Tanzania inahitaji Rais Fyatu?

Aisee haya maombi siku Ingine tuachane nayo .

Nadhani mnaelewa kilichotokea
 
Kama kumbukumbu zangu ziko sawa. Wakati wa Magufuli ulikuwa supporter wake. Nashangaa now ni kama umemgeuka
Itakuwa kumbukumbu zako haziko sawa.

Hayati rais Magufuli alifanya baadhi ya mambo ambayo najivunia mpaka kesho kwayo. Nimehojiwa na baadhi ya Taasisi za kimataifa kuhusu Tanzania's approach on COVID-19 na mahojiano hayo yamerikodiwa (reference zipo), katika mahojiano hayo nimejivunia kuwa naongozwa na rais Magufuli. Namna serikali yake ilivyoliendea suala la COVID basi kwangu alistahili na anastahili pongezi za hali ya juu. Sitokutajia hayo mahojiano kwa sababu za privacy.

Ila pia hayati rais Magufuli alifanya mambo ya ajabu sana ambayo hakuna mtu au Mtanzania mwenye akili timamu, mpambanuzi na mwenye uelewa wa mambo atayakubali. Bahati mbaya mambo hayo mabaya yalikuwa mengi kuliko mema aliyoyafanya. Na hata hayo mema ukiyaangalia kwa undani basi kuna ukakasi wa hali ya juu.

Mfano, ununuzi wa ndege za Atcl kwa cash na bila kupitia bungeni lilikuwa ni suala linamlomtia doa sana.

Ujenzi wa airport ya chato lilikuwa ni suala baya sana ambalo kiongozi mwenye busara hakutakiwa hata kulifikiria.

Namna ya suala la korosho mwaka 2018 liligubikwa na ghiliba na sintofahamu nyingi sana.

Jaribio la mauaji ya Tundu Lissu akiwa kama kiongozi bungeni, na namna ambavyo serikali ililiendea suala lile ilikuwa haikubaliki.

Kupotea/kutekwa kwa baadhi ya watu prominent ambapo hali hiyo ilikuwa ina public interests na serikali yake kutofanikiwa kutoa majibu mazuri kwa wananchi ilionyesha udhaifu mkubwa sana. Mfano Mohamed Dewji.

Suala la wateule wake kufanya mambo kinyume na muongozo wa viongozi wa Umma halafu yeye kuamua kunyamaza iliichafua picha yake.

All in all, mimi sikuwa supporter wake kama unavyosema lakini alikuwa rais wangu niliyemheshimu. Nilimpongeza alipopatia na alipostahili pongezi na kumkosoa na kumshauri alipokosea.

Usinichukie mkuu!
 
10 Years later... Rais Magufuli ni raisi katili nchi haina furaha [emoji23][emoji23][emoji23] kummmae zenu Watanzania! Uliyotaka yote ameyafanya bila kupepesa macho ila mnamuita raisi dikteta
Watanzania wanaafiki sana
 
Hongera aseeh!ametunyoosha ingawaa as a human being alikua na flaws lakini alisimama kiume!
 
Umeandika mawazo yangu
 
Exactly huku mitaani ambako ndo wapiga kura wapo mama kashapoteza credit haraka sana...ingawa wafanyakazi tulokua tunaminywa tunamfurahia Ila 2025 uchaguzi mama ajipange wapiga kura ambao ndo Tabaka la chini na kati Maza washamchokaa mnooo na hivi hatumbui ndo kabisaa yaani,hasikilizi shida za wananchi kwenye mikutano hiloo ndo kabisaa yaani
 
Muongo sana ww. Hiyo survey umeifanya wapi? Chato na kwa wasukuma? Huku kwetu mama anakubalika 100%. Tukutajie mazuri aliyoyafanya kwa muda mfupi kila mmoja anamsifu?
 

Tulimpata, tukamchukulia for granted, ameondoka zake leo imepita miezi saba!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…