Tanzania Katika Miaka Mitano Ijayo: Inatisha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania Katika Miaka Mitano Ijayo: Inatisha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kichuguu, Feb 14, 2011.

 1. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #1
  Feb 14, 2011
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Nina wasiwasi sana na hali ya Tanzania kiuchumi na kisiasa katika kipindi cha miaka mitano ijayo kwa sababu kadhaa:

  (1) wafadhili hawatahudumia bajeti ya serikali kama ilivyozoeleka kwa sababu ya utawala mbovu, na ukweli kuwa EU wameshajua kuwa serikali iliyopo madarakani imeingia kimabavu. EU wakisitisha misaada yao tu, basi tutasahau na misaada ya USA, Australia na Japan. Huenda tukabakiwa ni misaada kutoka China na Canada tu. Sina uhakika kama China iliwahi kutoa msaada wa kulipia bajeti ya serikali. Msaada wa Kanada kwenye bajeti ya serikali huwa ni mdogo sana. Serikali inaweza kulazimika kufanya mambo kadhaa: kupunguza wafanya kazi wake, na hivyo kuongeza unemployment rate, kuchapisha hela nyingi za madafu, na hivyo kuongeza inflation, au kujisahau na kutelekeza majukumu yake huku nchi ikibaki haina usimamizi.

  (2) Kikwete atakuwa bize sana kujijenga yeye na familia yake kwa vile uraisi wake ni swala la familia yake. Kwa sasa hivi kikwete hahitaji kura zetu tena, na hata akivurunda vipi, hilo yeye halimhusu tena. Kwa mazingira hayo, rushwa itashamiri sana kipindi hiki, na hivyo madhara yote ya rushwa yatang'aa sana na kufanya maisha yawe magumu zaidi.

  (3) Ndani ya CCM kutakuwa na msigishano mkubwa sana baina ya watu wanaotaka kumrithi Kikwete pale Magogoni: watu kama Lowassa, Nchimbi, Mwandosya, Membe, Magufuli, Sita, Mwakyembe, na wengineo watakwaruzana sana kupitia bunge na kulifanya bunge lisiendeshe majukumu yake ipasavyo hasa ukizingatia kuwa halina uongozi thabiti.

  (4) Kutokana na hayo yote, kutakuwa na malalamiko sana kutoka kwa wananchi wa kawaida ambayo yatatiwa chumvi zaidi na wagombeaji wa CCM ili kila upande ujipatie wafuasi wengi. Malalamiko hayo ya wananchi yataendana na maandamano na migomo ya mara kwa mara ambayo itaweza kuleta vurugu nchini na kusababisha watu wengi sana wapoteze maisha hasa kwa vile polisi wetu wanapenda sana kukamua trigger huku wakielekeza mitutu yao kwa raia.

  (5)Kutaibuka mtengano wa wazi baina aya makundi mbalimbali ya jamii, ambayo yatapandikizwa na wanasiasa wa CCM kuwania uraisi wa mwaka 2015.


  Yote hayo hapo juu yanatisha sana ila tujiandae kukabiliana nayo.
   
 2. SHERRIF ARPAIO

  SHERRIF ARPAIO JF-Expert Member

  #2
  Feb 14, 2011
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 7,081
  Likes Received: 1,819
  Trophy Points: 280
  Upole, amani na utulivu miongoni mwa watanzania vidumu!!:msela:
   
 3. YeshuaHaMelech

  YeshuaHaMelech JF-Expert Member

  #3
  Feb 14, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 2,624
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Eee Mungu naomba uhai nikione kifo cha sisi em!
   
 4. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #4
  Feb 14, 2011
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Hiyo miaka 5 mbali, yatunisia na egypt ndo solution. Bila hivyo, tutafika huko kweli tena kwa aibu zote.
   
 5. kisu

  kisu JF-Expert Member

  #5
  Feb 14, 2011
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 803
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Chukua Chako Mapema!!!
   
 6. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #6
  Feb 14, 2011
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,584
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Bajeti ya kutegemea ufadhili kwa nguvu sasa inatuadhiri ile mbaya!
   
 7. Nyenyere

  Nyenyere JF-Expert Member

  #7
  Feb 14, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,568
  Likes Received: 1,934
  Trophy Points: 280
  Lakini JK alidai wakati wa kampeni kuwa wafadhili wameahidi misaada zaidi tukimchagua.:A S 20:
   
 8. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #8
  Feb 14, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Labda ataongeza safari za nje kutafuta misaada zaidi! Cha ajabu sehemu nyingi ameshakwenda maradufu mpaka sasa anaona aibu kurudia tena.
  Kwa hiyo nchii bila misaada ya wafadhili na the so called wenza kati maendeleo itadhalilika?!
   
 9. I

  Interested Observer JF-Expert Member

  #9
  Feb 14, 2011
  Joined: Mar 27, 2006
  Messages: 1,402
  Likes Received: 434
  Trophy Points: 180
  Kichuguu,
  Sasa hivi kumezuka fisi ambaye anangojea mkono uanguke audake. Serikali ya CCM hawana njia yoyote ile kumkwepa huyu fisi. Lazima tuliwe safari hii. Kuna safari nyingi mno za mawaziri zimefuliza kwenda China, na huko kote waaambiwa kuwa pesa zipo, lakini kitu kimoja tu! Si mna dhahabu, gesi, Copper,etc etc basi tupeni hizo resources na sisi tutawajengea mnachotaka.

  Hapo ndipo kichwa kinawauma serikali ya CCM, je wafanyeje? infact China can enroll CCM in its lifetime, but headche is how to tell the people that they exchanged this country resources with such investments? Hawa CCM ni Mafisadi, lakini vile vile wana kale ka-uzalendo kwa nchi yao kama mtutu yeyote----conflict-- of interest?
  ATC privatization negotiation kwa wachina ndipo hapo ilipoanguka, maana walidai wapewe resources kama gaurantee ya hiyo investment. Yaani wapewe shirika, market na vilevile resources!!
   
 10. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #10
  Feb 14, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  YeshuaHaMelech ni kama ulikuwa kwenye akili yangu kila siku naomba niishi ili nione siku ccm itakapofukiwa kaburini
   
Loading...