Tanzania Kwa Yenyewe ni Moja ya Maajabu Saba ya Ulimwengu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania Kwa Yenyewe ni Moja ya Maajabu Saba ya Ulimwengu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by majany, Oct 3, 2012.

 1. majany

  majany JF-Expert Member

  #1
  Oct 3, 2012
  Joined: Sep 30, 2008
  Messages: 1,199
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  [FONT=&quot]jamani badala ya Watanzania kuhamasishwa wapigie kura vivutio vya utalii viingizwe kwenye maajabu saba ya dunia ni afadhali tuipigie Tanzania kura iingie kwenye maajabu hayo kwani hatutatoka haba maana Tanzania yenyewe ni moja ya maajabu kutokana na yanayoendelea na yatakayoendelea kama unabisha fuatilia hapa chini
  1. Ni wapi isipokuwa Tanzania utamsikia waziri wa Nishati na madini akijiapiza kwa miungu yake kwamba hakuna mgawo wa umeme wakati kila siku tunaona umeme ukikatika sehemu tofauti kwa muda mrefu za ukiuliza unaambiwa wanarekebisha miundo mbinu wakati kwa akili ya kitoto tu huo ni mgawo wa umeme, kwetu mgawo ni mgawo tu iwe wameshindwa kuilipa DOWANS au iwe ukarabati wa miundombinu, iwe hitlafu ya mitambo au kushuka kwa kina cha maji.

  2. Ni Tanzania pekee ambako utakuta wanafunzi hawana madawati wanakaa chini na wengine kwenye vyumba visivyostahili kuitwa vyumba kwa ubovu na uchakavu pia hata umeme hakuna lakini ukasikia ahadi ya kila mwanafunzi kupewa Komputa(Laptop)

  3. Haijawahi kusikika popote ulimwenguni kwamba kuna mhitimu aliyefaulu mtihani wake tena wa maandishi huku yeye hajui kusoma wala kuandika isipokuwa Tanzania.

  4. Ni wapi duniani Kiongozi wa chama tawala atawaambia wananchi wake hajui chanzo cha umasikini wao kisha akarudi katika uchaguzi na kauli mbiu ya maisha bora kwa kila mtu halafu akapeta katika huo uchaguzi, hii ipo Tanzania pekee ambapo watu wanakichagua chama hicho kwa miaka dahari licha ya ukweli chama hicho hakijajua sababu ya umasikini wao.

  5. Hakuna sehemu duniani ambako watu kusahau ni sehemu ya maisha yao ni Tanzania pekee yanaweza yakatokea kama yaliyomkuta Dr. Ulimboka watu wakajidai kupata kiwewe halafu ndani ya mwezi mmoja watu wamesahau kabisa wengine kudai kujiuliza Dr. Ulimboka ni nai?

  6. Hii ipo Tanzania tu anaweza kuibuka babu akawaambia nimezungumza na Mungu na amempa dawa na watu wakapanga foleni kama wasio na akili nzuri kwenda kupata muujiza wa mungu unaouzwa kwa shilingi 500 mungu wa wapi anafanya biashara zama hizi.

  7. Ni wapi duniani unakuta barabara iliyotengenezwa kwa minajiri ya njia mbili yaani kwenda na kurudi lakini serikali inaamua zigeuzwe ziwe njia tatu yaani mbili za kwenda na moja ya kurudi bila upanuzi wa barabara hiyo kama unabisha nenda Dar ukatembelee barabara ya Ali H.Mwinyi ujionee siasa zinavyoweza kufanya kazi ya kitaalamu hakuna anayeshangaa licha yaugumu kwa magari kushindwa kupishana njia ya kati, pia nauliza ni wapi duniani utakakokuta njia rahisi na salama inayokubalika na askari wa usalama barabarani kuruhusu magari yapite njia zote mbili kuelekea upande mmoja?

  8. Maajabu yapo mengi mno na ya kushangaza bado hatujaingiza yale ya Chenji ya RADA, Twiga kupakiwa kwenye ndege kwenda ughaibuni, Polisi kutuhumiwa kuua kisha wenyewe kuunda tume kuchunguza na wakati tume inachunguza mtuhumiwa yuko mahakamani, nyingine ya kushangaza waziri kuunda tume baada ya kuambiwa hana mamlaka anasema ameunda kamati na vyombo vya habari viko kwenye usingizi wa pono, biashara inaendelea kama hakuna lililotokea hii ni Tanzania na Tanzania ni zaidi ya uijuavyo.[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
   
 2. MATESLAA

  MATESLAA JF-Expert Member

  #2
  Oct 3, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 1,252
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  We mtowa mada acha uvivu wa kusoma huu uzi teyari umeshaandikwa hapa

  mod naomba uutowe
   
 3. ligendayika

  ligendayika JF-Expert Member

  #3
  Oct 4, 2012
  Joined: Aug 31, 2012
  Messages: 1,175
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 145
  kweli hapa ni a home of great thinker. mi naipigia kura Tanzania kama ulivyotaka
   
 4. Arushaone

  Arushaone JF-Expert Member

  #4
  Oct 4, 2012
  Joined: Mar 31, 2012
  Messages: 14,357
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  Ni kweli majany na kuongeza tu ni TZ tu raisi anatawala miaka 7 ambayo ukifanya ni siku, 7 times 365=2555 lakini kumbuka rais kasafiri mara karibu 380 (zaidi ya mwaka). NiTZ tu watu watafukuzwa kwa faida ya mwekezaji, twiga kwenye ndege.. khaa ptuu!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #5
  Oct 4, 2012
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Nchi pekee dunia inayoona USAHAULIFU ni sehemu ya maisha. Hasa katika yafuatayo:-

  -EPA
  - Radar
  - Richmond
  - Rushwa ya Wizara ya Nishati
  - Mauaji ya polisi
  - Dr. Ulimboka n.k.
   
Loading...