Tanzania inazidi kupata heshima mapambano dhidi ya rushwa

mamayoyo1

JF-Expert Member
Jul 25, 2018
1,011
1,019

Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora), George Mkuchika amesema Tanzania inaendelea kupata heshima kubwa katika Jumuiya ya Kimataifa katika vita vya mapambano dhidi ya rushwa kutokana na mshikamano na nguvu ya pamoja iliyopo katika vyombo na taasisi zinazosimamia utawala bora nchini.

Akizungumza katika kongamano la siku maalum dhidi ya rushwa katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea Jijini Dar es Salaam leo Jumatano hii Waziri Mkuchika alisema utafiti uliofanywa na taasisi hizo zimesifu juhudi za zinazofanywa na Serikali ya awamu ya tano na kuitaja Tanzania kuwa ni nchi ya mfano katika vita vya mapambano dhidi ya rushwa.

Mkuchika aliasema taasisi hizo zikiwemo MO Ibrahim, Transparency International, APRM na taasisi nyingine kubwa duniani zinazosimamia masuala ya utawala bora zimefanya utafiti na kusifu juhudi kubwa zinazofanywa na serikali ya Tanzania chini ya Rais Dkt. John Magufuli katika mapambano dhidi ya rushwa ambapo tafiti mbalimbali zimeifanya Tanzania kushika nafasi ya pili nyuma ya nchi ya Rwanda.

Waziri Mkuchika alisema Serikali ya Awamu ya tano imeendelea kuweka mkazo na msukumo katika mapambano dhidi ya rushwa ambapo taasisi zote zinazosimamia masuala ya utawala bora zimekuwa zikiunganisha nguvu ya pamoja na kulifanya suala la rushwa sasa kuwa na nguvu na msukumo mpya wa mapambano katika jamii.

“Kwa sasa vyombo vyetu vyote serikalini si TAKUKURU pekee bali pia polisi, tiss (usalama wa taifa), Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ICAG) na vingine vyote, vimeendelea kuunga katika kusimamia masuala ya utawala bora na hili limeleta msukumo na hamasa mpya katika vita dhidi ya rushwa hapa nchini,” alisema Waziri Mkuchika.

Akizungumzia rushwa katika sekta ya viwanda na biashara, Waziri Mkuchika alisema Serikali imeendelea kuweka mikakati mbalimbali katika kupunguza tatizo hilo ambalo limekuwa likiathiri sekta binafsi ambayo imekuwa mshirika wa karibu wa serikali katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo nchini.

Kwa mujibu wa Waziri Mkuchika alisema rushwa katika sekta biashara imekuwa ikiathiri sana masuala ya uwekezaji wa kigeni, ambapo eneo lililonyesha kutawala kwa rushwa ni katika eneo la utoaji wa vibali na leseni kutoka katika taasisi na idara muhimu za serikalini na hivyo serikali imeendelea kulifanyia kazi ili kuhakikisha kuwa vikwazo hivyo vinaondolewa kwa wawekezaji na hivyo kuharakisha ukuaji wa uchumi.
 
Mfumo unaotawala dunia ni wa kibepari, principle ya mfumo huu ni kunyanganyana fursa za kujitajirisha ( debt someone and get credited)
Hivo rushwa haiwezi kuwa nje ya mfumo huu.

Hata hivo nimalizie kwakusema tuendelee kupunguza rushwa nchini Hadi dunia itakapo pata mfumo mahususi baada ya mfumo wa kibepari kupitwa na Wakati.
 
Back
Top Bottom