Tanzania inatumia teknolojia ya miaka 21 iliyopita katika Telecommunication Industry

Anonymous

Senior Member
Feb 3, 2006
125
321
Habari 👋🏾

Kwa takribani siku tano nimekuwa katika mazungumzo na Dr. Dan Havlick, Bw. Medenne Stephenson na Prof. Sara Ramirez ambao ni wakurugenzi watendaji wa kikanda wanaosimamia maslahi ya makampuni ya mawasiliano ya AT&T, T-Mobile na Verizon kwa Kansas City, Toronto na jimbo la Bavaria, Ujerumani.

Mazungumzo yetu yalilenga kufahamu utendaji, teknolojia, huduma mbalimbali, teknolojia ya 5G na kuangalia fursa za uwekezaji katika sekta ya Telecommunications kwa mataifa ya Tanzania, Marekani, Kanada na Ujerumani.

Mazungumzo yetu yalikuwa ni yenye shauku kufahamu utendaji wa makampuni yatoayo huduma ya mawasiliano kwa simu, na idadi yake kwa mataifa hayo. Viongozi hawa walifurahishwa sana kusikia Tanzania inaowatoa huduma wengi ambao ni Vodacom Tanzania, Tigo Tanzania, Airtel Tanzania, Halotel, Zantel, Smart, Smile na TTCL huku wakiamini kwamba mtumiaji wa mwisho anachagua huduma aitakayo na kusikitishwa na ufinyu wa mitandao katika mataifa yao.

Kadri tulivyozidi kujadili masuala mbalimbali walishangazwa na mfumo wa bundles (Vifurushi) na kusema hiyo ikiwezesha kutokea katika mataifa yao watumiaji watanufaika pakubwa. Pamoja na kushangazwa kwa utumiwaji wa bundles, walisikitishwa kwa ukosefu wa WiFi katika taifa.

Jambo kubwa lilitokea ni baada ya kufanya utafiti mdogo kupitia wakati wa mazungumzo na kugundua teknolojia inayotumika hii leo na taifa zima katika Telecommunication Industry ni ndio iliyotumika miaka 21 nyuma kwa Marekani, Ujerumani na Canada. Walishangazwa na kujiuliza kama taifa linaweza vipi?

Hali hii iliibua swali endapo Tanzania na Marekani wanayo mahusiano na kuuliza imekuwaje Marekani imeshindwa kupeleka teknolojia Tanzania na kufanya uwekezaji?

Sasa hapa najiuliza maswali mengi lakini moja wapo ni, Je uliwahi kufahamu Tanzania inatumia teknolojia ya miaka 21 iliyopita katika simu?
 
Kule mwanzo umetiririka vizuri na umeeleweka ila hapa naona kama mawasiliano yamekatakata sijakuelewa vema, kama hutajali paelezee tena kiundani zaidi
 
Angalia tu smartphones zimeanza kusambaa lini ndio utajua tofauti ya huduma za 21yrs ago na sasa.
Nilidhani huduma za telecommunication ndio unasema. Kwa upande wa Smartphones tumefika mbali ila yote mwanzilishi ni hao Westy people. So tech walioyoitumia wakati wa 2000 ni tofauti na wanayotumia sahi.
 
Hebu ichambue hiyo teknolojia ya miaka 21 iliyopita kwa undani kidogo mkuu.
Binafsi sifahamu maana waliomba details za bandwidths katika mitandao inayoongoza baada ya muda wa kuipekuwa kampuni ya Vodacom Tanzania ndio walikuja na kauli hiyo.

Wataalamu wa katika Telecommunications ndio wakutusaidia kutokana na swali langu la mwisho.
 
Hujaelewa nini katika hizo paragraph?
Kadri tulivyozidi kujadili masuala mbalimbali walishangazwa na mfumo wa bundles (Vifurushi) na kusema hiyo ikiwezesha kutokea katika mataifa yao watumiaji watanufaika pakubwa. Pamoja na kushangazwa kwa utumiwaji wa bundles, walisikitishwa kwa ukosefu wa WiFi katika taifa.
 
walikuona upoupo hata kuhoji vitu vyenye logic huwezi wakaona bora wakulishe upumbavu ili ukahadithie wajinga wenzako. Kwa kifupi waliona unawapotezea muda wakaona wakujibu pumba uondoke
 
Kadri tulivyozidi kujadili masuala mbalimbali walishangazwa na mfumo wa bundles (Vifurushi) na kusema hiyo ikiwezesha kutokea katika mataifa yao watumiaji watanufaika pakubwa. Pamoja na kushangazwa kwa utumiwaji wa bundles, walisikitishwa kwa ukosefu wa WiFi katika taifa.
Sio kukosa Wi-Fi kabisa ila kuwa haipatikani kila pahali nchini. Mfano nchi nyingi za ughaibuni Wi-Fi iko karibu 95% ya nchi na kuna zile pocket WiFi pia bei rahisi kulingana na hali ya maisha yao. Na speed ipo nzuri tu. Kumbuka pia kuna sehemu wifi bure kabisa nchi hizo sana sana, mashuleni, kwenye transport systems nk. Sasa tofauti yetu na wao ndipo inapoingilia.
 
Kadri tulivyozidi kujadili masuala mbalimbali walishangazwa na mfumo wa bundles (Vifurushi) na kusema hiyo ikiwezesha kutokea katika mataifa yao watumiaji watanufaika pakubwa. Pamoja na kushangazwa kwa utumiwaji wa bundles, walisikitishwa kwa ukosefu wa WiFi katika taifa.
Nadhani public wifi ,huduma hii haipo kabisa miji yetu.
 
Back
Top Bottom