Tanzania Isishiriki London Olympiki 2012? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania Isishiriki London Olympiki 2012?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Oct 11, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Oct 11, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kwa vile tunategemea neema ya Mungu kufanya vizuri, nashauri Tanzania isishiriki mashindano hayo. Tusishikiri kwa sababu hatutaki kushinda bali tunataka tuwepo kwenye orodha ya nchi zitakazopita mbele kwenye gwaride la wanamichezo wote. Kwa vile Waziri wetu wa Michezo ameshindwa kabisa kuandaa timu kwa karibu miaka 4 sasa tangu Olimpiki ya China 2008 ni wazi kuwa hatuna uwezo, vifaa, mbinu wala lengo la kufanya vizuri.

  Na hatuna watu wenye uwezo wa kufikiria namna ya kujiandaa na mashindano haya hasa ukiangalia kuwa karibu mashindano yote ya kimataifa ya mwaka huu ambapo nchi mbalimbali zimekuwa zikifudhu katika riadha Tanzania imefanya vibaya na mara zote ni kwa sababu ya "kukosa maandalizi ya kutosha".

  Sasa kwanini tusiamue kutoshiriki hadi pale tutakapokuwa na uongozi wa kisiasa wenye lengo la kuhakikisha timu zetu zinafanya vizuri na kutenga fedha na muda wa kutosha kwa maandalizi.
   
 2. Z

  Zion Train JF-Expert Member

  #2
  Oct 11, 2011
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 503
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  naafiki wazo 100% siyo tu olympika,tusishiriki michezo yoyote ya kimataifa tunaenda kutia aibu tu, tungejiwekea mkakati wa kama miaka miwili ama mitatu tujijenge haswa kisha ndiyo tuende,viongozi wengi waliopo kwenye michezo siyo wenyewe kabisa, unawaona siku ya kukabidhi bendera ya taifa tu, wanamichezo wakoje hakuna anaejali.
   
 3. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #3
  Oct 11, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Its waste of money, lakini ufisadi ndio utakaotupeleka kwenda kutumbua kodi
   
 4. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #4
  Oct 11, 2011
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  But you know tutashiriki. na tutafikia lengo letu asilimia 100% "kushiriki"
   
 5. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #5
  Oct 11, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Hapo kwenye red who decides? The principle of the IOC is that participation in the Olympics of nations must be independent of government.
   
 6. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #6
  Oct 11, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  well.. kama wao OIC watatoa fedha za mafunzo, na kugharimia wanamichezo wetu tushiriki; lakini kama fedha zitatoka kwa serikali yetu well huwezi kuwa independent of the government. Serikali ikisema haina fedha itakuwaje?
   
 7. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #7
  Oct 11, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Wabaki tu hapa nchini wale ugali wao. Huko London waende kufanya nini labda kwa hela zao na si hela za walipa kodi kwani mwisho ni ku enjoy kupanda ndege na kununua mashati tu!
   
 8. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #8
  Oct 11, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Wewe Mgonjwa kweli Kenya Riadha wanajituma na sio Viongozi wa kisiasa waiaowafanya wanariadha wao kukimbia na kushinda Medali

  This topic is bogus hapa haifai kuwa hapa kwenye Siasa... yaani watanzania hatuna siasa yaani tumechoka; bogus bugus complaints...
   
 9. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #9
  Oct 12, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Serikali itasemaje haina fedha wakati juzi tuu wizara husika imemwaga fedha kwenye sherehe isiyokuwa na mpango huko Butiamna? Kwenye Olympic hatupeleki athletes kwa maana ya kushindania medali. Ndio maana unakuta msafara una viongozi wengi zaidi ya wachezaji.
   
 10. M

  Mkandara Verified User

  #10
  Oct 13, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mzee Mwanakijiji,
  Ndugu yangu maji haya hatuyawezi hata kama tutasema tusipeleke utaonekana una wivu tu watu wanaenda kutanua roho inakuuma. Hivyo fanya ni wajibu wao kama vile wanakwenda kanisani au msikitini kufanya ibada za wanamichezo..utaumiza kichwa sana mkuu wangu Tanzania yetu ndio inakwisha hivyo! ukiwauliza wao watakwambia wee ndio hujui maanake siku hizi tuna vijana wanakimbia metre elfu 1.5 na 3 kwa kazi zaidi kuliko Filbert Bay, Juma Ikangaa na Nyambui ingawa hawashindi, hivyo tuna maendeleo ya michezo kuliko enzi za Nyerere.
   
Loading...