Tanzania inamwitaji Mwaisapile (mpya). Kwa kweli.

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,268
33,040
“Tunamwitaji atakayeoteshwa kuhusu ‘dawa’ ya kumaliza matakataka mijini. Na mwingine aoteshwe ‘dawa’ ya kuwaondoa wapiga debe mijini. Mwingine aoteshwe ‘dawa’ ya kuwaondoa wafanyabiashara wanaopanga bidhaa mabarazani na njiani.”
Hivyo ndivyo ilikuwa ikisema “status update” yangu kwenye facebook. Nilisukumwa kuandika huo ujumbe kwa sababu ya

mambo ambayo yamekuwa yakitokea katika nchi yetu kwa siku za karibuni.

Tumekuwa tukisikia kila kukicha juu ya watu ambao wanadai kuwa “wameoteshwa” na mungu (lower case m) dawa ya magonjwa

sugu yanayowakabili waTZ. Mambo yalianzia Loliondo au ‘kwa Babu’ kama wengi wetu tunavyopenda kupaita. Ilianza kwa mchungaji mstaafu wa KKKT, Ambilikile Mwaisapile, “kuoteshwa” dawa ya magonjwa sugu.


Baada ya hapo umefuata utitiri wa watu ambao kila kukicha wamekuwa wakiibuka na kudai kwamba “wameoteshwa” juu ya dawa ambayo ‘hakuna ugonjwa ambao haitibu’ — ukiamini. Ukiamini nini? Ni swali ambalo watu, hata waliotumia hiyo dawa,

hawawezi kukwambia. Ukimwamini Mungu? Ukiliamini neno la Mungu? Ukiiamini dawa? Ukiamini kwamba dawa ile inaponya? Ukimwamini mtoa dawa? Ukiuamini mrigariga? UKIAMINI NINI?


Nilishasema hapo awali na ninarudia kusema: jamii ya Watanzania inayo ‘magonjwa’ sugu mengi ukiachilia ya kisukari, UKIMWI, kansa, stroke, shinikizo la damu, presha, vidonda vya tumbo n.k. Tunayo ‘magonjwa’ ambayo yanahitaji ‘tiba’ isiyo ya kawaida. Je nani atathubutu kujitokeza akadai kuwa “ameoteshwa” kuyatibu haya magonjwa?


Ni nani ataoteshwa ‘dawa’ ya foleni mijini? Nani ataoteshwa ‘dawa’ ya ukosefu wa maji vijijini? Nani ataoteshwa ‘dawa’ ya kukatikakatika kwa umeme? Nani ataoteshwa ‘dawa’ ya uchafu unaozagaa kila kona katika miji na majiji yetu? Nani ataoteshwa ‘dawa’ ya kupanda bei kwa bidhaa kila kukicha? Nani ataoteshwa ‘dawa’ ya umaskini? Nani ataoteshwa ‘dawa’ ya mikataba mibovu? Nani? Nani?


Ila sasa, Je, akijitokeza atakayeoteshwa ‘dawa’ ya magonjwa haya TUTAMSHABIKIA? Je, tutapanga foleni kumpa sapoti? Je, tutajipanga nyuma yake na kumwambia, “tuna imani na wewe”? Je, tutaamini?


Rafiki yangu mmoja akaniambia na hapa namnukuu: “Magufuli alioteshwa dawa ya kuondoa kero za barabara mbovu. Je, uliona kilichompata?” Sote tunajua kilichompata. Hatukumwamini. Hatukuamini!
 
Hoja yako na mawazo yako yamekaa kiutaniutani lakini ndani kuna ukweli uliojificha.Iko hivi Mzizimkavu. Binadamu, hasa watanzania wametawaliwa na 'unafsi'. Likitokea jambo lenye maslahi kwa nafsi ya mtu mmojammoja,watu wataunga foleni yenye urefu toka Mwanza hadi Maputo kufaidi hilo jambo.Chukua huo mfano wako wa Babu wa Loliondo. Watu, kuponyesha nafsi zao walipiga kambi kule Samunge kwa wiki kadhaa licha ya matatizo ya mazingira duni ya hicho kijiji ili wanywe kikombe cha kuponyesha magonjwa sugu.Na waliamini sana kwamba dawa hiyo ni kiboko. Lakini akijitokeza mtu akasema ameoteshwa dawa ya kuondoa ufisadi kwa mfano, itakula kwake maana atataniwa na kubezwa sana. Kisa? Watu wanafikiri ufisadi ni jambo linalohusu ustawi wa jumuiya na siyo nafsi ya mtu mmoja mmoja. Naomba nimalizie hapo kwa sababu atakuja Nyani Ngabu na kusema maelezo haya hayana aya wala nukta na koma.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom