Tanzania kupiga marufuku mashirika ya hisani ya uingereza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania kupiga marufuku mashirika ya hisani ya uingereza

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sijali, May 23, 2011.

 1. Sijali

  Sijali JF-Expert Member

  #1
  May 23, 2011
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 2,054
  Likes Received: 405
  Trophy Points: 180
  Habari hii ni ya mwanzo katika the East African. Kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Tanzania, Bernard Membe, iwapo kampuni ya BAE itatekeleza mpango wake wa kulipa fedha za fidia (zilizotokana na rushwa katika mauzo ya Radar) kwa mashirika ya hisani ya Uingereza yanayotoa huduma za binadamu Tanzania, badala ya kuzipeleka kwenye mfuko wa serikali, basi Waziri huyo atayapiga marufuku mashirika yote ya hisani ya Uingereza nchini. Membe alinguruma:

  “If the UK goes ahead or sticks to its original plan to reimburse money stolen from our government, through their own charitable organisations in the country, then we shall ban all such organisations that originate from Britain,”

  Miongoni mwa mashirika ambayo yatakayofukuzwa kama hatua hiyo ikipitishwa ni:
  Save the Children, Oxfam, Action Aid na Care Tanzania, ambayo yanatoa huduma za binadamu kwa mamilioni ya Watanzania.

  Jee, kitendo cha Membe kitakuwa na mantiki? Hii siyo kama kumtishia mwanamke asiyekupa ngono kwa kutia moto nyumba yako!
   
 2. F

  FJM JF-Expert Member

  #2
  May 23, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Ah wapi! ajaribu aone kasheshe.

  Uingereza kupitia shirika lake la maendeleo (DFID) ni miongoni mwa wachangiaji WAKUBWA kwenye bajeti ya serikali (GBS). Mwaka jana walitoa almost 26 % ya hela zote za wafadhili kwenye GBS. Haitalipa hata kidogo kwa Membe kuanza malumbano na Uingereza. Tutakwama!
   
 3. The Prophet

  The Prophet JF-Expert Member

  #3
  May 23, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 682
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  by the way, who is this person called Membe?
   
 4. Guyton

  Guyton JF-Expert Member

  #4
  May 23, 2011
  Joined: Jan 15, 2011
  Messages: 252
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Tukiwaambia waanje porojo tujenge uchumi hawaelewi, wao ni kutegemea wahisani tu, matokeo yake ndo dharau kama hizi.
  THERE IS NO FREEDOM WITHOUT DEVELOPMENT.
   
 5. Ziada Mwana

  Ziada Mwana JF-Expert Member

  #5
  May 23, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 201
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni waziri wa mambo ya nje, mwenyeji wa mkoa wa Lindi huko mitaa ya Ruangwa na Nachingwea, ni mwanachama wa chama cha mapinduzi.mchapa kazi hodari na tegemeo mojawapo la ccm. kuhusu hoja yake ya kuwaondoa waingereza hiyo hata mimi siipendelei, kwani bado tunahitaji msaada wao. pia membe akumbuke kuwa ni waingereza haohao ndio waliopigania haki yetu hiyo.hivyo ni muhimu tukaonesha kuwaamini.
   
 6. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #6
  May 23, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0

  One of the Tanzania with retarded minds,
  you call them your Ministers
   
 7. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #7
  May 23, 2011
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,919
  Likes Received: 608
  Trophy Points: 280
  Labda niulize, I may not know anything.
  Who is it usually benefit from these Charitable organizations? Is it Tanzania or The USA.
  If I get an answer, I will advice Membe.
   
 8. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #8
  May 23, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Hivi Membe kama hana cha kuongea kwa nini asikae kimya tu. Anajiabisha huyu "Rais" Mtarajiwa
   
 9. eliakeem

  eliakeem JF-Expert Member

  #9
  May 23, 2011
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 2,900
  Likes Received: 1,005
  Trophy Points: 280
  Kwanza kudai kizo pesa zilizoibwa hawakwenda....... pili hawajawawajibisha akina chenge waliosababisha huo wizi..... halafu sasa wanashupalia sana pesa....
  wamkamate chenge ndiyo tutaona wana machungu......
   
 10. TabletFellow

  TabletFellow JF-Expert Member

  #10
  May 23, 2011
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 928
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kakurupuka yule pimbi!!! huwezi kamwe kusema utaban shirika la donor wakati hata pesa ya per diem wanakupa wao

  he is just trying to buy some mileage and unfortunately ahvutii, hatii hamas wala hajui kujenga hoja!!!

  I never liked Member, never will .........
   
 11. G

  GJ Mwanakatwe JF-Expert Member

  #11
  May 23, 2011
  Joined: Mar 26, 2011
  Messages: 241
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Zile ni fedha zetu sio msaada, hivyo hawana haki kutupangia matumizi zirudishwe serikalini mara moja hatutaki porojo. BAE ni kampuni/shirika, sio nchi au mnamaana huo uamuzi ni wa uingereza sio wa bae? Tuna uwezo wa kujitegemea hata ktk bajeti kama tukiamua, na ni wao ndio wanaotudekeza tuwategemee wao katika misaada ili watuibie vizuri. Hata hayo mashirika yao ya misaada yakiondoka au kufukuzwa ni sawa tu , hayana faida yoyote zaidi ya kuendelea kutudumaza akili zetu kwamba bila wao hatuwezi kuishi. Mashirika hayo yanayojiita ya misaada yapo nchini kwa masrahi yao na nchi zao wala sio masrahi ya tz na watz wake, TUAMKE, tuache kulala.
   
 12. N

  Ngo JF-Expert Member

  #12
  May 23, 2011
  Joined: May 25, 2010
  Messages: 284
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  [GJ Mwanakatwe:Zile ni fedha zetu sio msaada, hivyo hawana haki kutupangia matumizi zirudishwe serikalini mara moja hatutaki porojo. BAE ni kampuni/shirika, sio nchi au mnamaana huo uamuzi ni wa uingereza sio wa bae? Tuna uwezo wa kujitegemea hata ktk bajeti kama tukiamua, na ni wao ndio wanaotudekeza tuwategemee wao katika misaada ili watuibie vizuri. Hata hayo mashirika yao ya misaada yakiondoka au kufukuzwa ni sawa tu , hayana faida yoyote zaidi ya kuendelea kutudumaza akili zetu kwamba bila wao hatuwezi kuishi. Mashirika hayo yanayojiita ya misaada yapo nchini kwa masrahi yao na nchi zao wala sio masrahi ya tz na watz wake, TUAMKE, tuache kulala.


  Mkuu Serkali haioni haibu kukomalia pesa ambayo walikuwa hawana mpango wa kuipata na hao wanaoidai walishasema hakukuwa na rushwa kwenye manunuzi ya Rada? Leo hii hiyo pesa imetoka wapi wakati walikana mwanzoni? Wamesaidiwa kuipata hiyo pesa sasa hivi ndo unaona ni haki yako, mbona hukuidai mwanzoni? Umeonyeshwa kulikuwa na wizi kwenye rada ndo maana hiyo pesa inataka kurudishwa, Serikali Imewafanyia nini Waliyohusika?

  Una uhakika serikali yako na Viongozi waliyopo madarakani wanaweza kukusanya mapato ya kujiendesha yenyewe? Kwa vyanzo vipi Tanzania ilivyonavyo kwa sera mbovu tulizo nazo kwenye hivyo vyanzo? Kwa uwajibikaji upi wa Viongozi wa Serikali yako?Ni akili ya viongozi wako na wewe ndo Imedumaa kutegemea misaada, Wahisani wamekata milija na leo hii serikali iko hoi hawana pesa wanakopa kwenye local banks. Ni haibu Mwanakatwe kwako na Serikali yako.

  Hafadhari na hizo NGOs zinatowa ajira kwa Watanzania wachache kuliko kama zisingekuwepo Maana watu wanahudumia familia zao kwa kufanya kazi kwenye hizo NGOs
   
 13. Fredwash

  Fredwash JF-Expert Member

  #13
  May 23, 2011
  Joined: Oct 27, 2009
  Messages: 593
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 60
  walishaona kuwa wakizileta hapa kuna watu washareserve viwanja ili wajijengee mahekalu kwa pesa hizo wakashtukia na kuona watafute njia mbadala.... sasa ye ajaribu aone. kama hawajaanza na yeye kumfungia asiingie kwao
   
 14. m

  mmakonde JF-Expert Member

  #14
  May 23, 2011
  Joined: Dec 26, 2009
  Messages: 967
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mpaka leo nashindwa kuelewa kwa nini serikali ya UINGEREZA haijawapiga marufuku kuingia UK hawa mamluki wa CCM ,hasa baada ya scandals nyingi kuanzia EPA na mengineyo.Halafu bado wanachangia budjet!!!!!
   
 15. F

  Fideline JF-Expert Member

  #15
  May 23, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 200
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Membe ni mwehu.Na wehu tunao wengi.Serikali inayotegemea 60% misaada haiwezi kuwakoromea donors wake.Awaaache watumie hela wanavyotaka wao cause si Membe wala yeyote serikalini aliyethubutu kufuatilia hela hiyo toka BAE Systems.

  Uingereza wana uwezo wa kutukoromea kwa sababu sisi tumeshika makali.Kwa taarifa yake Zimbabwe mambo yalianza hivi hivi mpaka wakafika walipo sasa.Serikali inapaswa kujenga uchumi kwanza ndipo tuweze kuwakoromea hawa wazungu!!!! Otherwise tukae kimya!!!
   
 16. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #16
  May 23, 2011
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana nawe kuwa tukiamua tunaweza kujitegemea. Ila kwamba fedha ni zetu sina uhakika kwa sababu:

  • Hatukuwahi kuzidai - kama si yule mama Short wa Labour wala zisingepatikana (kumbuka tuliambiwa na serikali yetu kuwa tuliyolipa ilikuwa bei halisi na hatukulanguliwa.
  • Kumbuka ile ni faini ambayo BAE wameaamuriwa kuilipa na Mahakama Kuu ya Uingereza kutokana na "unfair business practices", sio kwamba Mahakama ilipunguza bei ya Rada kiasi kwamba serikali (iliyoridhika yenyewe kulipa hiyo bei) iwe na haki ya kurudishiwa. Hata Mahakama haikutamka wazi kuwa serikali ya Tanzania ndio ipewe hiyo faini bali jamii zilizoko Tanzania. Ingeamuriwa BAE walipe hiyo faini Haiti, serikali ingepinga kwenye mahakama gani ukitilia maanani walishasema mara kadhaa kuwa hakukuwa na utata wowote kwenye hayo manunuzi ya Rada?
  Kwangu mimi bora kina CARE wapewe, angalau kuna senti kidogo zitawafikia watu waliosababishiwa umasikini. Kina JK wanataka kutanulia tu na hizo pesa, hakuna lolote jingine.
   
 17. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #17
  May 23, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Memba anaongea tu hawezi mfukuza yeyote .Anataka asikik lakini ajue kauli hizi wanazisoma waingereza na wataanza kucheza na CCMhapo watajua ugumu wa Chupi kwa nini iwe na fomula kuvaa . Wacha pesa zipitie huko siyo kukosa uzalendo ila tabia za serikali narushwa na kuto kujali wanachi na maisha yao
   
 18. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #18
  May 23, 2011
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Mkuu siyo kwamba tutakwama, Ila Membe atakwama. Boss wake atakachokifanya ni kumtoa kafara (kama walivyowatoa kina MARANDA leo kwa kuwafunga jela miaka mitano) kwa kuweka mtu mwingine ili GB ijiridhishe kuwa wana-deal na friend not foe. Huwezi kutishia kufukuza mashirika yanayotoa huduma kwa wananchi kwa kutumia pesa zao nchi kisa wamepewa pesa uliyoitoa kununulia radar kifisadi waendeleze huduma. Maswali utakayoulizwa ni je wale walioingia deal hilo umewachukulia hatua gani?, kama kweli una uchungu na pesa unayodai yako?.
   
 19. Msarendo

  Msarendo JF-Expert Member

  #19
  May 23, 2011
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 9,127
  Likes Received: 3,316
  Trophy Points: 280
  He! he! England aint got nothing to loose!..ndo kwanza watashukuru.
   
 20. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #20
  May 23, 2011
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Hii pesa ni ya msaada si ya Tanzania kama wengine wanavyosema. Kama tungelipa Lawyers kwenye hii case na kushindana na ma lawyer wa hiyo kampuni tusingeshinda kesi wala kupata hii settlement. Gharama za kesi nani kalipia?? Pesa ambayo Tanzania ilishalipa kwa njia ya rushwa ni kwa nini irudishwe kwa serikali ileile??. Kama Tanzania ikikataa kuchukua pesa basi UK watoe Scholarship kwa Watanzania kusoma huko kwa hiyo pesa hii itasaidia jamii zaidi kama ni Pound 30,000,000 na wakitoa Scholarship za pound 20,000 watasaidia wanafunzi 1,500. Hawa wanafunzi watakuwa middle class Tanzanians popote walipo na watasaidia jamii kuliko hao mafisadi na elimu waliyopata ni ya maisha.
   
Loading...