Tanzania inayotaka kujitegemea kiuchumi sasa inarudi zama za kutembeza bakuli ughaibuni

Kwa mara ya kwanza Magufuli ndani ya muda mfupi kututoa mstari wa nchi maskini mpaka nchi yenye uchumi wa kati , it's wonderful!, endelea na majungu kama ni mtaji
Walioutufikisha hapo ni JK ($480) na Mkapa ($330).
Magufuli ($100) mpira ulimgonga kalio akiwa kwenye mstari wa goli na mpira ukatinga wavuni wenyewe!
 
Kujitegemea kiuchumi sio kujitenga
Tungejitenga tusingefikia uchumi wa kati ,hatukujitenga kwa miaka 55 lakini tumeendelea kuwa nchi maskini , Magufuli miaka mitano tumeingia uchumi wa kati ,ficha upumbavu wako
 
Walioutufikisha hapo ni JK ($480) na Mkapa ($330).
Magufuli ($100) mpira ulimgonga kalio akiwa kwenye mstari wa goli na mpira ukatinga wavuni wenyewe!
Ndie aliytufikisha uchumi wa kati ndani ya miaka 5 tu toka mstari wa nchi maskini ,ficha upumbavut wako
 
Tulifikia vipi uchumi wa kati kama alifunga uchumi?,acheni ujinga basi
Hata hujui uchumi wa Kati maana yake ni Nini.

Halafu kumbuka watangulizi wake ndio waaliofanya kazi kubwa tangu 1995 ulipozindukiwa Vision 2025. Usiongee Kama kutoweo kilichokatwa kichwa. The fundamental micro and macro economic policies zilizowekwa na watangulizi wa mwenda zake. Kisha angalia alipotea wapi

Rudi kwenye mfano wangu wa Mimba, ilitoa mimba haikurudishi kuwa bikra Bali mwili unahesabu umezaa Mara ya Ila watoto mfu.

Sorry for my language lakini itakusaidia kuwaza kwa kushirikisha ubongo
 
Lini hamjatembeza bakuli mkuu... Kwenye mradi wa SGR tu ameombwa Mchina, akaombwa S.A akaombwa Turkey yani huku pesa alikuwa akisema ipo ila kila anayekuja anamwomba.

Hata ela ya corona iliombwa ikaletwa wakati tunasema hakuna corona.

Hatujawahi kuacha kutembeza bakuli yale ya tunajenga kwa pesa ya ndani ni maneno. Lile deni la taifa kuongezeka kwa kasi we unadhani limeongezeka ka sababu gani kama si kukopa kopa?
Hatuombi tunakopa na hakuna asiekopa dunia hii , America ni nchi tajiri lakini inakopa sembuse sisi?,tofautisha msaada na mkopo
 
Hatuombi tunakopa na hakuna asiekopa dunia hii , America ni nchi tajiri lakini inakopa sembuse sisi?,tofautisha msaada na mkopo
Basi tunaendelea kukopa hakuna cha tofauti hata kikwete alikopa, magufuli kakopa na mama samia kakopa.
 
Mleta Mada unaposema bunge lisikubali mikataba hii isainiwe gizani kama mkataba wa kuuza gas kenyaj

Je mkataba upi Kabla ya huu wa kuuza gas Kenya kuwahi kuwekwa hadharani? Tunasheria mbovu kupindukia hili suala la kusaini mikataba gizani wapinzani wa kweli wamelipigia Sana kelele lkn nyie vijana wa lumumba mkaja hapa na hadithi za abunuasi ohooo eti wametumwa na mabeberu . Sasa si Mnaona
 
Vita ya kiuchumi huwezi ipangua kwa kuwalamba watu miguu, kutembeza bakuli na ku compromise na kila kitu. Nchi yoyote yenye viongozi makini, huhakikisha wanatumia kila walichonacho +resources za nchi nyingine kujikwamua. Tulianza kupiga hatua, tukafika mpaka uchumi wa kati wa chini sio haba ila huko tuendako naona tunarudi tena kwenye group la nchi masikini kwa uzembe wa watawala wasio na maono. Inasikitisha Sana, endeleeni kupiga makofi na vigelegele.
Logical arguments ni muhimu wakati mwingine yaani unapigana vita vya uchumi na nani?kwa sababu nilichoona awamu tano ilichofanya ni ku initiated ni negotiations iliyozaa agreements kati ya makampuni haya ya uchimbaji Wa madini mpaka tukapata 16% stake na mgawo wa 50/50 economical benefits ,faida ya pili ni mabadiliko ya sheria ya madini ya mwaka 2017 ambayo inatamka madini yote kuwa chini wa umiliki wa serikali , Sasa Hapo kuna vita gani tena ?aproacha ilitumika kuyaleta hayo Makampuni kwenye meza ya mazangumzo ndiyo ilikuwa Harsh hakuna vita tuache kupotosha....
 
Rais wa JMT mama Samia yupo vizuri sana, anaongea ukweli na siyo kufichaficha@ anasema hali kwa sahizi siyo nzuri tujifunge mkanda ili baadaye panapo majariwa tutafurahi wenyewe@ hatumii nguvu kubwa, kwa maneno yake hata Kama una njaa unahisi kushiba tu. Mungu mbariki Rais wetu Samia S.H na zaidi ya yote ibariki Tanzania
 
Jakaya alikuwa na maneno matamu huku taifa linaambulia vyandarua kwenye safari zake, hopeless kabisa !
 
Dalili ya mvua ni mawingu, hali hii inatokana na matamshi na vision ya kiongozi aliyeko Madarakani.

Si kweli kwamba utaratibu wa uwekezaji nchini ni mbaya, nakataa hili kwa ushahidi kwa kupitia kauli ya mfanyabiashara maarufu hapa nchini Rostom Aziz aliyoitoa akiwa ziarani Kenya aliyeambatana na Rais Samia.

Alisema, mfano kuna kampuni 530 za Kenya zimewekeza nchini Tanzania,hebu lingania makampuni ya Tanzania nchini Kenya ,ambayo ni 30 tu, hivyo uwekezaji nchini kwetu ni rahisi kabisa, ispokuwa kuna machache ya kurekebisha kulingana na matakwa ya muda husika.

Hivyo sisi tumefungua fursa zaidi kuliko wenzetu, isipokuwa wenzetu wametugeuza sisi ndio raw materials producers wa viwanda vyao na wanahakikisha hatukui kwenye eneo la viwanda nchini. Hili Magufuli alilipinga kwa nguvu zote ndio maana akaja na sera ya viwanda.

Niseme tu hayati Magufuli alikuwa ni mtu ambaye Mara nyingi alifanya tafiti na kupata takwimu kabla ya Maamuzi magumu kutolewa, hii ilimfanya aheshimike sana duniani licha ya mahasimu wake kumshusha thamani.

Hayati Magufuli enzi ya utawala wake hakupenda kabisa ubabaishaji na hili lilimgharimu sana .ndicho kilichopelekea baadhi ya makampuni na wafanyabiashara matapeli kukimbia nchini, ambao Mama Samia kaenda kuwapigia Magoti.

Sasa naiona Tanzania inarudi ilipotoka, Tanzania inaenda kuwa nchi ya wachuuzi tena ,pamoja na raslimali lukuki ilizonazo,hii inaendana pia na kushuka kwa morali ya uwajibikaji wa baadhi ya viongozi wetu na kujiingiza kwenye rushwa.

Maneno aliyosema Rais Samia alipokutana na wafanyabiashara nchini Kenya ya kwamba anaenda kuifungua nchi. Je, ni lini nchi hii ilifunga mipaka yake?

Nafikiri angesema hakusanyi kodi tena wawekezaji ruksa kufanyabiashara nchini bila masharti tungrmuelewa na jambo hilo halipo duniani, kodi ndio msingi wa maendeleo, serikali kama haikusanyi kodi haina uhalali wa kutawala.

Mwisho kataja bandari ya Bagamoyo na eneo la viwanda, tusikubali uharaka haraka wake kusaini hii mikataba bila ya kujiridhisha, bunge lihakikishe mikataba hii haisainiwi gizani kama alivyofanya kwenye hili bomba la kuuza gasi nchini Kenya.

Mambo haya yalifanyika sana enzi za awamu ya nne, na yameligharimu sana taifa baada ya hayati Magufuli kutaka kuinasua nchi kwenye ujinga huu, naona Mama Samia anataka kupita kulekule kulipotugharimu. Vinginevyo nchi hii tunaenda kugawana mbao, Magufuli kaondoka kawatoa watanzania tongotongo machoni.
Kwanza kbs acha ujinga mkuu kiongoz alieko madarakani ndo kitu gan? Mtaje Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania. Suala la kufungua nchi kibiashara kwanza ww hujui chochote mpaka upinge, yy yupo jikoni anajua in and out. Scenario ya kwamba NCHI inarudishwa kama awamu ya nne huo ni ujinga haiwezekan muaminishe watu kua kiongoz bora ni aliepita. Awamu yake ishapita muache Rais afanye kaz yake, kama vp hama NCHI au nenda kale ulipopeleka mboga. OVER!!
 
Kwani huyu aliyepo anarekebisha kitu gani kama sio kurejesha kile ambacho kilikuwa kinalalamikiwa awamu zilizopita sasa anazirejesha kwa mbwembwe huku akiwazodoa wale wale waliosababisha yeye na hayati wawape kura?

Kauli ya kwamba 'mimi na JPM ni kitu kimoja' tayari imemuanika kwenye taswira ambayo ama aliilenga kwa makusudi au kutokujua matokeo ya kauli.

Ni kweli walikuwa ni kitu kimoja lakini kwa matendo walikuwa hawaivi chungu kimoja, hizi ni hisabati ndogo za upili kuzitanzua.

Nchi nzima mmezunguka mnanadi ilani na kuwapa matumaini kwamba mtatekeleza kwa kutumia rasilimali zetu lakini kuanguka kwa nguzo kaya mnakimbilia kutafuta wawekezaji ambao hawana manufaa yoyote kwa nchi na wananchi wake, mnatembeza bakuli la misaada na hisani kutoka nje. Mkijinadi kwamba hamuwezi kuendelea kuwa kisiwa tena, je, kabla mlikuwa kisiwani? Kwanini wasingejiuzulu ili haya yanayoendelea yaungwe mkono pasipo kutupia lawama kwa mtu mwingine?

Kama Busara na Hekima kutoka kwa Mungu aliye hai hazitazingatiwa na kukumbatia matakwa ya dunia historia ya Tanzania itaendelea kutotabirika hivyo imani kupotea jumla
mkuu Magufuli alidumaza sekta binafsi na uwekezaji nchini, kwa kodi kubwa na sera zisizotabirika hadi wafanyabishara kukimbia, kuna mazuri aliyafanya ndio kama ujenxzi wa miundombinu na Samia kasema ataendeleza. Ilani itatekelezwa na Samia ana namna yake ya kuitekeleza, tatizo sio ilani,
Na je kwani Samia katembeza bakuli? na je Magufuli alikuwa haombi msaada? alikuwa hapokei msaada?

Na tangia lini waweklezaji wakawa wabaya kwa nchi? nchi kama Marfekani, Uingereza zenyewe zimepiga hatua kutokana na mitaji ya watu wa nje kuwekeza huko, Tanzania ndio isihitaji wawekezaji?

na je Magufuli nae alipokuwa akimpond Kikwete wakati yeye alikuwa sehemu ya Serikali yake ni kwa nini na yeye asijiuzulu?
 
Dalili ya mvua ni mawingu, hali hii inatokana na matamshi na vision ya kiongozi aliyeko Madarakani.

Si kweli kwamba utaratibu wa uwekezaji nchini ni mbaya, nakataa hili kwa ushahidi kwa kupitia kauli ya mfanyabiashara maarufu hapa nchini Rostom Aziz aliyoitoa akiwa ziarani Kenya aliyeambatana na Rais Samia.

Alisema, mfano kuna kampuni 530 za Kenya zimewekeza nchini Tanzania,hebu lingania makampuni ya Tanzania nchini Kenya ,ambayo ni 30 tu, hivyo uwekezaji nchini kwetu ni rahisi kabisa, ispokuwa kuna machache ya kurekebisha kulingana na matakwa ya muda husika.

Hivyo sisi tumefungua fursa zaidi kuliko wenzetu, isipokuwa wenzetu wametugeuza sisi ndio raw materials producers wa viwanda vyao na wanahakikisha hatukui kwenye eneo la viwanda nchini. Hili Magufuli alilipinga kwa nguvu zote ndio maana akaja na sera ya viwanda.

Niseme tu hayati Magufuli alikuwa ni mtu ambaye Mara nyingi alifanya tafiti na kupata takwimu kabla ya Maamuzi magumu kutolewa, hii ilimfanya aheshimike sana duniani licha ya mahasimu wake kumshusha thamani.

Hayati Magufuli enzi ya utawala wake hakupenda kabisa ubabaishaji na hili lilimgharimu sana .ndicho kilichopelekea baadhi ya makampuni na wafanyabiashara matapeli kukimbia nchini, ambao Mama Samia kaenda kuwapigia Magoti.

Sasa naiona Tanzania inarudi ilipotoka, Tanzania inaenda kuwa nchi ya wachuuzi tena ,pamoja na raslimali lukuki ilizonazo,hii inaendana pia na kushuka kwa morali ya uwajibikaji wa baadhi ya viongozi wetu na kujiingiza kwenye rushwa.

Maneno aliyosema Rais Samia alipokutana na wafanyabiashara nchini Kenya ya kwamba anaenda kuifungua nchi. Je, ni lini nchi hii ilifunga mipaka yake?

Nafikiri angesema hakusanyi kodi tena wawekezaji ruksa kufanyabiashara nchini bila masharti tungrmuelewa na jambo hilo halipo duniani, kodi ndio msingi wa maendeleo, serikali kama haikusanyi kodi haina uhalali wa kutawala.

Mwisho kataja bandari ya Bagamoyo na eneo la viwanda, tusikubali uharaka haraka wake kusaini hii mikataba bila ya kujiridhisha, bunge lihakikishe mikataba hii haisainiwi gizani kama alivyofanya kwenye hili bomba la kuuza gasi nchini Kenya.

Mambo haya yalifanyika sana enzi za awamu ya nne, na yameligharimu sana taifa baada ya hayati Magufuli kutaka kuinasua nchi kwenye ujinga huu, naona Mama Samia anataka kupita kulekule kulipotugharimu. Vinginevyo nchi hii tunaenda kugawana mbao, Magufuli kaondoka kawatoa watanzania tongotongo machoni.
sukuma GANG mtapata taabu sana. mnapaswa mtambue mtu wetu kaenda zake na chuki na ulaghai wake aliokuwa anawaaminisha kuwa ni mzalendo sijui mpenda wanyonge
 
hii
mkuu Magufuli alidumaza sekta binafsi na uwekezaji nchini, kwa kodi kubwa na sera zisizotabirika hadi wafanyabishara kukimbia, kuna mazuri aliyafanya ndio kama ujenxzi wa miundombinu na Samia kasema ataendeleza. Ilani itatekelezwa na Samia ana namna yake ya kuitekeleza, tatizo sio ilani,
Na je kwani Samia katembeza bakuli? na je Magufuli alikuwa haombi msaada? alikuwa hapokei msaada?

Na tangia lini waweklezaji wakawa wabaya kwa nchi? nchi kama Marfekani, Uingereza zenyewe zimepiga hatua kutokana na mitaji ya watu wa nje kuwekeza huko, Tanzania ndio isihitaji wawekezaji?

na je Magufuli nae alipokuwa akimpond Kikwete wakati yeye alikuwa sehemu ya Serikali yake ni kwa nini na yeye asijiuzulu?
na huu ni kweli. jamaa kauwa uchumi kwa kuendesha nchi kimachinga kama sakosi ya babake
 
Kweli wewe ni msukule wa Jiwe! Unajua mwendazake wenu alikuta deni la nje shs ngapi na ameondoka kukiwa shs ngapi?

Kuna Rais katembeza bakuli kuomba na kukopa nje Kama huyo Mwendazake wenu?

Yaaani bado mnaamini hiki ni kipindi cha propaganda? Sikilizeni niwaambie, Hakuna propaganda zitafanikiwa katika Awamu ya 6. Nchi imerudi kwa watanzania halisi wanaojua waiendesheje. Nyie wa Burundi rudini kwenu
Kwa hiyo watanzania halisi wanaanzia mashariki kuelekea linakozania jua, uenda kweli!
 
Back
Top Bottom