Tanzania inahitaji sera ya Malezi

Gamba la Nyoka

JF-Expert Member
May 1, 2007
7,023
9,284
Katika taifa masikini kama la kwetu, ni dhahiri kwamba lazima mikakati kabambe na juhudi maridhawa vifanywe ili kutuwezezesha kupiga kasi ya kutosha katika kuondokana na matatizo lukuki tuliyokuwa nayo.

Miongoni mwa juhudi zenyewe ni kutafuta na kujipatia maarifa mbali mbali ya yale yatakayotufaa katika nyanja mbali mbali za maisha yetu.

Lakini sehemu mojawapo ya kusambaza maarifa hayo ni kupitia Malezi ya watoto wetu."

Kwa dunia ya leo ambayo maarifa yamejaa tele ,kumbe tatizo haswa si maarifa yenyewe bali tatizo ni namna ya kuyasambaza maarifa hayo.

Sisi kama jamii tuna utaratibu gani wa kueleweka wa kusambaza maarifa hayo?. je elimu ya darasani pekee yatosha kupima kiwango cha mzazi au mlezi kumpa mwanae maarifa.

Kwa mujibu wa maswali hayo kiufupi ninahoji iko wapi sera ya malezi ya watoto wetu?

Je, Tangu mtoto anapoanza kutambaa, kutembea , kuzungumza n.k upo mwongozo kwa mzazi wa kitanzania bila kujali yeye ni tajiri au masikini kuufuata muongozo huo ili kumpa mtoto maarifa yanayoendana na umri wake?

Je sisi kama taifa tuna viwango tumeviweka kwamba mtoto akiwa na umri kadhaa basi atleast ajue hiki na kile, na akifikisha umri kadhaa at least ajue hiki na kile?

Kwa sababu mimi ninavyoona hatuwezi kukuza IQ ya mtoto wa Kitanzinia bila malezi bora yenye kuendana na mpangilio maridhawa wa kumjaza uelewa mtoto husika.

Kutokana na sababu hiyo, mimi napendekeza serikali ifanye yafuatayo:

1. Iandae mwongozo wa malezi kwa wazazi. Kila mzazi apewe mwongozo huo, na kila mzazi ajitahidi kuufuata huo muongozo. Akiweza kuwa mbunifu zaidi ya hapo, basi nayo ni kheri pia. Lakini minimum kila mzazi aufuate muongozo huo.

2. Mwongozo huo ueleze wazi na kwa ufasaha mkubwa mzazi katika kila hatua ya ukuaji wa mtoto afanye vipi ili kukuza akili ya mtoto. Na ueleze wazi kwamba katika umri fulani wa mtoto, mzazi ajitahidi mtoto wake ajue vitu kadhaa wa kadhaa na kadhaa.

Ni nini faida kubwa ya mwongozo huu? Faida kubwa itakuwa ni kukuza IQ ya mtoto wa Kitanzania.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom