Tanzania kusitisha matangazo ya analog Januari 2013 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania kusitisha matangazo ya analog Januari 2013

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Rutunga M, Feb 26, 2012.

 1. Rutunga M

  Rutunga M JF-Expert Member

  #1
  Feb 26, 2012
  Joined: Mar 16, 2009
  Messages: 1,556
  Likes Received: 230
  Trophy Points: 160
  Imeandikwa na mwananchi la leo

  soma hapa


  Raymond Kaminyoge
  LUNINGA au televisheni za teknolojia ya analojia zenye `matumbo' hazitafanya kazi kuanzia Januari Mosi, 2013 hadi ziunganishwe na ving'amuzi vitakavyonunuliwa kutoka kwa kampuni ambazo ni wakala wa vituo vya televisheni.

  Hatua hiyo imekuja baada ya Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa kutangaza kusitishwa kwa matangazo ya Televisheni kwa kutumia analojia kwenda digitali kuanzia Januari Mosi 2013.

  Akizungumza na Mwananchi kuhusu kauli hiyo ya Waziri, mtaalam wa vifaa vya elektroniki, Damas Mligo alisema zile luninga za zamani itabidi ziunganishwe na ving'amuzi ndipo zifanye kazi. Bei ya ving'amuzi katika kampuni mbalimbali zinaanzia Sh70,000.

  Alisema kuna baadhi ya luninga za digitali ambazo ving'amuzi vimejengewa ndani hizo zitatumika kama kawaida.
  Waziri Mbarawa aliwataka wananchi kujiandaa mapema hasa kununua ving'amuzi kwa luninga ambazo zinatumia teknolojia ya analojia.

  Alisema faida ya digitali ni kuongezeka kwa ubora wa matangazo na ongezeko la vituo vya televisheni.
  Aidha Mbarawa alisema faida nyingine ya kuingia kwa teknolojia ya digitali ni matangazo ya televisheni kupatikana katika wingi zaidi vya mawasiliano kama vile simu za mkononi na kompyuta kupitia mtandao wa intaneti.

  " Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zimekubaliana kuwa ifikapo Desemba 31, 2012 saa sita kamili usiku vituo vyote vya utangazaji vinavyotumia teknolojia ya analojia vitazima mitambo yake na kutumia digitali,"
  alisema Profesa Mbarawa.
   
 2. Chipukizi

  Chipukizi JF-Expert Member

  #2
  Feb 26, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 1,972
  Likes Received: 430
  Trophy Points: 180
  Ni technology nzuri,lengo kuwezesha wadau wa mawasiliano kutumia masafa(frequency)ambazo TV za leo inazitumia kwa kazi nyingine.Pia itawezesha wasanii kupata kipato bila rabsha.
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  Feb 26, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,471
  Likes Received: 19,862
  Trophy Points: 280
  Tanzania nilikuwa wameshaanza kutumia hii technology ..kumbe bado
   
 4. i

  iMind JF-Expert Member

  #4
  Feb 26, 2012
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 1,907
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Itawezeshaje wasanii kupata kipato bila rabsha?

  Baadhi ya vituo vya tv vinarusha both analog na digital. Ndo maana waweza kupata station kana clouds tv na TBC kwa kutumia ving'amuzi au bila king'amuzi.
  Itakachotokea ni Dec 31 ni kusitisha urushaji wa analog signals.

  Najiandaa kuingiza macontena ya vingamuzi maana najua tarehe 1 jan 2013 itakua mshike mshike.
   
 5. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #5
  Feb 26, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Hii itakuwa kitu cha maana sana, hata mtandao wa sasa itabidi hawa ma ISP wanatuibia kwa sana tu sasa, wajipange upya, maana tutakula mtandao na TV.

  Hapa ndio tutaipata utaaaamu ile teknoloji ya Apple "clouds". TiGO na ife, maana hizi signal zitaweza kurusha, mpaka simu, internet, na zinazeweza zikakupikia chai.

  The only setback ni kuwa sasa hata Serikali inaweza kukujuwa upo nyumbani au haupo, unatazama TV, ukiwa mzima au umelewa. Ni hatua kubwa sana.
   
 6. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #6
  Feb 26, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Pia tutegemee kurudishwa kodi za TV maana monitoring itakuwa kitu rahisi sana.
   
 7. Chipukizi

  Chipukizi JF-Expert Member

  #7
  Feb 26, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 1,972
  Likes Received: 430
  Trophy Points: 180
  Kingamuzi kimoja Tv moja so kodi included mkuu
   
 8. LE GAGNANT

  LE GAGNANT JF-Expert Member

  #8
  Feb 26, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 1,247
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Mbona hizo tv zenye matumbo kwenye ving';amuzi zinaona!
   
 9. Pasco_jr_ngumi

  Pasco_jr_ngumi JF-Expert Member

  #9
  Feb 26, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 1,811
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  dish langu hapa mbugani selous..... looooh, itakuwa kigae cha kukaanga nyama ya nyani????? looooh
   
 10. P

  Paul S.S Verified User

  #10
  Feb 26, 2012
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Wakuu tusi changanye mambo hapa, teknolojia ya digitali sio kama imeanza juzi wengi wetu tulioishi mikoani tumeitumia sana

  Analogi ni kurusha matangazo na tv za tumbo hupokea kwa kutumia antena za kawaida (miba)
  So kama wewe unatumia dish na receiver maana yake unatumia digitali, kwahiyo wenye tv za tumbo na madish na receiver tupo kwenye digitali, na madish tutatumia kukamata free to air chaneli

  Tatizo na changamoto ni kuwa je hiyo receiver yako inaweza kupokea aina ya channel unataka, mfano kama una mediacom upo kwenye digitali lakini huwezi kukamata chaneli fulani hadi ununue receiver yao, hapa ndio mtihani kwa wahusika.
  Itv watakuja na recever yao startv, tbc nao na receiver zao, sasa itakuwaje? tutanunua receiver ngapi

  Swali je kama mimi nina tv ya digitali nitawezaje ku access chaneli za Ting au Startime au easy tv iwapo kila mmoja ana recever yake na card haziingiliani? au pamoja na kuwa na tv ya digitali bado nitalazimika kununua receiver husika ili ku access chaneli zao

  Changamoto nyingine ni kwa hawa warushaji wa chaneli wanatumia teknolojia ngumu kidogo kwenye usamabazaji wake, wenyewe wanaita dvb na nini sijui kama sijakosea

  Teknolojia hii haitumii setelaiti inatumia minara kurusha signal kitu kinachoifanya ichukue muda mrefu kuwafikia walaji kwa maana ya wingi wa minara,
  mfano startimes wana mnara mmoja tu hapa DSM basi ukitoka nje ya mji kidogo tu ina kuwa matatizo, inabidi wafunge minara mingi kila baada ya umbali fulani ili walaji wapate signal nzuri

  Njia mnzuri zaidi ya kurusha matangzo ni kwa kutumia setelaiti kama wafanyavyo DSTV, unafunga dish lako unaelekeza usawa wa setelite popote ulipo mchezo umekwisha

  Sasa jiulize wewe wa mpitimbi madongo kuinama mtapata lini minara ya kupokelea signal kutoka kwenye vingamuzi vyenu vya dvb na jamaa wa kwenye tv wakikamilisha zoezi wanatoa chaneli zao kwenye free to air kwenye satalite na kuzibakisha kwenye minara yao tu, Hii inamaana wale wenye madish tutaishia kuangalia chaneli za nje tu

  Hii inanifanya niamini kuwa zoezi hili bado gumu kidogo kama anavyosema huyo muheshimiwa
   
 11. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #11
  Feb 26, 2012
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Nadhani kuna watu wanachanganya mambo. Nawshauri watazame clip hii ya video wajue kuna implicationgani warusha matangzo kuswich off Analog transmission.  Dondoo
  • Watumiaji wenye decoder na wanaopokea matangzo ya satelite (madish) hawana cha kuhofia hata kma wana Televison za tumbo.....
  • Watumiaji wanaopokea matangazo kwa njia ya cable nao hawana cha kuhofia
  • Kwa wasiokuwa na dish na cable yaani ambao wanategema antena za kawaida kupokea matangazo ya FTA(free to Air) yataonekana kama
   • Televishen ya mtumianji ni ya kisasa yaani ina inbuilt digital tuner . kwa set za zamani na TV zisizo na Digital tuner hata kam ni flat creen mtumiaji atalazimika kununua digital tuner ya pembeni ( Inafanana kama ka decoder)

  NB
  Kwa hiyo unaponunua tv set mpya uliza kama iko Digital ready. Sabanu tanzania mashirika kama TBS hayafayi kazi yao vizuri unaweza kuta mpaka sasa waagizaji TV wanaruhusiwa kuleta na kuuza TV ambazo si digital ready. Na si formula kila flat screen ni digital ready.

  hii ni sehemuya chapisho lnaloapatikana pia kwenye ka gym ka mtazamaji - DIGITAL TELEVISHENI NINI TUTARAJIE
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #12
  Feb 26, 2012
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Mfano wa kifaa watakachohotajika kununua watu Wenye TV sizokuwa Digital ready na hawana uwezo au hataki Kulipa satleite au cable Transmiision na wanataka kuendelea kupokea matangazo ya FTA ni huu hapa
  [​IMG]

  Kwa mujibu wa ebay gharama ya hutu tu vifaa ina range lakini sidhani kam inaweza kuzidi $50 . Ukinunua kifaa hicho utaendelea kuona matanagazo ya free to ya digital bila shida hata kama una TV ya 1990 lol

  Au sijaelewa wakuu ?????
   
 13. twatwatwa

  twatwatwa JF-Expert Member

  #13
  Feb 26, 2012
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 2,038
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Hilo analosema waziri ni ndoto. mpaka leo hao startime awajaweza kusambaza ata robo ya nchi sasa hii miezi kumi ilobaki ndo wataweza ? Labda watumie satelaiti .kwa fundi kama mimi nawaona kama mfanyabiashara anayelazisha kuuza kuhuza mti wa xmas wakati dec aijafika
   
Loading...