Naona tumekuwa na unyonge usiokuwa na sababu, kwa kusema Wakenya kuiharibia Tanzania sio sahihi.
ukweli uliosimama hiyo barabara kujengwa katika mbuga ya hifadhi ya serengeti itahathiri kiasi kikubwa
( Ecology ) ikolojia ya wanyama wakati wa kuhama. Serikali ya Tanzania ilifikiria kwa ufupi lakini matatizo
yake ni marefu sana. Wakati wa kiangazi maji ya mito inapokauka na majani kukauka, kimazingira ya hao
wanyama ni lazima kuhamia kwenye mbuga za masai mara kufuata maji pamoja na chakula chao yaani
majani, na mpaka wakati mvua zinapoanza kunyesha serengeti na mito kujaa maji na majani kuchipua
huo ndio unakuwa wakati wa wanyama kurudi serengeti. Na kwa tabia hiyo ya wanyama kwenda Kenya
na kurudi Tanzania kusema kweli haiwezi kuzuilika, hapo Serikali ya Tanzania ni mbinu tu waliyotumia
ya kutaka kuwazuia wanyama wasiwe wanahamia Kenya, na mbinu hiyo ni sawa na kupanga mauaji ya
wanyama, kwa sababu watakuwa hawana maji ya kunywa wala majani ya kula. Na vile vile watakaojaribu
kuvuka barabara watagongwa na magari, kama unavjojua madereva wetu wa bongo awamjali binadamu
je kwa wanyama itakuwaje. Mimi siono kama Serikali ya Kenya ina matatizo bali wamesimamia ukweli ulivyo.
Kipofu hawezi ona labda utokee muujiza, hivi unajua kwamba wananchi wa wilaya ya ngorongoro haeana barabara ya uhalika ya kuwafikisha mkoani kwao? Kipi ni muhimu zaidi, wananchi wa ngorongoro au wanyama wanaobebwa kila wiki wakiwa hai pale loliondo gate na wale waarabu waliouziwa kipande cha mbuga na mwinyi enzi zile. Napata tabu kuamini kwamba una mapenzi ya kweli na watanzania wenzako waishio loliondo, barabara yawezajengwa kwa kuzingatia environmental compliance na bado ikolojia na mazingira yakabaki safi. Mfano ni barabara ya makuyuni- ngorongoro ambayo inapitia kwenye hifadhi ya ziwa manyara barabara hii iko usawa wa ardhi kuruhusu wanyama kupina na pia kuna mikondo inayokatiza barabara na vivuko vya wanyama. Hapajawa na kesi mbaya za kugongwa wanyama zaidi ya accidents kama inavyotokea kwa binadamu. Pia tuna barabara inayopita kwenye hifadhi ya mikumi ambayo sio environment compliant wala hakujawa na shia kubwa ya kuuwa wanyama na kuharibu ikolojia. Sheria zipo kinachotakiwa ni usimamizi eg kusimamia speed limit nk. Barabara ya vumbi toka muugumu kupitia hifadhi ya serengeti na ngorongoro inaongoza kwa uchafuzi wa mazingira kwani vumbi inayotoka wakati mwingine hata mbele huoni miti na majani hukaushwa na vumbi. Sioni point ya kukataa lami na kuwatesa wananchi wa loliondo kwa kigezo cha wanyama na ikolijia wakati waarabu wamejenga uwanja wa ndege na wanaingiza ndege ya mizigo kupakia wanyama hai wakaanzishe zoo kwao. Ikumbukwe pia wanazuia ujenzi huo pamoja na kiwanda cha kuprocess magadi pale ziwa natron kwa kigezo cha framingo. To hell framingo & ecosystem for development of loliondo community. Natamani kupata uanachama wa al-shabab