Tanzania Internet Rates as of May 25, 2011 (Comparison)

Maxence Melo

JF Founder
Feb 10, 2006
4,230
13,414
Mara ya mwisho kuongelea haya ilikuwa ni 2008, wakati huo tulikuwa bado tunabamizwa zaidi ya sasa, lakini mambo yamebadilika.

The below rates are the current rates of our ISPs in Tanzania, as of today (May 25, 2011):

#1. Airtel:

airtel-internet.jpg


So, hapa utapata 8 GB kwa TZS 70,000/= monthly. Kama una ofisi ndogo na unataka kutumia same bundle bado kuna routers. Routers hizi zinauzwa kwa TZS 350,000/=. Kama ukiwasiliana na kitengo cha DATA unasaidiwa haraka sana tofauti na wengine. Ukichukua package ya 96GB ikaisha haimaanishi usubiri 1yr ndo uweze ku-renew, uki-renew hapohapo package inaanza upya.

#2 TTCL

TTCL-internet.jpg

CHANZO: Products and Services

TTCL Mobile na modem zao bado ni nightmare, rates zinafurahisha lakini bado service hii ukweli haipewi support ya nguvu. Wengi wanadai ni kwakuwa ni mali ya umma, sipendi kuamini lakini nalazimika kukubaliana nao. TTCL Broadband ina speed nzuri na ya kuridhisha, tatizo ni pale unapokumbana na tatizo kupata msaada inaweza kukuchukua hata wiki. Tatizo jingine ni namna ya ku-recharge internet inapoisha, inawezekana ukalazimika kufunga safari kwenda kwao ama kupiga simu kuomba kujaziwa huku ukiulizwa password ya line yako! This' frustrating.


#3 Zantel:

Hawa rates zao ni kama za VodaCom kwa kiwango flani lakini nasikia wametoa rates mpya ambazo kilichobadilika ni kuwa bundle imekuwa doubled rate inabaki palepale. Tatizo kubwa ninaloliona kwa jamaa hawa ni pale walipoanza kuwabana watu kuwa lazima wawe wateja wa 'high life' na wateja wengi wakaanza kujikata. Zantel kwa sasa nasikia wanatoa 2GB - 40,000 per month. Si bei nzuri kulinganisha na waliowatangulia lakini ni afadhali kuliko wengine tutakaowaona chini yao. Customer service ya Zantel wanajitahidi lakini BADO wanahitaji wataalam wa DATA kuwepo kusaidia kwani wengi huonekana kubahatisha tu. Ukweli huu unakera lakini tukubali kukosolewa. 20GB kwa Zantel unalipia TZS 270,000 per month!

Rates Source: http://www.zantel.com/zconnect.html
z-connect_plan.jpg


Routers za Zantel ni nzuri na zinafaa sana kwa wenye biashara ndogo ndogo. Aidha, ukiwa nayo unaweza kuitumia kwa VodaCom pia. Nimejaribu kufanya hivyo na imewezekana.

#4. VodaCom

Rates za VodaCom ni kama nilivyozitoa hapa - Internet Bundles

VodaCom wapo safi upande wa customer service, lakini naamini kuna watakaokuwa na maoni tofauti na yangu, naamini tunaweza ku-share.

VodaInternet.jpg


Hapo juu utachanganya na za kwako!

#5. tiGO

Hawa rates zao ziko clear lakini unakuwa limited kwa speed, kuna kitu sijakielewa hivyo hii rating inaweza kuwa unfair. Angalia chini unaweza kung'amua nini kinatatiza.

Chanzo cha bei hizi ni hapa: - http://www.tigo.co.tz/internet/packages.php

tigo-packages.png


#6. SasaTel

Hawa jamaa nadhani strategically walikosea, wanatakiwa kuangalia upya service yao. Customer care saaafi lakini packages hizi ni utata mtupu

Chanzo cha bei: - Bundle Codes - Sasatel homepage

SasaTel-Internet.jpg


Kwa ujumla bado internet ni bei ya juu kwa TZ kulinganisha na Kenya, naamini kufikia mwishoni mwa mwaka mambo yatakuwa safi zaidi ya inavyoonekana kwa juu.
 
Muheshimiwa asante kutujuza, lakini tatizo lililoko kwa hawa jamaa bado ni customer care,issue zinazohusu customer rights hawaziweki wazi hadi mtu atumie nguvu ya ziada lakini matangazo ya promosheni ndo kila siku.

LET'S WAIT.
 
Muheshimiwa asante kutujuza, lakini tatizo lililoko kwa hawa jamaa bado ni customer care,issue zinazohusu customer rights hawaziweki wazi hadi mtu atumie nguvu ya ziada lakini matangazo ya promosheni ndo kila siku.

LET'S WAIT.
Uko sahihi mkuu,

Ndo maana nikawa kila sehemu nagusia suala la CUSTOMER CARE. Ni tatizo sugu, kwenye mabenki ndo balaa kabisaaaa
 
Maxence,mbona kama vile highlife wanatoa 8 GB kwa tshs 40,000/= kwa mwezi na sio 2 GB kama ulivyosema? Inakuwa bundle ya 2 GB weekly na wanachaji tshs 10,000/= for 7 days. Wana package pia ya 2 GB monthly kwa highlife. Hiyo ya line ukiongezea tshs 5,000/= kwa mwezi inakuwa sio mbaya. It is very fast na it doesn't encounter technical problems often.

Shida kubwa ni kuwa package ikiisha kabla ya kumaliza window hawaruhusu kuongeza hadi siku ziishe.
 
Ndo maana nikawa kila sehemu nagusia suala la CUSTOMER CARE. Ni tatizo sugu, kwenye mabenki ndo balaa kabisaaaa
Tatizo la kwanza ni gharama, sio customer care.

Nanunua vocha kwa muuza spana barabarani, iki boomer imekula kwangu, customer care nawajulia wapi?

Bei zishuke, period!
 
Naweza kuwa tofauti kidogo lakini nataka niwakumbushe hao wanaokuwa duty (customer care) kumwelewesha mteja juu ya 3G coverage. Ukienda kununua modem utajibiwa service inapatikana eneo lote la Dar es Salaam wakati ukiwa hata Kimara tu unapata GPRS ambapo hata attachment ya 10MB inashindwa kushusha na hapo umenunua 2GB kwa wiki.

Ni uhuni na inaboa sana na uchakachuaji hautaisha. Bei kubwa wakati service mbovu kabisa
 
Yani kwa wengine cjui lakini sasatel wako slow mpaka bac ila kwa upande wa tigo wako safi hawasumbui hata kidogo na wapo fasta
 
kadiri siku zinavyokwenda, na ushindani unazidi kuwa mkubwa. pia huduma zinazidi kuboreka, ingawa taratibu sana. tatizo lipo kwenye customer care na speed ya internet. mfano customer care ya tiGO ukipiga hadi wakutoze mia moja. wapi na wapi
 
Dah! Mambo ya internet bongo, kama zilivyo anza simu za mikononi, bei ilikuwa juu sana, na mwishowe zikateremka, japo kuwa si rahisi ukilinganisha na vipato vya raiya wa kawaida.
 
tatizo ni selikali yetu inafunga mikataba yakitapelitapeli ndomana na haya makampuni yanaendesha vitu kihuni kunasiku nimenunuwa modem ya zantel nafika nyumbani hakuna mtandao baadayasiku 2 nikawakuta mitaani na polomosheni nivoanza kuwahoji ikaonekana modem zao zinafanyakazi mikowani sehem nyingi hawajafunga vifa kama siufisadi ninini? Unafanyia polomosheni kwakitu kisichofanya kazi selikali yetu haifatili
 
Yani kwa wengine cjui lakini sasatel wako slow mpaka bac ila kwa upande wa tigo wako safi hawasumbui hata kidogo na wapo fasta

Na kubaliana na wewe 100% tigo wako safi, ila kuna vitu hawajaweka wazi kwa wateja wao ndio maana wengi wanalalamika.... Ila kwa upande wangu na enjoy sana kwa kutumia huduma ya tigo,iko fast na inakidhi mahitaji yangu....


Ila bado gharama za mtandao kwa upande wa data ziko juu sana kiasi kwamba kama hauna kipato cha kutosha kupata hii huduma kwa usahihi wake ni ndoto kwa baadhi ya watu....
 
Maxence,mbona kama vile highlife wanatoa 8 GB kwa tshs 40,000/= kwa mwezi na sio 2 GB kama ulivyosema? Inakuwa bundle ya 2 GB weekly na wanachaji tshs 10,000/= for 7 days. Wana package pia ya 2 GB monthly kwa highlife. Hiyo ya line ukiongezea tshs 5,000/= kwa mwezi inakuwa sio mbaya. It is very fast na it doesn't encounter technical problems often.

Shida kubwa ni kuwa package ikiisha kabla ya kumaliza window hawaruhusu kuongeza hadi siku ziishe.

tatizo lingine la hawa zantel modem zao zinafanya kazi mjini tu ukiwa wilayani inabidi utafute modem nyingine
 
HIZI HUDUMA ZINAPISHANA PISHANA KWELI YAN.

MIMI NATUMIA INTERNET YA VODA YA BOMBA30. NI SHILING ELFU 30 KWA MWEZI.

NDANI YA SIKU 25, NIMESHA DOWNLOAD ZAIDI YA 100GB.
 
HIZI HUDUMA ZINAPISHANA PISHANA KWELI YAN,
MIMI NATUMIA INTERNET YA VODA YA BOMBA30. NI SHILING ELFU 30 KWA MWEZI.
NDANI YA SIKU 25, NIMESHA DOWNLOAD ZAIDI YA 100GB.
Mkuu,

Hao Voda Unaowasifia nadhani kama umesoma maoni ya wengine chini hapa utakubaliana nami kuwa bado kabisa.

BTW, nimepata rates za Zantel (online) nazo nimeziambatanisha; ni uamuzi wa mtumiaji kuchagua ISP gani amhudumie.

Checki maoni ya wadau kuhusiana na internet ya Voda (kutoka hii thread - https://www.jamiiforums.com/tech-ga...-voda-internet-bomba30-ni-nomaaaaaaaaaaa.html ) :
Voda wezi wezi wezi

sina imani na hawa jamaa

Mimi Vodacom muda mrefu sana na hapa nilipo natumia Modem yao ya K3565. Kwa hapa nilipo kuibahatisha WCDMA, HSDPA ni mara chache saaaaaaana na nikiibahatisha inakaa dakika chache halafu inapotea kabisa na kubaki EDGE na wakati mwingine GPRS hata GCM. Matokeo unadownload file la 3MB kwa saa nzima. Aaaa Voda hebu rekebisheni hili. Wewe unayedownload 4GB kwa 12HRS yawezekana kabisa uko mita chache kutoka kwenye mnara wa voda. Hebu nenda sehemu za mbali na mnara uone kama hutaichukia Voda.

pia angalia baada ya kudownload GB kadhaa your speed will automatically be reduced. usifurahie ushindi ndio kwanza hata kipindi cha kwanza hakijaisha.

Nimeihama voda, wacha pumba. Speed mbovu, inakata kata, hata ya kwenye simu tu nayo ni bomu nataka niachane nayo hivi karibuni, nangoja credit zangu ziishe tu. TiGo ina afadhali inapopatikana.

Speed za Tigo hata hapa kwangu ni ndogo averages 125kbps download, lakini haikati. Voda loooo. Hata hiyo 125 nilikuwa sipati, tena kwa kukata ndio usiseme.

Teh huku mwanza zain ndiyo komesha maana speed kwenye download inasoma mpaka 168kbps then ile connection speed inachezea kwenye 2mbps had 3mbps hyo 4gb anayosema hapo juu naweza ipata kwanzia masaa 7-8

wanaosifia voda nadhani hawajajaribu mitandao mingine, mimi nipo eneo ambalo napata mawimbi ya hsdpa kwa mitandao yote inayoruhusu mawimbi hayo, airtel is the best, hakuna cha voda wala tigo, tena kwa bomba subscription ndio hovyo kabisa.

ttcl broadband ndio wenyewe. Speed hakuna mfano. Hizo 4 gb nadhani inashusha na kwa saa moja! ninashangaa sana watu wanaosifu mtandao unaoshusha 4 gb kwa masaa 7-8

kwa matumizi ya simu huwa nanunua 50mb kwa 2000tsh voda.sasa wakubwa huwa napunjwa au?msaada.
 
Mkuu Max, what makes you to believe kwamba mpaka mwisho wa mwaka huu mambo yatakuwa safi zaidi?

Kwa ujumla bado internet ni bei ya juu kwa TZ kulinganisha na Kenya, naamini kufikia mwishoni mwa mwaka mambo yatakuwa safi zaidi ya inavyoonekana kwa juu.
 
Mkuu Max, what makes you to believe kwamba mpaka mwisho wa mwaka huu mambo yatakuwa safi zaidi?
Nina neno moja tu mkuu ambalo tumepewa na mhe. rais... AHADI!

Walisema nchi nzima itakuwa imetandazwa Optical Fibre na gharama zitashuka sana
 
Mkuu, nilifikiri kuna progress fulani umeithibitisha ambayo ndiyo inayokupa imani kumbe ni promise ya Mr President! Mkuu wengi wetu tulikuwa na matumaini makubwa sana na huo mkonga lakini yanaanza kufifia kutokana na maneno mengi yaliyosemwa kuhusu huu mkonga. But let's wait, time will tell!

Nina neno moja tu mkuu ambalo tumepewa na mhe. rais... AHADI!

Walisema nchi nzima itakuwa imetandazwa Optical Fibre na gharama zitashuka sana
 
guess-what.jpg


Kuna jamaa alikuwa anasifia Cheka Internet kwa speed ya ku-download files... Nampa snapshot ya hapa nilipo speed ikoje
 
Huku kwangu Airtel wanataka kunipa presure naweka bandle ya 15000 per week lakini hat file la 20KB linashindwa ku upload.

Zaidi zaidi speed in less than 2kb/s very low utadhani ujafungua kitu. Ukipiga customer care ndio kabisa ugonjwa wa moyo dakika 10 kungojeaa. Na ukimopata hana majibu . Ukipiga Tawi lao la Arusha ukichaa mtupu kuna dada pale sijui kwa nini alitoa.

Simu yake unaweza piga siku nzima asipokee. Sasa najiuliza kwa nini akupe simu yake aliopewa na ofisi na ukipiga hapokei. Yaani maudhi matupu nipeni ushauri wandugu nihamie wapi?. Yaani kuna siku natamini kuivunjilia mbali ka modem kao
 
Back
Top Bottom