Tanzania: Land rights vs biofuel development – in pictures

Tanzania: Land rights vs biofuel development – in pictures

Panaponishinda kuelewa nipale nisikiapo Mwekezaji kanyang'anya Ardhi, tena mgeni kutoka nje ya Nchi. Yaani mmelala kijijini kwenu Asusubuhi mnaamka mnakuta Wachina, Wahindi au Wazungu ati wamevamia Maelfu ya hekta za Ardhi wanafanya shuhuli zao, yani ndio tuamini hivyo? Au kuna namna zinazotumika kuwapagaisha Wananchi/Wanavijiji, na wao huwa wako wapi mpaka yote hayo yanatokea?
 
jasusi,
Yapo mambo ambayo ya msingi naweza kukubaliana na wewe kwamba baadhi ya watendaji serikalini si waaminifu na wanapindisha sheria za uwekezaji kwa manufaa yao binafsi; tukirudi kwenye neno pembezoni nina uhakika unafahamu vyema mh. Raisi hakuumaanisha watu wadhulimiwe ardhi yao alichomaanisha watu wa maeneo yanazunguka mashamba ya wawekezaji watafaidika na ajira; hapa naona unaongelea zaidi ushabiki wa kisiasa na si kutafuta suluhisho wa mgogoro husika.

Chama
Gongo la mboto DSM

Chama,
Ni vema unakubali, kuna tatizo katika hili zoezi. Ni kweli kuna baadhi ya watendaji si waamifu na wanapindisha sheria za uwekezaji kwa manufaa yao binafsi. Hawa watu wanamuwakisha Raisi, kama wanafanya Dhulma, na yeye ataulizwa kuhusu uchungaji wake. Waliofanya vitendo hivi hapa Pwani, Rukwa na Kigoma na kwingineko, wapo na wajaulizwa ili kuwaambia watanzania inakuaje binadamu wenzetu kuwekwa katika hali hii. Chama, hudhani hii ni sababu nzuri ya kuirudia mikataba hii, na kuhakisha wawakilishi wa taifa watatilia maanani watu wenye ardhi na manufaa yao. Raisi anaweza akabatilisha mikataba hii kwa sababu hiyo, au akasimamisha mchakato huo, mpaka wapewe haki zao. Natural resources zinakua plundered. Na pia ni muhimu kufaham wanaemshauri mkulu katika haya mambo, unajua wakati mwingine watu wanaokuzunguka ni muhimu kama wewe.
Kwa upande mwingine, nadhani Raisi inawezekana alimaanisha "Marginalized" which is probably what they are. Hili neno ni miongoni mwa maneno mapya ambayo tafsiri yake kwa Kiswahili inaweza maanisha kitu kingine, (Namuelewa Jasusi vizuri tu,) It is another way of saying poor, lakini kwa kitamaduni masikini ni wale wasioweza kubadili hali Fulani katika maisha yao haiwezekani, kama vile walemavu.
 
Na hiyo nishati haitatusaidia kitu. Mzungu atavuna na kuuza kwao. Na faida anaweka kwenye akaunti yake kwao.
Sisi tunaambulia patupu.

Vipi kuna makubaliono gani kuhusu Chakula? Chakula kisipotosha nchini, wataendele kulisha magari wakati watu wanashida ya chakula: Nafikiri wananyonge wajulishwe ili kuondoa ikhtilafu mbele ya safari.
 
Panaponishinda kuelewa nipale nisikiapo Mwekezaji kanyang'anya Ardhi, tena mgeni kutoka nje ya Nchi. Yaani mmelala kijijini kwenu Asusubuhi mnaamka mnakuta Wachina, Wahindi au Wazungu ati wamevamia Maelfu ya hekta za Ardhi wanafanya shuhuli zao, yani ndio tuamini hivyo? Au kuna namna zinazotumika kuwapagaisha Wananchi/Wanavijiji, na wao huwa wako wapi mpaka yote hayo yanatokea?

Kasukali, Inawezekana wamedanganywa kua Ardhi ni ya Serikali na kua serikali inafanya itakavyo.
kama unavokumbuka katika historia, Wakoloni walipokuja waliingia mikataba ya kilighai na wenyeji wachache. Sasa kuna kampuni za kushauri Wawekezaji (Consultant Company) ambao kazi yake ni kua kiungo kati ya wawakilishi wa serikali na Wafanya biashara wa nje. Hawa inawezekana mikono yao pia michafu. Ndio maana mliambiwa Ubepari ni Unyama, ni kwa sababu kama hizi, za kujali pesa tu, hata kwa dhuluma kinyume cha sheria.

Kujibu swali lako Je hawa Wanakijiji hupagaishwa au wao hua wako wapi mpaka haya yanatokea? kulingana na nngu007 Wazee wa kijiji huingia maelewano na serikali. Kama vilevile wakati wa ukoloni, mkoloni anakuja anaongea na chifu. Hii sio halali.
 
Vipi kuna makubaliono gani kuhusu Chakula? Chakula kisipotosha nchini, wataendele kulisha magari wakati watu wanashida ya chakula: Nafikiri wananyonge wajulishwe ili kuondoa ikhtilafu mbele ya safari.
Nadhani hawa priority yao ni kuzalisha nishati. Hatujaweka mapendekezo yeyote ya kuwataka wazalishe chakula. Na soko lao ni la nje ya nchi.
 
Back
Top Bottom