mkuu sijui kama umeweza soma posts nyingine humu ndani na kutafakari. Tanzania siyo sehemu ya ardhi ambayo iko nje ya dunia hii,lazima tushirikiane na majirani zetu na dunia nzima,tukitanguliza maslahi yetu ya sasa na vizazi vijavyo. Ndiyo maana nikauliza hivi ni kweli hiyo barabara ilikua ijengwe kwa maslahi yetu ama kwa maslahi ya kibiashara ya baadhi ya watawala wetu? Tafakari kabla ya kupost!Sijui nani katuloga watanzania manina!!!. Hata hili nalo. Hivi ni kitu gani kinatubakiza EAC mpaka sasa. Nchi kubwa zaidi ya kuziunganisha zote Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi hazifikii Tanzania. Mimi kwa kweli uchaguzi ujao chama chochote kitakachoahidi kujitoa EAC mimi nitakipigia kura. Hata kama kitashindwa nitajua nilipiga kura ya maana. Viongozi amkeni vizazi vijavyao vitayachapa viboko makaburi yenu kwa hasira haki ya nani
Pamoja na kwamba binafsi siungi mkono ujenzi wa hiyo barabara napenda kusema na kusisitiza kuwa hili ni swala la sisi wa Tanzania kujadili na kufikia muafaka. Wakenya wanahusika vipi na barabra tunayojenga sisi ndani ya nchi yetu? Basi na NGO ya Tanzania ifungue kesi mahakama ya Afrika Mashariki kupinga ujenzi wa Lamu Port. Nilikwisha andika humu jamvini kuwa hawa Wa Kenya si rafiki zetu na hatuna uhusiano mzuri nao. Tujenge uhusiano na nchi za kusini kwetu ambao tunaheshimiana sana.
Nawakilisha.
SERIKALI ya Tanzania imebwagwa katika rufaa yake iliyokata dhidi ya uamuzi wa mahakama ya Afrika Mashariki ya kuzuia ujenzi wa barabara ya Musoma-Serengeti-Arusha baada ya kitengo cha Rufaa cha Mahakama hiyo jana kuamua kuwa uamuzi huo ulikuwa sahihi.Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali ya Tanzania ilipinga hati hiyo kwa madai kuwa mahakama haikuwa na mamlaka ya kufanya hivyo kisheria.Kupitia kwa Wakili Mkuu wa Serikali, Gabriel Malata serikali ya Tanzania ilidai mbele ya jopo la majaji watatu wa mahakama hiyo wakiongozwa na Rais wao, Jaji Harold Nsekela, Jaji James OgoolaMaombi hayo ya Tanzania yalipingwa na wakili Saitabao Kanchory Mbalelo anayewakilisha walalamikaji aliyedai mahakama hiyo ina uwezo na mamlaka ya kutoa hati ya kuzuia utekelezaji wa mradi huo na kuomba mahakama kutupilia mbali rufaa hiyo.
kama wanaingilia mambo yetu na wanatushinda ni kwa sababu ya upumbavu wetu'kwani sisi hatuna wataalam wa sheria wa kupambana nao?nchi hii wote tuko sawa msomi na asiye msomi
Mwisho tutaambiwa na hiyo barabara inayopita mikumi tuichimbue haraka.
Acha tuwasaidieni kufikiri nyie viumbe wa kusini mwa nchi yetu.
You have never been good at what you do.
Mulichimba madini na sasa munakaribia kuyamaliza bila ya nchi kufaidika, muekata magogo na uya export hamjali vizazi vijavyo, hamzingatii wala kujishughulisha na chochote tufanyacho nchini kwetu, mtajuaje hatari inayowajia.
Kila mtu kwenu ni politician hakuna professionals wa other field munapenda without reasoning kwa sababu ya kukata tamaa.
Wacha tuwasaidie kufikiri, but we know kile tunapata in return, tutaingia popote kulinda maslah ya wakenya, ninyi endeleeni kupiga politiki.
iyo barabara cyo wakenya wenyewe hawakuikubali hata wana mazingira wa tz na dunia kwa ujumla pia hawakuitaka.
Nawambia hivi lowassa akishika hii nchi michezo ya kidali poo tunayochezewa na wakenya itakuwa mwisho . Hata wao wanajua kabisa .
shida watz hatupendi challenges hata hizo nchi za kusini zikituchallenge tutawachukia tuseme ni maadui zetu baada ya hapo naona tutaenda west africa
Unatwambia mazingira wakati tunajenga ndani ya mto Msimbazi? Njoo Mwanza mjini uone kilimo cha mboga pembeni mwa ziwa Victoria kilivyoshamili,watu wananyunyizia dawa za kuulia wadudu,mbolea za viwandani, watu wa mazingira wapo wanaangalia tu kwanini tusisaidiwe na wakenya.