Tanzania inayotaka kujitegemea kiuchumi sasa inarudi zama za kutembeza bakuli ughaibuni

thetallest

JF-Expert Member
Oct 21, 2017
8,256
9,085
Dalili ya mvua ni mawingu, hali hii inatokana na matamshi na vision ya kiongozi aliyeko Madarakani.

Si kweli kwamba utaratibu wa uwekezaji nchini ni mbaya, nakataa hili kwa ushahidi kwa kupitia kauli ya mfanyabiashara maarufu hapa nchini Rostom Aziz aliyoitoa akiwa ziarani Kenya aliyeambatana na Rais Samia.

Alisema, mfano kuna kampuni 530 za Kenya zimewekeza nchini Tanzania,hebu lingania makampuni ya Tanzania nchini Kenya ,ambayo ni 30 tu, hivyo uwekezaji nchini kwetu ni rahisi kabisa, ispokuwa kuna machache ya kurekebisha kulingana na matakwa ya muda husika.

Hivyo sisi tumefungua fursa zaidi kuliko wenzetu, isipokuwa wenzetu wametugeuza sisi ndio raw materials producers wa viwanda vyao na wanahakikisha hatukui kwenye eneo la viwanda nchini. Hili Magufuli alilipinga kwa nguvu zote ndio maana akaja na sera ya viwanda.

Niseme tu hayati Magufuli alikuwa ni mtu ambaye Mara nyingi alifanya tafiti na kupata takwimu kabla ya Maamuzi magumu kutolewa, hii ilimfanya aheshimike sana duniani licha ya mahasimu wake kumshusha thamani.

Hayati Magufuli enzi ya utawala wake hakupenda kabisa ubabaishaji na hili lilimgharimu sana .ndicho kilichopelekea baadhi ya makampuni na wafanyabiashara matapeli kukimbia nchini, ambao Mama Samia kaenda kuwapigia Magoti.

Sasa naiona Tanzania inarudi ilipotoka, Tanzania inaenda kuwa nchi ya wachuuzi tena ,pamoja na raslimali lukuki ilizonazo,hii inaendana pia na kushuka kwa morali ya uwajibikaji wa baadhi ya viongozi wetu na kujiingiza kwenye rushwa.

Maneno aliyosema Rais Samia alipokutana na wafanyabiashara nchini Kenya ya kwamba anaenda kuifungua nchi. Je, ni lini nchi hii ilifunga mipaka yake?

Nafikiri angesema hakusanyi kodi tena wawekezaji ruksa kufanyabiashara nchini bila masharti tungrmuelewa na jambo hilo halipo duniani, kodi ndio msingi wa maendeleo, serikali kama haikusanyi kodi haina uhalali wa kutawala.

Mwisho kataja bandari ya Bagamoyo na eneo la viwanda, tusikubali uharaka haraka wake kusaini hii mikataba bila ya kujiridhisha, bunge lihakikishe mikataba hii haisainiwi gizani kama alivyofanya kwenye hili bomba la kuuza gasi nchini Kenya.

Mambo haya yalifanyika sana enzi za awamu ya nne, na yameligharimu sana taifa baada ya hayati Magufuli kutaka kuinasua nchi kwenye ujinga huu, naona Mama Samia anataka kupita kulekule kulipotugharimu. Vinginevyo nchi hii tunaenda kugawana mbao, Magufuli kaondoka kawatoa watanzania tongotongo machoni.
 
Tunawajua kundi lenu loote mnaojitahidi kumkwamisha mama Samia.

Mnajitahidi kubeza kila anachokifanya.

Hata hivyo hamtaweza maana tayari mshajulikana.

Niwashauri tu kuwa mnatakiwa mkubali kuwa mama Samia ndiye Rais wa JMT.
 
Mama alikuwa makamu wa Rais aliyeenda zake, yeye na wewe nani yuko kwenye nafasi ya kujua kuwa nchi ilikuwa imefungwa au haijafungwa? Tumuamini nani zaidi kati yako wewe na Mama yetu?

Mitano tena kwa Mama Samia Suluhu Hassan
 
Kwa dunia ya leo bila kuvutia uwekezaji sahau maendeleo. Kimsingi hakuna taifa lolote duniani linaloweza kupiga hatua kama hakuna muingiliano wa kiuchumi kwa mashirikiano na nchi zingine na hii ni kwasababu tunaishi kwa kutegemeana. Sasa nyie sijui ni nani aliwaaminisha kuwa nchi inaweza kupiga hatua ikibaki yenyewe.
 
Huyo mwendazake wako ndani ya miaka mi5 aliongoza kibabe, pamoja alizuia hela za wafanyabiashara wakubwa na kwenda kuzijengea chato na kujitapa kua yeye nitajili na hana shida, mwisho wasiku anasema tunakopa na hatusemi tunakopa wapi eni la taifa limepaa kuliko vindi vipindi vyoote kuwahi kutoke.

Mwisho wasiku presha inapanda na kuitwa mwendazake.

Acha kuleta porojo mkuu.hali ilikua inaendea kubaya. Walionufaika na upuuz ule ni POLEPOLE NA KATIBU WAKE LABDA. Maana ndio walikua watetezi wakuu wa mwendazake.
 
Kweli wewe ni msukule wa Jiwe! Unajua mwendazake wenu alikuta deni la nje shs ngapi na ameondoka kukiwa shs ngapi?

Kuna Rais katembeza bakuli kuomba na kukopa nje Kama huyo Mwendazake wenu?

Yaaani bado mnaamini hiki ni kipindi cha propaganda? Sikilizeni niwaambie, Hakuna propaganda zitafanikiwa katika Awamu ya 6. Nchi imerudi kwa watanzania halisi wanaojua waiendesheje. Nyie wa Burundi rudini kwenu
 
Mwendazake ni mkataba gani alipeleka bungeni. Mikataba ya vivuko fake iko wapi. Mumrudishe basi akalinde raslimali zenu.

Sasa kama unakiri sera za mwendazake zilikimbiza wawekezaji, kwanini umlaumu anayewarudisha? Sukuma gang mmepatikana safari hii. Hakuna kupumua.
 
Alisema, mfano kuna kampuni 530 za Kenya zimewekeza nchini Tanzania kulingana na Tanzania nchini Kenya ambazo ni 30 tu, hivyo uwekezaji nchini ni rahisi kabisa, ispokuwa kuna machache ya kurekebisha kulingana na matakwa ya muda husika.

Hivyo sisi tumefungua fursa zaidi kuliko wenzetu, isipokuwa wenzetu wametugeuza sisi ndio raw materials producers wa viwanda vyao na wanahakikisha hatukui kwenye eneo la viwanda nchini. Hili Magufuli alilipinga kwa nguvu zote ndio maana akaja na sera ya viwanda.
Wachaga wana biashara zao karibu kila mahali ndani ya Tanzania, including vijijini!

Kinyume chake, unakuta jamii zingine hawana biashara yoyote ya kueleweka hata kwenye maeneo yao wenyewe!!! Na hata wale wenye biashara, unakuta wapo maeneo yao tu, na wanashindwa kuvuka hata wilaya ya jirani hata kama wana uwezo huo kibiashara!!

Je, unataka kusema Tanzania inatoa fursa kwa Wachaga peke yake na sio kwa jamii zingine na ndo maana wao utawakuta karibu kila sehemu?!
 
Kuna biashara nyingi zilifungwa wakati wa awamu ya tano sababu ni namna kodi ilivyokusanywa kibabe. Makusanyo kuwa mengi wakati uhalisia ni kifo cha biashara ni kitu ambacho hakingeweza kuwa na tija ya kudumu.

Rais Samia amekuwa muungwana kuwa na uthubutu wa kusema hadharani juu ya uonevu waliokutana nao wafanyabiashara na siku ile ikulu ni kama vile alikuwa anawaangukia wafanyabiashara.

Huwezi kushindana na mfanyabiashara mwenye mtaji wa mamilioni ya pesa halafu waajiriwa wake wasiwe ni wa kwanza kuumia iwapo ataamua kutoipa ushirikiano serikali.

Kukusanya kodi hakukwepeki lakini maarifa ya hali ya juu ya ukusanyaji ndio silaha ya uwepo wa amani kati ya mkusanyaji na mlipaji.

Na ni ngumu sana kujitegemea katika dunia ambayo mwenye teknolojia ndiye mtawala mwenye ushawishi wa kuanzia kwa mtu mmoja mmoja mpaka kwa viongozi wa serikali.

Huwezi kuishi kama kisiwa, kwa namna moja au nyingine utawahitaji tu hao wenye teknolojia ili uingie nao ubia.
 
Wachaga wana biashara zao karibu kila mahali ndani ya Tanzania, including vijijini!

Kinyume chake, unakuta jamii zingine hawana biashara yoyote ya kueleweka hata kwenye maeneo yao wenyewe!!! Na hata wale wenye biashara, unakuta wapo maeneo yao tu, na wanashindwa kuvuka hata wilaya ya jirani hata kama wana uwezo huo kibiashara!!

Je, unataka kusema Tanzania inatoa fursa kwa Wachaga peke yake na sio kwa jamii zingine?
Mtetezi wa mama Samia, mkosoaji wa Magufuli. Rangi halisi haijifichagi sheikh.
 
Mtetezi wa mama Samia, mkosoaji wa Magufuli. Rangi halisi haijifichagi sheikh.
NONSENSE... Jiwe lilikuwa linapingwa na kila mwenye akili timamu kwa sababu lilikuwa Katili, Liuaji, Dikteta, na sifa zingine zote za kishetani!

Ingawaje hakuna alipotajwa Samia, bado ulitaka nimkosoe Samia kwa lipi?!

Ulitaka nimkosoe kwa kuwataka TRA waache kutumia nguvu badala ya akili?

Ulitaka nimkosoe kwa kutaka kufungua uhusiano wa kibiashara na taifa la jirani?

Ulitaka nimkosoe kwa kuzifungua akaunti za Watetezi wa Haki za Binadamu ambazo zilifungwa na Shetani Jiwe

Hivi una akili kweli wewe?!

FYI, hata huyo Jiwe alipoingia madarakani nilikuwa namuunga mkono hadi pale alipoanza kuonesha udhalimu wake!!!

Ulivyo mpumbavu unadhani kila mmoja anaongozwa na mihemuko ya kidini! Na hiyo inadhihirisha unalitetea lile dhalimu kwa kuongozwa na udini... VERY STUPID!

Nikujuze tu kwamba, Jiwe alikuwa anapingwa na Wakristo na Waislamu!!! SSH at least for now, anaungwa mkono na Wakristo na Waislamu!!

Endelea tu kutapatapa na udini wako huo!!
 
Jiwe alikua anajua fedha za ndani ni kuchukua hela za wastaafu kule kwny mifuko ya kijamii,kubambikizia watu makosa ya uhujumu uchumi ili awanyanganye pesa zao etc

Utamsikia tu nchi hii ina mahera mengiiiiiiiiiiii.
 
Vita ya kiuchumi huwezi ipangua kwa kuwalamba watu miguu, kutembeza bakuli na ku compromise na kila kitu. Nchi yoyote yenye viongozi makini, huhakikisha wanatumia kila walichonacho +resources za nchi nyingine kujikwamua. Tulianza kupiga hatua, tukafika mpaka uchumi wa kati wa chini sio haba ila huko tuendako naona tunarudi tena kwenye group la nchi masikini kwa uzembe wa watawala wasio na maono. Inasikitisha Sana, endeleeni kupiga makofi na vigelegele.
 
Back
Top Bottom