Tanzania na Barrick zasaini mkataba wa makubaliano. Tanzania kuwa na hisa asilimia 16 na kupata faida ya asilimia 50

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,438
3,333
Rais Magufuli atashuhudia utiaji saini makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya madini ya Barrick. Tukio hili litafanyika leo tarehe 24 Januari, 2020 Ikulu Jijini Dar es Salaam kuanzia saa 4:30 asubuhi hii.

Rais Magufuli:
"Rais Magufuli: Nawashukuru sana Barrick. Watanzania waliokuwa kwenye mazungumzo ni Wazalendo sana - Fikiria kutoka 'share' ya 0 hadi ya 16%, lakini pia faida itakayopatikana ni 50 kwa 50 ni ushindi mkubwa kwa pande zote mbili"

"Napenda kuwashukuru ndugu zetu wa Barrick na Watanzania wote - Mengi yamezungumzwa kwa hisia kali. Kabudi hakueleza yote, misukosuko aliyokuwa anapata - Nilikuwa nampigia simu saa 7 usiku akipokea ni matusi. Ananizidi Umri lakini alikuwa mvumilivu"

Rais Magufuli: Nawashukuru Viongozi wa Dini mliopo hapa, mmekuwa mkiendelea kuliombea Taifa - Wakati madini yakisombwa kwa miaka mingi na Watanzania tukaambiwa tuamini kuwa ni mchanga na wengi tukaamini - Ila kujuliza ni kwanini wasafirishe? Kwanini haukuwa wa Bahari?

Mark Bristow (Barrick):
"Ukiwa Afrika lazima uipende Tanzania. Tanzania inawakilisha kila ambacho sisi katika Afrika tunakipenda - Tunafurahi kurejea. Leo tumefikia sehemu ambapo safari ya maisha haiwezi kusimama"

"Leo tumeanza Ushirikiano mpya. Kwenye Ushirikano kuna njia moja ya kuitafsiri ambayo ni asilimia 50 kwa 50 - Twiga inawakilisha Muundo ambapo Serikali ya Tanzania na Watanzania wote watakuwa na maamuzi ya kinachofanyika ndani"

"Tunapotoka kwetu tunakuwa na wajibu mkubwa wa kuvuna Rasilimali za Taifa na si kwa faida yetu tu bali kwa wadau wote katika Nchi husika - Wadau sio tu wanaomiliki hisa ila ni watu wote katika Nchi husika hivyo ni lazima kulipa kodi ili kurudisha fedha"

"Katika Migodi yetu kuna Jamii zinazozunguka migodi hiyo ambazo lazima zishiriki katika shughuli za Kiuchumi za Migodi - Kulikuwa na tetesi na ukosaji mwingi ktk safari hii ya kufikia mafanikio ambayo Kabudi ameeleza - Nadhani hii ni Siku ya Kihistoria"

Wengi walikosoa uamuzi ya kuwa unafukuza wawekezaji lakini safari uliyoanzisha imeonesha kuwa lazima tuende kwenye shughuli yenye manufaa kwa wote - Afrika tunalalamika sana kuwa tunapata kidogo na kutoa zaidi ila ikiwa ni 50% basi tutakuwa tunapata pamoja

Mh. Palamagamba Kabudi, Waziri wa Mambo ya Nje:
"Tume-renegotiate mikataba iliyokuwepo ili kupata 'terms' nzuri - Wawekezaji wote wa madini watapata Leseni zinazofaa kwa maamuzi ya Rais na Leseni hazitatolewa na Waziri wa Madini bali Tume ya Madini kwa maelekezo ya Baraza la Mawaziri"

"Tumejitahidi kuboresha Mikataba hii. Rais na sisi Wasaidizi wake tuhukumiwe kwa Leseni mpya tutakayotoa. Ila kwa haya tumesafisha nyumba - Nyumba ya sasa haina takataka. Uvundo tumeusafisha. Wapo waliosema huu ni mchanga tu ila tunajua si mchanga tu"

"Tarehe 20 Oktoba 2019 tulikubaliana kuunda Kampuni itakayoitwa ‘Twiga Minerals Cooperation’ - Tuna 16% kwenye Kampuni hiyo na kila Mgodi tuna 16% na wamekubali. Katika kujipanga kwa Kipindi cha Mpito, wameleta Waafrika wenzetu kuendesha Kampuni"

"Ningependa Watanzaia muelewe, tuna Barrick kama Mbia ndani ya Kampuni ya Twiga - Na Barrick pia muelewe, hakuna Barrick peke yake, kuna Barrick na Serikali ya Tanzania ndani ya Twiga. Na Twiga ndio Kampuni yetu ya pamoja"

"Katika kujadili Mikataba 9 itakayosainiwa leo, hicho kipindi kilikuwa kigumu. Hawakuwa hawa, walikuwa wenzao hawapo hapa - Sipendi kuwataja majina ila hawakutaka Mikataba hii isainiwe na tufanikiwe. Kila tulipokutana na kukubaliana kesho yake walibadilika"

"Ilifika mahali Rais nilitaka kuingiwa na dhambi ya kukata tamaa na vitimbi hivyo viliishia kwa wao wenyewe kufukuzana kazi - Leo nataka kumshukuru Luteni Kanali Mstaafu Richard William ambaye aliwashinda wenzake walioamua Kuhujumu Uchumi"

NILIANDIKA BARUA YA KUJIUZULU:
"Tulipofika kukata tamaa, Rais nilikuwa nimendika barua ya kujiuzulu kuja kwako. Kwamba kazi uliyonipa imenishinda - Aibu hii na fedheha hii nitaibeba. Barua hiyo sikuileta maana Casmir Simba Kyuke alininyang'anya na kuichana"

"Nilisema sijawahi kutumwa kazi na Mkuu wangu wa Nchi nikashindwa, ila sasa hawa watu hawataki - Rais unaniuliza mnakwendaje, mbona nasikia hamuendelei, namjibu tunaendelea huku najua hatuendelei. Ndipo nilipowapigia Maaskofu wangu wa Anglikana wawili"


 
21 Reactions
Reply
Back
Top Bottom