhakikisha Watanzania watakaopewa dhamana kwenye Kampuni ya pamoja baina ya Tanzania na Barrick ya Twiga Mineral Corporation,kuhakikisha kuwa Wanaangalia maslahi ya nchi na si yao binafsi.

#Naweza kusema kuwa Majadiliano haya yalikua ni vita ya Tembo na Sungura,lakini kwa hatua ya leo ni sawa na kusema vita imeisha kwakua lengo lilikua pande zote kufaidika na wamekubali.

*Profesa Kabudi*
Kubwa katika Mazungumzo yetu tulikubaliana kuunda kampuni ya Twiga Mining Corporation,ambayo Barrick atakua ni mbia ndani ya kampuni hiyo.

#Watanzania muelewe kuwa Serikali itashiriki maamuzi ya kila kitu katika kampuni hiyo ya Twiga Mineral Corporation,ambayo Serikali itakua na hisa za asilimia 16 na siyo Twiga tu bali asilimia 16 kwa migodi yote.

#Nyie Barrick Ondoeni Mtazamo kua kuna Barrick Tanzania bali ni mbia wa Twiga Mineral Corporation iliyoundwa Septemba 10,2019.

*Mark Bristow*
*Rais na Mtendaji Mkuu Barric*

#Mheahimiwa Rais,hii ni siku ya kipekee barani Afrika,tuna furaha kuanza upya ushirika wetu,tunakubali kuwa awali kulikua kuna tatizo mahaka,lakini sasa tuko tayari kuwa na mwanzo mpya wenye faida kwa pande zote.

#Kuna baadhi ya Watanzania;walivumisha kuwa eti Tanzania,inataka kuwakera wawekezaji,siyo kweli na niko hapa kuwahakikishia kuwa huo ni uzushi na kwamba inachokifanya Tanzania,ni kitu chema kwa maslahi ya Watanzania.
 
..usd 191 billion tunazowadai ziko wapi?

..na kwanini tupewe asilimia 16 tu na siyo 50 au zaidi wakati madini ni yetu?

..na kwanini wameanza kupunguza wafanyakazi?

Kweli uliamini tunawadai US$ 191 Billion?..kupewa asilimia 50 bila kuwekeza chochote ni sawa hiyo? Tuache kuwa walalamishi kama wale waisrael waliofia jangwani sababu ya kushindwa kusema asante.
Tulioharibu haya mambo ni sisi wenyewe. Kurekebisha sio kazi rahisi kama kuandika haya maneno ya kejeli kwenye key board.
Shida hakuna kwa kushika. Wanasiasa wote ndio wale wale. Kam tunabisha tuwape uongozi. Afrika mambo bado sana
 
..usd 191 billion hatukuitoa vichwani vyetu. Viongozi, tena wanaojiapiza kuwa ni wacha mungu, ndiyo waliotoa madai hayo. Sasa sisi wananchi kwanini tusiwaamini viongozi wetu?

..pia umesikia kuwa MAKINIKIA nayo yataanza kusafirishwa? Unakumbuka mzee alidai dhahabu iliyopo kwenye makontena inatosha kujaza lori 7 za tipper, na landrover 1? Je, makinikia yatauzwa kwa bei ya KIZALENDO au yatauzwa kwa bei ya MABEBERU?

..Walioharibu ni serikali na wabunge wa CCM. Wapinzani na wanaharakati waliwaonya mapema tangu miaka ya 90 wakati mkataba wa kwanza wa migodi mikubwa unasainiwa. Tundu Lissu na Rugemeleza Nshala walifunguliwa kesi kwa sababu tu walikuwa wanaieleza jamii mapungufu ya sheria na mikataba ya madini.
 
Can you make a demarcation line between the politicians we have in this country? Mfano mdogo tu...TL alipigana sana kuhusu madini na wizi unaoendelea kwenye madini. Because of his own personal test na wamu hii, akaamua kuungana na wale aliowapiga vita kwa nguvu zote. Unajua kwamba usipoaminika kwenye suala dogo hata makubwa hutaaminika? Wanasiasa wetu wote ndio wale wale. wanaumwa njaa. wanataka kula.
Kuhusu bil 191, aliyetoa hizo figure ni mwendawazimu. Ameiaibisha fani yake.
Na kuhusu kusafirisha makinikia, kama sisi ni sehemu ya mchakato wa kusafirisha naamini tutajilaumu wenyewe, mambo yakiharibika.
Nisichoelewa mimi ni kwanini tunajivua wajibu wote na kufikiria kulalamika na kulaumu ndio dawa ya matatizo. Huoni kwamba kwa kufanya hivyo tunaonyesha ni jinsi gani tuna uwezo mdogo wa kufanya mambo? halafu nani amesema short term solutions ambazo hazina tija zitalisaidia taifa letu? Kweli tuna safari ndefu sana.
JPM ameonyesha njia, kama JKN alivyoonyesha kwa kuunda Taifa la Tanzania akishirikiana na wengine. Lakini hata JKN hakumaliza mambo yote. Tunaopokea vijita tujiulize tumefanya nini? Au tunaendekeza njaa tu?
 
Back
Top Bottom