Mr Dudumizi
JF-Expert Member
- Sep 9, 2020
- 6,885
- 12,325
Habari zenu wana JF wenzangu. ama baada ya salam ningependa sasa nijielekeze kwenye mada husika.
Ndugu wana JF wenzangu, leo asubuhi mimi na watanzania wenzangu tulikuwa tumealikwa katika birthday ya rafiki yetu mkenya, ambayo imefanyika nyumbani kwake huko Melvin hapa Johannesburg.
Kama ilivyo ada, sehemu yoyote inapowakutanisha watanzania na wakenya lazima pawepo ubishi wa aina fulani. Eidha inaweza kuwa ubishi wa siasa, uchumi, maendeleo nk. Ila kwa leo naona ubishi wetu ulijikita zaidi katika nguvu za kijeshi za nchi zetu kati ya Tanzania na Kenya.
Kwa upande wa Tanzania sisi tulijivunia historia nzuri ya jeshi letu, ambapo toka tulipopata uhuru mwaka 1961, jeshi letu halijawahi kushindwa oparation au vita yoyote hapa duniani. Tukianza na historia ya ukombozi wa nchi za kusini mwa Afrika, jeshi letu lilitoa mchango mkubwa katika ukombozi huo kwa kuwatrain wapigania ukombozi mbali mbali kutoka katika nchi za Zimbabwe, Msumbiji, Afrika kusini, Namibia.
Lakini kama hiyo haitoshi jeshi letu lilishiriki moja kwa moja katika vita vya ukombozi kule Zimbabwe, Msumbiji nk, hadi kupelekea mamlaka za wakati huo kukaa chini na wapigania ukombozi hao na kuangalia namna ya kumaliza vita, na hatimae malengo ya wapigania ukombozi hao yakatimia kwa kukabidhiwa serikali zilizokuwa zinaongozwa na walowezi wa kizungu huko Zimbabwe na Msumbiji.
Hapo hatukuzungumzia vita ya Uganda, uzuiaji wa mapinduzi ya kisiwa cha Comoros, kuwatimua na kuwasambaratisha M23 kule Congo (japo kwa sasa inasemekana wameanza kurudi kwa kasi baada ya kugundua kuwa jeshi letu halipo tena katika maeneo yao)
Kwa upande wa ndugu wetu wa Kenya wao walizungumzia mafanikio ya jeshi lao katika oparation mbali mbali za kuleta amani katika nchi zenye mizozo, pia wanasema jeshi lao limefanikiwa kwa kiwango kikubwa kuwasambaratisha wapiganaji wa alshabab ambao walikuwa ni tishio katika ardhi za Kenya na Somalia.
Sasa basi baada ya mabishano marefu huku kila mtu akitetea jeshi lao. Nikaona bora nije hapa niwashirikishe na nyinyi wana JF wenzangu ili kila mtu achangie kwa kile anachokijua kuhusu majeshi yetu haya ya East Africa Countries.
Jukwaa hili lina mchanganyiko wa raia kutoka nchi mbali mbali za East Africa, kwahiyo ninatarajia kupata majibu sahihi kutoka kila pande ya kanda yetu ya Afrika mashariki. Hapo chini kushoto ni mwanajeshi wa Kenya, akiwa na mwanajeshi wa Tanzania kulia.
Asanteni na karibuni kuchangia kwa hekima.