SoC04 Wazazi/ walezi wengi hawana elimu ya malezi, tuwape elimu ili kutengeneza jamii bora ya baadaye

Tanzania Tuitakayo competition threads
May 5, 2024
20
9
UTANGULIZI
Wazazi au walezi wengi wa kitanzania hawana elimu bora ya malezi jambo linalopelekea kutokuzalisha vijana walio bora kwenye jamii wenye kuleta matokeo chanya kwa taifa na hatimae kuzalisha watoto wa mtaani.

Kuna tofauti kubwa kati ya kumhudumia mtoto na kumlea mtoto, hapa wazazi wengi wanashindwa kutofautisha hizi hoja mbili kimajukumu jambo ambalo linasababisha wakidhani kuwa kumhudumia mtoto ndiyo kumlea jambo ambalo siyo kweli, wazazi au walezi wengi wanaishia kuwapa watoto yale mahitaji muhimu ya binadamu na wanaishia hapo lakini neno malezi ni pana sana kimajukumu, mbali na mahitaji hayo wanapaswa pia kugundua kipaji, tabia za watoto kwa kushirikiana nao kwa kila hatua.

Je' malezi ya wazazi/walezi yanawaandaaje watoto kuwa wazazi wazuri katika familia zao, jamii inayowazunguka na taifa kwa ujumla.

Basi ninaenda kueleza kwa kila hatua jinsi wazazi wanavyoshindwa kumlea mtoto katika misingi inayotakiwa pia namna sahihi ya malezi bora Ili tujenge Tanzania iliyo bora.

AINA YA MALEZI
- Malezi yenye miongozo iliyo wazi.

Hii ni aina ya malezi ambayo katika familia kuna miongozo ya uwazi inayohusisha wazazi wote wawili pamoja na watoto kushirikiana katika mambo mbalimbali na hatimae wazazi kugundua tabia mbalimbali za watoto wao na kuwaonya kwenye tabia zisizofaa.

Wazazi hupanga ratiba za watoto kuendana na mfumo wa maisha na watoto hufuata ratiba hizo kwa ajili ya faida ya makuzi yao.

Aina hii ya malezi ndiyo inayofaa kwenye jamii zetu kwa sababu huandaa vijana bora na wazazi bora wa baadae, wazazi au walezi wanapaswa kuishi katika familia ya aina hii ili kuokoa vizazi vijavyo.

-Malezi yenye ubaguzi na mabavu.

Haya ni yale malezi ambayo watoto wanalelewa kwa ubaguzi unakuta mama anapenda watoto wa kike pekee halafu wa kiume hawaoneshewi upendo wanaopaswa kupewa, mama anaenda sokoni kununua nguo za watoto wa kike tu ingali ana watoto wa kiume pia au muda wa kula mama anafanya ubaguzi watoto wa kike wanapewa mboga nzuri "masotojo" halafu watoto wa kiume hawapewi aina hiyo ya chakula, pia kwa mfano unakuta familia zingine mzazi anaonyesha mapenzi ya kweli kwa jinsia mmoja ya watoto mfano watoto wa kiume au wa kike hupewa maisha bora ingali wengine hubaguliwa.

Mabavu huonekana sana kwenye familia nyingi huku wazazi/walezi wengi wakiamini kuwa namna sahihi ya kumrekebisha mtoto pindi akoseapo ni kutumia kiboko na mtoto hupata kichapo cha kweli kutoka kwa mzazi na matokeo yake ni mtoto kuvishwa roho ya kikatili akiamini hamna upendo duniani.

-Malezi ya kudekeza.

Hii ni aina mbaya sana ya malezi kwa watoto kwani huzalisha vijana wazembe wasio wachapakazi na wapambanaji kutokana na aina ya malezi aliyokulia.

Familia za aina hii unakuta asubuhi mtoto huanza kwa kuamshwa na akiamka anakuta ameshaandaliwa kila kitu, amepashiwa maji ya kuoga, ameshapelekewa bafuni, ameshaandaliwa kifungua kinywa cha nguvu, baada ya kuogeshwa huvalishwa nguo, huchanwa nywele baada ya yote husindikizwa kwenye basi la shule na kuagwa kwa bashasha kwelikweli.

Aina hii ya malezi hudumaza akili na maendeleo ya watoto na hupelekea kuzalisha vijana wasio wachapakazi na wapambanaji, Kuna nyakati kwenye malezi inapaswa kumwacha mtoto afanye baadhi ya mambo mwenyewe na kujitatulia baadhi ya matatizo yake mwenyewe, mruhusu mtoto awe mdadisi Ili kujitengenezea ubunifu.

-Malezi ya kutokujali

Hii ni aina ya malezi ambayo watoto hulelewa kwenye maisha ya kutokupewa misingi muhimu ya kimalezi jambo linalopelekea watoto kuishi maisha ya kujihudumia tangu wakiwa kwenye umri wa kuhitaji usaidizi kutoka kwa wazazi au walezi.

Mambo yanayochagiza malezi ya aina hii ni kama wazazi kuachana kisha watoto kulelewa na watu baki pia kuongezeka kwa akina mama wanaofanya kazi za kuajiriwa husababisha watoto kutokulelewa na wazazi pia kuwategemea na kuwaamini wafanyakazi wa kazi za ndani maarufu kama "housegirl "pia ongezeko la matumizi ya simujanja na kompyuta husababisha wazazi kuwa bize na simu kuliko kuzingatia malezi ya watoto.

Jamii inatakiwa isiamini kwenye malezi yasiyo na faida kwa watoto wao Ili kuzalisha vijana na wazazi bora wa baadae, wazazi wasiamini sana kwenye matumizi ya viboko kwa watoto kwani mtoto anaelewa hata kwa kumwambia na kumwelekeza njia sahihi na njia isiyo sahihi vinginevyo watoto watakimbia nyumbani na kuwa na ongezeko kubwa la watoto wa mtaani, machokora, vibaka na wezi.

MAJUKUMU YA MSINGI YA MZAZI/MLEZI KWA MTOTO.
-Chakula bora.
Siyo kila chakula anachokula binadamu yapaswa kuitwa lishe bora, hivyo mzazi/mlezi anapaswa kuzingatia lishe Bora yenye mlo kamili.

-Malazi
Malazi ni faragha, uhuru, heshima na usalama. Malazi ni msingi muhimu wa starehe na furaha ya haki nyingi za kibinadamu.

-Mavazi
Wazazi/walezi wengi husema watoto hawana shida hata wakiwa uchi kwani hawajajua aibu ya kuwa uchi lakini huo niudhalilishaji wa kiutu.

-Malezi Bora
Mfumo wa maisha ya baadae ya mtoto yeyote ni matokeo ya mafunzo na malezi bora aliyopewa enzi ya utoto wake, pia wazazi wataigwa na watoto kwahiyo yawapasa kuishi maisha Bora.

-Ulinzi na usalama
Watoto wanapopewa ulinzi na usalama na wazazi wao hufurahia mazingira, maisha ya kijamii na mfumo wa utamaduni ndipo anapata nafasi ya kuishi, kupata riziki na heshima.

-Elimu Bora
Elimu bora kwa mtoto huchagizwa na kumchagulia shule bora yenye mazingira rafiki ya kujifunzia, pia kufuatilia maendeleo ya mtoto kimasomo, kushirikiana na waalimu wake na mwisho sapoti ya mzazi kwa mda wa ziada pale mtoto awapo nyumbani katika kumfundisha mambo mbalimbali.

WAJIBU WA SERIKALI
Serikali yapaswa kutengeneza mifumo rasmi mashuleni hususan shule za msingi na sekondari kufundisha masomo ambayo yanachochea uwazi, uzalendo, uwajibikaji na uadilifu Ili kuandaa kizazi bora cha baadae.

Serikali kwa kushirikiana na sekta binafsi yapaswa kuandaa semina za wazi kwenye serikali za mitaa hususan maeneo ya vijijini kwani ndiyo wahanga wakubwa wa malezi duni.

Serikali pia kwa kushirikiana na vyombo vya habari yapaswa kuandaa majukwaa rasmi yatakayochochea malezi bora kwenye jamii kwa maslahi mapana ya taifa.

HITIMISHO
Tatizo la malezi kwenye jamii nyingi za kitanzania imekuwa tatizo kubwa matokeo yake ni kuwa na vijana wasio na mawazo chanya kifikra na kupelekea ongezeko la familia maskini mjini na vijijini. Wito wangu kwa wadau ni kuhamasisha malezi bora kwenye jamii Ili kuokoa kizazi kijacho. MWISHO.
 
Tuzingatie malezi bora nduguzangu kwa maendeleo ya kesho
 
Kuna tofauti kubwa kati ya kumhudumia mtoto na kumlea mtoto, hapa wazazi wengi wanashindwa kutofautisha hizi hoja mbili kimajukumu jambo ambalo linasababisha wakidhani kuwa kumhudumia mtoto ndiyo kumlea jambo ambalo siyo kweli, wazazi au walezi wengi wanaishia kuwapa watoto yale mahitaji muhimu ya binadamu na wanaishia hapo lakini neno malezi ni pana sana kimajukumu
Vizuri kama hivi unapowaambia watu wakajua kuwa zipo tofauti. Ndio mwanzo wa kubadilika. Ahsante.
-Malezi Bora
Mfumo wa maisha ya baadae ya mtoto yeyote ni matokeo ya mafunzo na malezi bora aliyopewa enzi ya utoto wake, pia wazazi wataigwa na watoto kwahiyo yawapasa kuishi maisha Bora
Hakikaa

Tatizo la malezi kwenye jamii nyingi za kitanzania imekuwa tatizo kubwa matokeo yake ni kuwa na vijana wasio na mawazo chanya kifikra na kupelekea ongezeko la familia maskini mjini na vijijini. Wito wangu kwa wadau ni kuhamasisha malezi bora kwenye jamii Ili kuokoa kizazi kijacho. MWISHO.
Yaani hadi natamani, wazazi wangekuwa wanapewa kozi maalumu ya muda mfupi ya MALEZI kutoka ustawi wa jamii, wajue hata tuvitu tudogodogo hata saikolojia ya mtoto, makuzi na aina bora za malezi.

Maana wengine unakuta alipigwa mtama tu mimba. Sasa mtama hautoshi tunahitaji malezi, na mtama sio ulezi.
 
Wazazi hawajui hata jukumu la kugundua kipaji Cha mtoto ni chao, wanadhani ni jukumu la mwalimu shuleni
 
Back
Top Bottom