TANZANIA inakutegemea wewe mzalendo wa kweli

TANZANIA inakutegemea wewe mzalendo wa kweli

canular

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2018
Posts
1,083
Reaction score
1,305
Watumishi wote mnao husika na Serikali moja kwa moja
TAKUKURU Tujitafakali
Polisi Tujitafakal
JWTZ Tujitafakali
Magereza Tujitafakali
Usalama wa Taifa Tujitafakali
Watanzania TUJITAfakari! wote kwa ujumla wetu watanzania
Leo mali za nchi zinaporwa kwa dharau na ujasiri wa hali ya juu. Ufisadi na wizi umegeuka utamaduni. Viongozi na watendaji wakuu mnatazama kwa mbali kana kwamba hamhusiki na dhambi hizi. Mnajua kinachoendelea, mnashuhudia, lakini hamchukui hatua. Mnataka kuwa mabubu mpaka lini, mkiwa mnatajwa kama sehemu ya tatizo?
Ikiwa taasisi zote za usalama na ulinzi mnashindwa kuchukua hatua, nani atasimama? Kama mnashindwa kuchunguza, kuuliza na kudhibiti wizi huu wa hadharani, nani atasimama kwa ajili ya nchi hii? Au mmekubali kufanywa makondoo, kupoteza sauti, msimamo na heshima mbele ya wachache wanaotafuna nchi kama wanyama pori?
Tanzania ni nchi ya watu wenye heshima, moyo, na uzalendo. Mbona leo hakuna mwenye uchungu na mali za taifa hili? Mbona hakuna anayepaza sauti, wala kufa kwa ajili ya haki? Tumekufa ganzi na kuishi kwa hofu — mpaka lini?
Kama mko tayari kuuzwa, kama mpo tayari kukaa kimya — basi historia itawahukumu! Wanaopora mali, wanaojenga utajiri wa familia zao kupitia damu na jasho la wananchi, wajue siku yao inakuja!
Ewe nchi yangu, Tanzania — nimesimama kupaza sauti kwa uchungu na hasira. Wazalendo wa kweli msikae kimya! Ni wakati wa kuchukua hatua, ni wakati wa kuhoji, ni wakati wa kukemea waziwazi. Afadhali lawama ya wazi kuliko unafiki wa kimya.
Nchi hii si mali ya mtu, si mali ya kundi, ni yetu sote. Hakuna atakayeendelea kutukandamiza bila sisi kusimama. Chukua hatua sasa! Isemee TANZANIA inakutegemea wewe mzalendo mpenda Haki huinua Taifa tueni na uchungu na nchi yetu watanzania tuamkeni
 
Siasa ni mbaya kila siku mahubiri ya uzalendo ilihali mataperi, mafisadi, majambazi na wahalibifu wa nchi yetu wote mnawajua, maana yake ni nini kama siyo kupakwa mafuta kwa mgongo wa chupa, hii nchi ya ajabu sana.
 
29/10/2025 tutokeni kwa wingi tuingieni barabarani kupaza sauti zetu kuiondoa hii serikali ya kifisadi na kijambazi Bora kufa kuliko kuishi kuliko kuendelea huyashuhudia haya maovu ya wenye madaraka
 
29/10/2025 tutokeni kwa wingi tuingieni barabarani kupaza sauti zetu kuiondoa hii serikali ya kifisadi na kijambazi Bora kufa kuliko kuishi kuliko kuendelea huyashuhudia haya maovu ya wenye madaraka
Safi kabisa tutakuweka mstari wa mbele ili ukivunjwa miguu uwe ushahidi wa vizazi vyetu kwamba tulipigania haki kwa jasho na damu.
 
Back
Top Bottom