Tanzania inahitaji chama kipya cha upinzani chenye sera mbadala za kueleweka za kudumu kwa wananchi sio za matukio

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,906
51,924
Tanzania inahitaji chama kipya cha upinzani chenye sera mbadala za kueleweka za kudumu kwa wananchi sio za matukio.

Hivi vilivyopo hakuna hata kimoja chenye sera ya kudumu kinachoeleweka sera zake za kudumu hasa ni zipi.

Hivi vya kwetu havieleweki kabisa vinaenda na matukio tu.

Mfano CCM ikisema kila mtanzania lazima awe na shamba upinzani watakuja mbio kupinga na kutishia kuipeleka CCM Umoja wa Mataifa kwa kulazimisha kila mtu awe mkulima!!!

Lakini ukiwauliza vyama vya upinzani vyote kuwa hivi nyie sera zenu za kudumu ni zipi ambazo vyama vyenu vikitajwa tu mtu anajua yes hii ndio sera ya kudumu ya chama changu?
 
Labda pia wala hatuhitaji hicho Chama cha Upinzani, ukiniuliza mimi tunaweza kwenda hivi hivi tu.
 
Mfano CCM ikisema kila mtanzania lazima awe na shamba upinzani watakuja mbio kupinga na kutishia kuipeleka CCM umoja wa mataifa kwa kulazimisha kila mtu awe mkulima!!! Lakini ukiwauliza vyama vya upinzani vyote kuwa hivi nyie sera zenu za kudumu ni zipi ambazo vyama vyenu vikitajwa tu mtu anajua yes hii ndio sera ya kudumu ya chama changu?
Sidhani kama unajua ulichoandika ni vyema ukaacha mihemko wakati wa kuandika AU uwezo na upeo wako wa kupambanua mambo ni mdogo mno.

Ni bora ungekaa kimya kuficha ujinga wako.
 
Chama kipya cha upinzani cha nini sasa wakati wananchi kwa ujumla wetu kwa mamilioni tumeamua kwa dhati kabisa kuchagua CCM kuanzia ngazi ya Serekali za mitaa mwaka jana, Wabunge wote nchi nzima na hadi Rais?

Sasa badala wewe kada kufurahia nchi imekuwa ya kijani unanza kuota mambo ya vyama vipya vya Upinzani, umelogwa nini? Au huamini kama Wabunge wote sasa hivi ni CCM Nchi nzima?

Kuna vitu binadamu ukifanya lazima nafsi itakusuta tu! Kataa au kubali kada. Roho zenu hazijatulia kabisa yaani.
 
Labda pia wala hatuhitaji hicho Chama cha Upinzani, ukiniuliza mimi tunaweza kwenda hivi hivi tu.
Vyama vya upinzani TANZANIA tulikataa katakata tume iliyoundwa kuzunguka nchi nzima asilimia 82 ya waliohojiwa na tume mijini na vijijini walikataa kata kata vyama vingi

Nyerere alipopelekewa hiyo ripoti akasema ahhh hata kama wako wachache wanataka ruhusuni tu

Lakini ukitizama hadi leo msimamo wa watanzania walio wengi hawajabadilika hawataki vyama vingi

Hata vilivyoanzishwa vyote viianzishwa na wana CCM ambao walipigwa chini uongozi kwenye serikali na chama mihasira yao ndio wakapeleka kuanzisha vyama vya siasa

mfano CHADEMA kilianzishwa na MTEI NA BOB MAKANI wote walikuwa viongozi wa serikali waliopigwa chini na serikali

CUF ILIANZISHWA NA WAPIGWA CHINI, NCCR pia, NK
 
Si mnavyo vingi mmevianzisha na Sera mmevipa na speeches nini cha kusema na matamko yao mnawaandalia havitoshi tu hivyo?
Nini tena mnataka?

Haya ongezeni vingine!
 
Hata Upinzani wa aina gani bado hawataweza kuitoa CCM.

Ila CCM inatakiwa ijisafishe kwanza,ikiwezekana wabadilishe jina na nembo,viongozi wao wa juu kuanzia kata na kuendelea wafanyiwe semina hasa kwehemu ya kujiona bora kuliko wengine,kujua haki na heshima kwa kila mtanzania.

Lasivyo wakiendelea hivyo walivyo watakuja kugawanyika wenyewe na kitakacho wagawa ni tabia yao ya ubinafsi maana watajiona bora kuliko wengine hadi ndani ya chama na kwatabia hiyo watajisahau na watafikia hatua watawatenga watu kwa baadhi ya nyazifa fulan na kumbe kila mtu wakati huo ananguvu.

Mfano tumeona kwenye kula za maoni za mwaka huu,

Alieshinda anaenguliwa kwenye kupeperusha bendera anawekwa namba mwingine eti kwa kua anajina kubwa,hapa wanatengeneza tatizo ambalo linatoa matokeo mabaya kwa muda mrefu bila kujua.

Wasipoangali hata kupotezana wenyewe kwa wenyewe itakua sio ajabu.

Yote kwa yote,Taasisi, Kampuni, Timu, nk
Ikikaa saana na nembo au jina la aina moja kunawakati itafikia inakosa mvuto.
 
Kwa sasa Tanzania inahitaji Katiba mpya na Tume huru ya Uchaguzi basiiiiiiii, kama vyama vya siasa vipo zaidi ya 20, bila Tume huru ya Uchaguzi chaguzi zote zitakazo fannyika ni 'ze comed'
 
Watanzania wanataka maendeleo sio brah brah za vyama vya upinzani, kwanza uchaguzi umekwisha.
 
Vyama vya upinzani TANZANIA tulikataa katakata tume iliyoundwa kuzunguka nchi nzima asilimia 82 ya waliohojiwa na tume mijini na vijijini walikataa kata kata vyama vingi

Nyerere alipopelekewa hiyo ripoti akasema ahhh hata kama wako wachache wanataka ruhusuni tu

Lakini ukitizama hadi leo msimamo wa watanzania walio wengi hawajabadilika hawataki vyama vingi

Hata vilivyoanzishwa vyote viianzishwa na wana CCM ambao walipigwa chini uongozi kwenye serikali na chama mihasira yao ndio wakapeleka kuanzisha vyama vya siasa

mfano CHADEMA kilianzishwa na MTEI NA BOB MAKANI wote walikuwa viongozi wa serikali waliopigwa chni na serikali

CUF ILIANZISHWA NA WAPIGWA CHINI,NCCR pia,NK
Wewe mwendawazimu, kama tulikuwa hatuna vyama vingi,ulitaka watu wakuanzisha vyama vya upinzani watoke wapi? Chama ni watu na itikadi, sio masuala ya katoka wapi!

Nakushauri wewe ridhika na CCM yako, ya upinzani tuachie wenyewe!
 
Chadema CCM tutakayobaki kuikumbuka ni ile ya kipindi cha DK Slaa iliyokuwa na hoja ya kupambana na ufisadi ,Rushwa na uzembe kazini.Hii Chadema yenu ya ushoga wa akina Amsterdam na ya kuweka rehani madini yetu kwa wazungu hatuihitaji itokomee kuzimu na hatuikumbuki
Dr Slaa yule ingekuwa ni awamu hii, angekuwa ameshauwawa!
 
Kwa sasa Tanzania inahitaji Katiba mpya na tume huru ya uchaguzi basiiiiiiii, kama vyama vya siasa vipo zaidi ya 20, bila tume huru ya uchaguzi chaguzi zote zinatakazo fannyika ni 'ze comed'

Na hapo ndipo mwizi aliposhika mavi.

Kukwiba hadi Lipumba kasusa Uchaguzi bila kuwa na Katiba mpya na tume huru.

Wamewaamsha hadi CUF na kina mama Tanzania.

Yajayo yanafurahisha!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom