Tanzania na Barrick zasaini mkataba wa makubaliano. Tanzania kuwa na hisa asilimia 16 na kupata faida ya asilimia 50

Ni kuhusu zile trilion 495++
Tungekomaa watulipe pesa zetu za fine (bilioni za kimarekani 190,yaan kwa pesa yetu ni bilioni 190 tuzipange pange mpaka zifike mara elfu mbili na mia tatu na saba (2307) hii pesa ingetuwezesha kujenga twiga ya kwetu wenyewe,kuanzia mitambo hadi makontena ya kusafirishia makinikia kwenda kwenye smelter yetu wenyewe,hao barick wangebakia kuwa wapenzi watazamaji tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unamshauri afanye biashara gani na ni fursa ipi unamshauri wakati biashara ndo hizo zinadorora fuatwafuatwa kibao na makodi kabakaba.Acha kumshauri vibaya ili aunguze mafao yake familia inyanyasike.
Positive attitude towards any challenge in life usually produce good results.
 
Ebu tulia kwanza naomba wajuvi wa masuala haya wanifafanulie sijaelewa kitu, kwamba sisi tuna 16% kwenye kampuni hiyo halafu faida ni 50% kwa 50%. Inakuwaje kwamba mtaji wetu au sijui niseme hisa kwenye kampuni ni 16% sasa sisi faida ya kugawana 50 kwa 50 inakuwaje?
 
Hivi hii biashara inakuaje? Unamiliki 16% ya hisa lakini faida mnagawana 50% kwa 50% na yule mwenye hisa 84%.

Mimi mbona sielewi hii biashara? Kama yupo aliyeelewa haya makubaliano naomba anifafanulie kuhusu huu mgawanyo wa faida
 
Binafsi Sina uelewa wa hili ila ninachoamini hao wazungu siyo maboga,they know why wakasign.
 
Mawazo ya mtu mweusi haya! Sishangai. Just ask yourself, mzungu angeuliza swali ulilouliza? Ndio maana marekani na kuwa taifa lenye watu zaidi ya mil 300, unemployment ni chini ya 4%, sababu watu hawaulizi maswali kama yako!!
Kinachoangaliwa ni issue ya unemployment? au maendeleo ya nchi miaka 100 mbele kpitia hao watu wako unaojaribu kuwatetea
 
Ebu tulia kwanza naomba wajuvi wa masuala haya wanifafanulie sijaelewa kitu, kwamba sisi tuna 16% kwenye kampuni hiyo halafu faida ni 50% kwa 50%. Inakuwaje kwamba mtaji wetu au sijui niseme hisa kwenye kampuni ni 16% sasa sisi faida ya kugawana 50 kwa 50 inakuwaje?
Nadhani wakujibu hili ni wale wanaoshangilia hiyo 50% kwa 50%. Wameelewa nini? Ni faida ipi? kwa vipi?
 
Kinachoangaliwa ni issue ya unemployment? au maendeleo ya nchi miaka 100 mbele kpitia hao watu wako unaojaribu kuwatetea
Hivi unajielewa wewe ? Ulisoma shule ya wapi? Kuna maendeleo bila watu kuwa na kazi? Uchumi gani huo, maendeleo gani hayo unemployment iwe 80%?
 
Hivi unajielewa wewe ? Ulisoma shule ya wapi? Kuna maendeleo bila watu kuwa na kazi? Uchumi gani huo, maendeleo gani hayo unemployment iwe 80%?
Kiongoz gan katika nchi yako kawahi kutengeneza ajira au mnajitengenezea pressure kwa ajira chache zitolewazo na hao wawekezaji walokua wapo kwa kujari masirahi yao zaid ....nchi kama marekan ambazo ndo ma role madel wako wanatengenezaje ajira kama si kwa kukatisha uhai wa watu ktk nchi maskin kpitia izo pandemic deseases....tujarib kuheshim processes maake hata hayo magonjwa yatengenezwayo watu wamekaa kwa mda na kifo chako ndo matokeo chanya ktk kazi zao
 
Mmmh, hizo conspiracy theories!!
 
Haiwezekani kwenye hisa ndogo kupata nusu ya faida na kwenye hisa kubwa. Watanzania tunadanganywa kama zama. CCM no ile ile.

Mikataba tuliambiwa itakuwa inajadiliwa Bungeni, nakupitishwa au kukataliwa. Leo, bado mikataba ina pitishwa Ikulu bila kujadiliwa na bunge wala nini? Huu ujanja ujanja hautufai.

Walisema tutalipwa milioni 300 za dola kwa mkupuo, Leo wanalipa kwa awamu awamu. Walisema Barrick wawe wanatumia Bank za ndani, imeshindikana wametudanganya, bado Barrick wanatumia Benki za nje. Kuna nsitofahamu nyingi karika mikataba umpya baina ya serekali na Barrick ambao serekali ina piga chenga kuuweka wazi kwa watanzania wenye Mali.

Tunadanganywa sana nchini hapa na serekali ya CCM, walaghai sana, wanaongea na sura ya huruma, kumbe hawana huruma kabisa na wanachi. Wanatumia na vibwagizo vya serekali ya wanyonge, watu masiki, sijui nini? Kumbe wananchi tunapigwa juu kwa juu, na viingozi wandamizi was CCM. Chakushangaza, hata wasomi wetu, wanaingizwa kwenye huu mtego na wanakua ma bubu. Angalia Leo Profesa Kabudi nguli wa sheria anavyo endeshwa na CCM kuziba uovu wao. Daah! Tuwapumzishe hawa.
 
Back
Top Bottom