Tanzania kuiuzia mahindi Zimbabwe tani 700,000

Tunauza Mahindi au Unga?
Maana wakulima walipigwa mkwara wasiuze mahindi ghafi nje.!
Wanyonge tutazijua rangi zote za kinyonga... tuombe iwe kheri maana msimu huu hata hapa kwetu hali ya mavuno ya mahindi si njema sana. Je tutaruhusiwa sote kuuza au serikali ndio itauza hayo mahindi? Hata Sudan kusini wanayahitaji sana...
Ah!!
Mchana inzi usiku mbu...
 
Hayo ni matunda ya ziara ya Rais Magufuli nchini Zimbabwe.
Rais wa Zimbabwe amemshukuru sana Rais Magufuli kwa kufikia makubaliano hayi, Mnangagwa amesema Tanzania ni rafiki wa kweli.
Naye Dr Magufuli amesema huo ni mwanzo wa kufungua fursa mbalimbali za kibiashara na kwa kuanzia ni huo mkataba uliosainiwa wa kuiuzia Zimbabwe hizo tani 700,000 msimu huu kwa kuwa tumezalisha zao hilo kwa ziada.
Source ITV habari!
azungumze lolote kuhusu zile KOROSHO ALIZOWAPORA WAKULIMA HUKO KUSINI! AMESHINDWA KOROSHO ATAWEZA MAHINDI? MUONGO MKUBWA
 
Wabunge ccm majority saidieni taifa lipate katiba bora itayolinda umoja na ustawi wa taifa. Zimbabwe ililisha Afrika, sera mbovu za Mugabe zikavuruga taifa kilimo na uchumi. Robo ya Wazimbabwe wapo uhamishoni SA,Zambia nk.
mbunge anayeomba muongozo wa kitambi hilo hawezi kulijua
 
Tani 700000 (laki 7)? Unajua tani 1 ni kilo 1000. Kwahiyo 700000×1000= kilo Mil 700. Umetia chumvi hii taarifa
 
Wabunge ccm majority saidieni taifa lipate katiba bora itayolinda umoja na ustawi wa taifa. Zimbabwe ililisha Afrika, sera mbovu za Mugabe zikavuruga taifa kilimo na uchumi. Robo ya Wazimbabwe wapo uhamishoni SA,Zambia nk.
Kweli hujafa hujaumbika-Tanzania kuiuzia Zimbabwe mahindi ni kama ndoto hivi. Sote tujitafakari.
 
Kweli hujafa hujaumbika-Tanzania kuiuzia Zimbabwe mahindi ni kama ndoto hivi. Sote tujitafakari.
Zimbabwe was Africa's /world food basket Leo hii wanatia huruma na huyu mnagwagwa Sera zilezile full mabavu sijui watatokea wapi.magu anaenda kutuharibia nchi kama mugabe
 
Hali ya mavuno s nzuri Sana nadhan mmejionea mvua za mwaka huu kwa wakaz wa moshi Arusha nadhan mnanielewa vzuri sasa tuuze tan lak7 haya any way vp na korosho hajapata Wateja bado maana znakutana na msimu mwingne huku za mwaka jana bado zpo ghalani tuwe makini jaman hawa jamaa wataharibu kila kitu Kama tukiendelea kuwachekea
 
Wabunge ccm majority saidieni taifa lipate katiba bora itayolinda umoja na ustawi wa taifa. Zimbabwe ililisha Afrika, sera mbovu za Mugabe zikavuruga taifa kilimo na uchumi. Robo ya Wazimbabwe wapo uhamishoni SA,Zambia nk.
Ndio maana jamaa wa ufipa wameacha kukarabati makao yao makuu, eti wanangoja katiba mpya ipatikane kwanza. Ha ha ha, tabu tupu.
 
h
Hayo ni matunda ya ziara ya Rais Magufuli nchini Zimbabwe.

Rais wa Zimbabwe amemshukuru sana Rais Magufuli kwa kufikia makubaliano hayi, Mnangagwa amesema Tanzania ni rafiki wa kweli.

Naye Dr Magufuli amesema huo ni mwanzo wa kufungua fursa mbalimbali za kibiashara na kwa kuanzia ni huo mkataba uliosainiwa wa kuiuzia Zimbabwe hizo tani 700,000 msimu huu kwa kuwa tumezalisha zao hilo kwa ziada.

Source ITV habari!

Hivi jiwe/katelephone wanakumbuka alikataza kusafirisha mahindi nje kweli mpaka wayachakate???? au nchi hii mwenye akili timamu ni yeye tu na wajeda wana kiwanda huko songea????? na amechukua miaka 4 kujua hili la kuzaliswha ziada baada yayeye kutembelea nyanda za juu kusini zile kelele zoote za wakulima hakumbuki na wala hataki kujua tani ngapi zilikuwa zinaenda nje ya nchi???? unajua upya/ulevi wa madaraka na ushamba umegharimu pesa nyingi zaidi ya wizi/ufisadi na vyeti hewa tokea nchi hii iundwe????

hii tisa kumi utasikia wajeda ndio wapeleke, sijui kama anajua korosho zimeua malori ya wajeda kibao si mnajua waliingiza malori mapya ya kihindi wakati wafanyabiashara hutumia mikangafu kwenye rough road yanayovuta matera (scania) konki nyie dona coountry mungu anawaona.

2020 ajenda iwe kuondosha hivi vitu kwanza sababu gharama yake kubwa mno kwa walipa kodi maskini na sekta binafsi ujinga maradhi, ufisadi na etal visubiri kwanza.
 
Tani 700000 (laki 7)? Unajua tani 1 ni kilo 1000. Kwahiyo 700000×1000= kilo Mil 700. Umetia chumvi hii taarifa
Hizo ni gunia milioni saba zenye ujazo wa kg100/gunia.

Nami nakubaliana nawe kuwa Johnthebabtist hapa kazidisha chumvi!

Sio kwamba gunia 7 milioni ni nyingi sana; lakini kwa sasa serikali haina kiasi hicho!
 
Nimecheka, hivyo walionunua mashine za kusaga kwa kauli mbiu ya mwaka jana ya kuuza unga ndo imekula kwao?
Unga tukilenga hawa majirani wa EAC, ni karibu nasi na tunalo soko la pamoja.
Kuongeza thamani ni bora, kuliko kuuza mali ghafi.

Vijana wanapata ajira (kwenye mashine hizo, na mnyororomzima wa zao hilo); bidhaa zinazotokana na uzalishaji huo wa unga inabaki hapa hapa au nayo inauzwa nje kama bidhaa, n.k.

Tuuze unga. Weka mashine pale mpakani, tengeneza unga kwa viwango vinavyotakiwa, fungasha vizuri na vusha mpaka ukatafute soko. Ugumu upo wapi?
 
Hayo ni matunda ya ziara ya Rais Magufuli nchini Zimbabwe.

Rais wa Zimbabwe amemshukuru sana Rais Magufuli kwa kufikia makubaliano hayi, Mnangagwa amesema Tanzania ni rafiki wa kweli.

Naye Dr Magufuli amesema huo ni mwanzo wa kufungua fursa mbalimbali za kibiashara na kwa kuanzia ni huo mkataba uliosainiwa wa kuiuzia Zimbabwe hizo tani 700,000 msimu huu kwa kuwa tumezalisha zao hilo kwa ziada.

Source ITV habari!
Huo ni mkataba hewa,ha hali njnayoiona hatuna mahindi ya kuuza nje mwaka huu,tukiuza sisi itabidi tuagize,nataka nione ikigika mwezi wa 9 kama utasikia kuna mtu anapeleka mahindi huko kwani bei ya ndani itakuwa kubwa kuliko hiyo ya kuuza nje.
 
Rais Magufuli akiwa Zimbabwe amefungua fursa ya soko la Mahindi nchini Zimbabwe, sasa Tz itauza tani Laki saba (700, 000) za zao hilo Nchini Zimbabwe kwa kila mwaka.
Tanzania inapaa kiuchumi, Rais Magufuli anafungua fursa.
IMG-20190529-WA0182.jpeg
 
Back
Top Bottom